Zitto Kabwe kaandika alichofwata Arusha,Na maelekezo aliyopewa na Mbunge LemaZiara Yangu Mkoani Arusha 
Leo mchana nilikuwa mkoani Arusha Kwaajili ya kutekeleza majukumu na kazi zangu kama Mbunge wa jimbo la Kigoma Mjini (Ujiji). Ziara yangu mkoani Arusha ilikuwa makhsus kwaajili ya kutembelea Chuo cha Kilimanjaro International Information Technology & Computing College (KIITEC).
Jimboni Ujiji tuna lengo la kuwa na chuo cha Ufundi cha namna hii, kwa lengo la kuwajengea uwezoa vyuo vya aina hii. Nawashukuru sana KIITEC, nimejifunza, Ujiji tutajitahidi kuiga jambo hili zuri la watu wa Arusha.
na kuwaongezea maarifa vijana wetu kupitia kozi mbalimbali zinazotolewa n

Pia, nilipata fursa ya kumsalimu Mbunge mwenzangu wa jimbo la Arusha Mjini, ndugu Godbless Lema, gerezani Kisongo. Nimefurahi kumkuta akiwa na ari kubwa na asiyekata tamaa.
Ujumbe wake kwangu ni kuwa yeye yu tayari kukaa mahabusu kwa muda wote ambao Serikali itaona inafaa, na akaniasa nisimpiganie kwenye hili, bali nilitazame kwa upana kwa kuwa wapo watanzania wengi mno wanaokaa muda mrefu sana mahabusu kwa kesi ambazo wangeweza kupewa dhamana. Amenihimiza tujikite katika kuwatetea hawa. Ombi ambalo nimeahidi kwake kulitekeleza.
Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Arusha
Disemba 2, 2016

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.