Friday, December 2, 2016

TAARIFA MBALIMBALI KUTOKA POLISI KANDA MAALUM DAR ES SALAAM


POLISI DAR YAWAKAMATA WATUHUMIWA SUGU 586


Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar Es salaam limefanya msako mkali kuanzia tarehe 22.11.2016  hadi 02.12.2016 na kufanikiwa kuwakamata jumla ya watuhumiwa sugu 586 wa makosa mbalimbali. Watuhumiwa hao wamekamatwa maeneo mbalimbali kwa nyakati tofauti tofauti. Wamekamatwa kwa makosa ya unyang’anyi wa kutumia nguvu,kuvunja nyumba usiku na kuiba, wizi kutoka maungoni, kucheza kamari, kubughudhi abiria, wizi wa magari, wizi kutoka maungoni, shambulio la aibu na la kawaida, kutengeneza,kuuza na kunywa pombe haramu ya Gongo, uvutaji bhangi nk


Operesheni iliyofanyika Buguruni na Magomeni jumla ya watuhumiwa 257 walikamatwa kwa makosa mbalimbali  na jumla ya lita 405 za Pombe haramu za Gongo  zilikamatwa, Mitambo miwili ya kutengenezea gongo na bhangi. Aidha  baadhi ya watuhumiwa hao walikutwa silaha ndongo ndogo za kufanyia uhalifu kama: Visu, nyembe, bisibisi nk. Baadhi ya watuhumiwa majina yao ni: (1) MARIA NGUTU (81) kabila Mzanaki mkazi wa Kiwalani alikutwa  na gongo lita 200, (2) BENSON RICHARD(43) kabila Mjita alikutwa na lita 50 za Gongo mkazi wa Kiwalani, nk.

KUKAMATWA KWA GARI AINA YA TOYOTA HIACE IKIWA IMEBEBA MALI YA MBALIMBALI ZA WIZI

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar Es salaam kupitia kikosi kazi chake cha kupambana na ujambazi wa kutumia silaha, mnamo Tarehe 29/11/206 majira ya saa nne na nusu huko Kijichi Neluka Mbagala wezi 03 wakiwa na gari no T.129 DDS Noah rangi ya fedha walivamia baa moja inayofahamika kwa jina la Whatsapp na kuvunja kisha kuiba vitu mbalimbali kama ifuatavyo;
 TV flat screen 01 aina ya Samsung, king’amuzi cha startimes kimoja, Radio 01, spika 02 aina ya sony, na Glass katoni 03.

Askari wa kikosi maalum wakiwa doria maeneo ya jirani na tukio, walisikia milio ya risasi  na kuwahi eneo la husika kwa haraka.

Walipokaribia eneo la tukio walifanikiwa kuiona gari hiyo ikiwa inakimbia kwa kasi. Askari walifyatua risasi hewani huku wakiwataka watuhumiwa hao wasimame, lakini majambazi hao hawakusimama na  kuendelea kukimbia.
 Ndipo walikosa mwelekeo na kugonga mti na gari hiyo kusimama hapo hapo na wao wakatokomea gizani kwa miguu.

Askari walifika kwenye Gari hiyo na kuipekua  vilipatikana vitu vyote vilivyoibiwa kwenye baa hilo.

Jitihada za kuwakamata watuhumiwa hao unaendelea
POLISI KANDA MAALUM DSM WAKUSANYA TSH 878,670,000/= KUPITIA TOZO ZA MAKOSA YA USALAMA BARABARANI
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dsm kupitia kikosi chake cha usalama barabarani kimekamata makosa mbalimbali ya usalama barabarani kwa kipindi cha siku nne  kuanzia tarehe 21/11/2016 hadi tarehe 02/12/2016 na kuingizia serikali mapato ya ndani kama ifuatavyo;
1.     Idadi ya magari yaliyokamatwa                            - 9,817
2.    Idadi ya Pikipiki zilizokamatwa                             - 708
3.    Daladala zilizokamatwa                                        - 3,268
4.    Magari mengine (binafsi na malori)                        - 6,548
5.    Bodaboda waliofikishwa Mahakamani
kwa makosa ya kutovaa helmet na
kupakia mishkaki                                                 -
6.    Jumla ya Makosa yaliyokamatwa                             -  29,289

Jumla ya Fedha za Tozo zilizopatikana TSH 878,670,OOO/=

Aidha ukaguzi wa magari na utoaji wa stika unaendelea katika vituo vya Polisi kikosi cha usalama barabarani na wananchi wapeleke magari yakakaguliwe katika vituo hivyo.


S.N.SIRRO - CP
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM

DAR ES SALAAM

No comments: