SHEIKH JALALA ATOA NENO KUELEKEA MAADHIMISHO YA KUZALIWA MTUME MUHAMMAD


Ikiwa zimebaki siku chache kufikia maadhimisho ya kuzaliwa Mtume Muhammad Kiongozi wa waislam wa madhebu ya shia Ithnashariya  Tanzania  Shekhe Hemed  Jalala amewataka  watanzania kuwa na tabia ya kuhurumiana hasa wenye uwezo kuwahurumia wasio na uwezo.


Akizungumza na waandishi wahabari Leo katika ukumbi wa habari maelezo Jijini Dar es salaam amesema Mtume Mohammad alifundisha kuwa dini imekuja kutunza Upendo na amani hivyo nivyema waTanzania  kuishi kwa Upendo bila kujali utofauti wa dini zao.

"Mtu kupenda nchi ni katika amani na pia dini imekuja kutunza upando na amani watanzania tusibaguane kutokana na dini zetu" amesema Jalala.

Hata Hivyo Sheikh Hemed amebainisha kuwa ni vyema jamii kuyaishi maisha aliyoishi Mtume Mohammad ikiwa ni pamoja na sifa kuumbili alizokuwa nazo Mtume ambazo  nikuwa mkweli na mwaminifu.

Sambamba na hayo ameongeza kuwa Kazi kubwa inayotakiwa kufanywa na watanzania hasa kwa kipindi hiki chakukumbukwa kwa kuzaliwa kwa Mtume ni kuishi kwa amani na ushirikiano kwa kuwa vitabu vyote vya dini vimekuja kuunganisha watu.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.