Waziri Nape afunga Mkutano Mkuu wa Waandishi wa habari za Mitandao 'Tanzania Bloggers Network' (TBN),ahidi kuanzisha tuzo.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akitoa Ufafanuzi wakati alipokuwa akieleza namna ya kuitambua mitandao ya Kijamii pamoja na uanzishaji wa Tuzo kwa Waendeshaji mitandao hiyo.
Waziri Nape alisema kuwa lengo la tuzo hizo ni kuzisaidia blogs za Tanzania kubobea katika nyanja tofauti ikiwemo kilimo, mifugo, viwanda, hifadhi ya jamii kwa nia ya kuipa heshima tasnia ya habari nchini.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye wakati akizungumza mapema leo jijini Dar wakati akifunga Mkutano Mkuu wa Tanzania Bloggers Network (TBN) iliokwenda sambamba na semina ya wanachama wa umoja wa waendeshaji wa blog nchini.Picha na Michuzi Jr.

 Na Beatrice Lyimo, Maelezo
Serikali inatarajia kuanzisha tuzo za umahiri kwa waandishi wa habari wa mitandao ya kijamii (blogs) nchini kuanzia mwaka 2017.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar  es salaam na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye wakati akifunga Mkutano Mkuu wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na semina ya wanachama wa umoja wa waendeshaji wa blog nchini.

Waziri Nape alisema kuwa lengo la tuzo hizo ni kuzisaidia blogs za Tanzania kubobea katika nyanja tofauti ikiwemo kilimo, mifugo, viwanda, hifadhi ya jamii kwa nia ya kuipa heshima tasnia ya habari nchini.

Aidha, Waziri Nape alisema kuwa tayari Serikali imeanza mazungumzo na   makampuni na taasisi mbalimbali kwa ajili ya kudhamini tuzo hizo ili kuhakikisha kuwa washindi wanapatikana kwa uwazi.

“Tuzo hizo zitakuwa za kwanza kwa namna zitakazovyoendeshwa kwa uwazi hivyo makampuni zaidi yanakaribishwa kuweza kuzidhamini mashindano hayo yatakayojielekeza kwenye nyanja tofauti” alisema Waziri Nape.

Waziri Nape pia alisema amewataka wamiliki na watendaji wa blogs nchini kushirikiana na Serikali ili kuweza kuijenga nchi.

“Tutumie fursa za kisiasa zilizopo, fursa za teknolojia ili kuhakikisha tiunajenga Tanzania tunayoitaka, ishaurini Serikali kwa kutumia taaluma mliyonayo ili kuweza kuipeleka nchi ya Tanzania tunayoitaka” alifafanua Waziri Nape.
Mwenyekiti wa Muda wa chama cha Waendesha mitandao ya Kijamii Tanzania Bloggers Network-TBN,Joachim Mushi akimkaribisha mgeni rasmi,Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kwa ajili ya kufunga mkutano huo na pia kuyotolea ufafanuzi baadhi ya mambo

Mmoja wa Wajumbe wa mkutano huo,Mzee John Kitime ambaye amebobea katika mambo ya Hakimiliki,akitoa elimu ya mambo ya Hakimiliki kwa washiriki wa mkutano huo.

Baadhi ya Waendeshaji wa mitandao hiyo wakiwa kwenye mkutano wao wa Mwaka wakifuatilia yaliyokuwa yanaendelea
Baadhi ya Wadau wakiendelea kusikiliza yaliyokuwa yakiendelea ukumbini humo.
Baadhi ya Waendeshaji wa mitandao hiyo wakiwa kwenye mkutano wao wa Mwaka wakifuatilia yaliyokuwa yanaendelea

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.