WAMILIKI WA BLOG TANZANIA KUKUTANA WIKI IJAYO,NMB YADHAMINI MKUTANO HUO

Chama cha  Wamiliki/Waendeshaji mitandao ya kijamii nchini (Tanzania Bloggrs Network-TBN) mapema leo Disemba, 2 imekabidhiwa  cheki maalum ya kiasi cha Tsh. Milioni 10, fedha zilizotolewa na  benki ya NMB kama wadhamini wakuu wa Mkusanyiko wa ‘Bloggers’ kutoka maeneo mbalimbali ya mikoa ya Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar.
Katika tukio hilo, Mwenyekiti wa muda wa TBN, Bwana Joachim Mushi amepongeza benki ya NMB kwa kuweza kudhamini tukio hilo muhimu na la kihistoria kwani litasaidia wana blogger kwa ujumla kuweza kukutana pamoja na kujifunza kile ambacho wanapaswa kuwahabarisha Umma kupitia blog zao.
“Tunawapongeza benki ya NMB  kwa udhamini huu na tunawaomba sana waendelee kutudhamini kwani kazi iliyopo mbele yetu kwa sasa ni kutoa elimu sahihi kwa wenzetu ambao watajumuika katika mkutano huu utakaofanyika siku mbili yaani 5 na 6 Desemba,2016. Kwa washiriki takribani 150 kutoka Tanzania  nzima ambapo pia tukio hilo litafuatiwa na mkutano mkuu kwa wanachama hai wa TBN  na kujadili mambo mbalimbali,” alieleza Joachim Mushi.
Ofisa Uhusiano wa NMB, Doris Kilale amesema kuwa wataendelea kushirikiana na Tanzania Bloggers Network-TBN kwani inaamini kufanya hivyo ni moja ya njia ya kufikisha ujumbe kwa jamii hasa kupitia mitandao ya kijamii.
“NMB imekuwa mstari wa mbele katika kushirikiana na wadau wa habari mbalimbali na sasa tunashirikiana na TBN  na tumeweza kutoa kiasi cha Shilingi milioni 10 kwa ajili ya mkutano wao wa mwaka utakaofanyika 5 na 6 Desemba  mwaka huuna. Pia kama munavyofahamu kuwa NMB ipo karibu yako hivyo kupitia mitandao ya kijamii na Blog itaendelea kufikisha habari zetu kwa jamii kwa wigo mpana zaidi.” alieleza Ofisa Uhusiano huyo, Doris Kilale.
Mkutano huo unatarajia kufanyika jijini Dar es Salaam hiyo 5 na 6 Desemba katika ukumbi wa wa mikutano wa makao makuu ya jengo la Golden Jubilee PSPF.
Aidha, mbali na Benki ya NMB kuwa wadhamini wakuu katika tukio hilo, pia wadhamini wengine ni pamoja na  NHIF,SBL, PSPF na  Coca Cola ambao wote kwa pamoja wamejitokeza kufanikisha katika tukio hilo.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.