Monday, February 29, 2016

Freeman Mbowe atoa vielelezo 2 vya serikali kupora demokrasia.


Mwenyekiti wa Umoja huo Freeman Mbowe amesema hayo kwenye Ibada ya Kuchangia kwenye kanisa la KKKT ,Nshara Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro na kuongeza kuwa suala la Uchaguzi wa Zanzibar na kusuasua kwa uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam, ni vielelezo vya serikali kupora demokrasia.
Aidha Mwenyekiti huyo Mwenza wa Umoja huo, amesema kuwa uvumilivu una mwisho hivyo ameitaka serikali kuacha kutumia nguvu katika masuala ya kuwatumikia wananchi na kuwapa uhuru wa maamuzi wanayoyataka.

Mhe. Mbowe amesema kuwa Chama cha Mapinduzi kimeonyesha kushindwa katika chaguzi kadhaa lakini kinalazimisha kuendelea kushikilia madaraka kwa nguvu hasa kwenye chaguzi za Mameya ikiwemo Uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam.

TAFRIJA YA MCHAPALO WA UZINDUZI WA INTANETI YA KASI ZAIDI YA TIGO 4G MKOANI KILIMANJARO YAFANA


Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini, George Lugata akiongea na wageni waalikwa na wanahabari wakati wa hafla ya uzinduzi wa  intaneti yenye kasi ya Tigo 4G LTE mkoani Kilimanjaro juzi.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara kampuni ya Tigo(B2B), Rene Bascope akiongea na wageni waalikwa na wanahabari wakati wa hafla ya uzinduzi wa  intaneti yenye kasi ya Tigo 4G LTE mkoani Kilimanjaro juzi.

MASHINDANO YA TIGO KILI HALF MARATHON YAFANA MJINI MOSHI

Maelfu ya wakazi wa Moshi na wanariadha mbalimbali wakifuatilia  mashindano ya Tigo Kili Half Marathon  katika mashindano hayo yaliyofanyika jana kwenye viwanja vya chuo cha Ushirika Mjini Moshi  
Wafanyakazi wa  kampuni ya Tigo wakiwa katika picha  ya pamoja  kabla  ya kuanza    mashindano ya Tigo Kili Half Marathon  katika mashindano hayo yaliyofanyika jana kwenye viwanja vya chuo cha Ushrika Mjini Moshi  
 Waziri wa habari, utamaduni, Sanaa na michezo Mhe. Nape mnauye  ( katikati mwenye kofia) akisubiri kufungua mbio za Tigo Kili half Marathon 2016, mkoani Kilimanjaro, kulia kwake  Meneja masoko Olivier prentout  atika mashindano hayo yaliyofanyika jana kwenye viwanja vya chuo cha Ushrika Mjini Moshi .
Wanariadha wa Tigo Kili half Marathon wakisubiri kuanza mbio   katika mashindano ya Tigo Kili Half Marathon  katika mashindano hayo yaliyofanyika jana kwenye viwanja vya chuo cha Ushrika Mjini Moshi  

WADAU WAAANZA KUJENGA UELEWA KUHUSU SIKU YA MAGONJWA YANAYOTOKEA KWA KUNDI DOGO LA JAMII



Wadau hao wakinyoosha mikono juu kuonesha umuhimu wa kuadhimishwa kwa siku hiyo ya Magonjwa Yanayotokea kwa kundi dogo la jamii ndani ya jamii.

MAKAMU WA RAIS MSTAAFU DKT. BILAL AKABIDHI ZAWADI ZA WASHINDI WA MASHINDANO YA KUTAFUTA WAWAKILISHI WA NCHI KATIKA MASHINDANO YA KIMATAIFA YA QUR’AN TUKUFU.


bil1

Makamu wa Rais mstaafu  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa mashindano ya kumtafuta mwakilishi wa Nchi atakayeiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Kimataifa ya Qur’aan Tukufu, yaliyoandaliwa na Kamati Maalum chini ya Mwenyekiti wake Saleh Omary, yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, jana Feb 28, 2016. Picha na Mafoto Blog
bil2
Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi, mshindi wa kwanza wa Mashindano ya kumtafuta mwakilishi wa Nchi atakayeiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Kimataifa ya Qur’aan Tukufu, Rajai Ayoub, aliyepata pointi 95 kwa upande wa Tajweed, wakati wa mashindano hayo yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, jana Feb 28, 2016. Mashindano hayo yameandaliwa na Kamati maalum chini ya Mwenyekiti wake, Saleh Omary. . Kushoto ni Balozi wa Iran nchini Tanzania, Mahd Aghajafar . Picha na Mafoto Blog

WAZIRI MKUU AAGIZA DAKTARI ASIMAMISHWE KAZI


MTW1

Wamawake wakiwa wametandika khanga kwenye wodi ya wazazi ya Hospitali ya Mkoa wa Mtwara, Februari 29, 2016.Waziri Mkuu, Kassim majaliwa alitembelea wodi hiyo na kukemea mtindo huo akiwataka wauguzi na waganga kutandika mashuka yahospitali ambayo alisema ana taarifa kuwa yapo ili kuepusha hatari ya wananwake hao kubeba magonjwa kupitia kahanga hizo watokapo hospitalini hapo.(Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
mtw2
Wamawake wakiwa wametandika khanga kwenye wodi ya wazazi ya Hospitali ya Mkoa wa Mtwara, Februari 29, 2016.Waziri Mkuu, Kassim majaliwa alitembelea wodi hiyo na kukemea mtindo huo akiwataka wauguzi na waganga kutandika mashuka yahospitali ambayo alisema ana taarifa kuwa yapo ili kuepusha hatari ya wananwake hao kubeba magonjwa kupitia kahanga hizo watokapo hospitalini hapo.(Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
mtw3
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea hospitali ya Mkoa wa Mtwara Februari 29, 2016. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Halima Dendego na kulia Ni Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dkt.Shaibu Maarifa.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
mtw4
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea hospitali ya Mkoa wa Mtwara Februari 29, 2016. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Halima Dendego na kulia Ni Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dkt.Shaibu Maarifa.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
mtw5
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza na Waganga, Wauguzi na wafanyakazi wa Hospitali ya Mkoa wa Mtwara wakati alipoitembelea Februari 29, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
mtw6
Baadhi ya Wauguzi na Madaktari wa Hospitali ya Mkoa wa Mtwara wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao hospitalini hapo Februari 29, 2016. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
mtw7
Waziri Mkuu, Kassim majliwa akitoa agizo la kusimamishwa kazi Daktari wa Hospitali ya Mkoa wa Mtwara, Fortunatus Namahala (kulia)  baada ya kutajwa kuwa alidai rushwa ya sh.100, 000/= ili aweze kumtibu baba mzazi wa Tatu Abdallah (wapili kulia) wakati alipoitembelea hospitali hiyo Februari 29, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
mtw8
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akiagana na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Mtwara, Shaibu Maarifa kwenye uwanja wa ndege wa Mtwara kabla ya kurejea Dar es slaam Februari 29, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
mtw9
Waziri Mkuu, Kassim majaliwa akitazama ngoma  kwenye uwanja wa ndege wa Mtwara kabla ya kuondoka  kurejea Dar es salaam Februari 29, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MKE WA RAIS MSTAAFU NA MWENYEKITI WA WAMA ASISITIZA UMUHIMU WA CHAMA CHA GIRL GUIDE TANZANIA KUONGEZA WANACHAMA


WAMA1

Mke wa Rais Mstaafu na Mwenyekiti wa WAMA akisalimiana na Mama Othman Chande alipowasili katika Shule ya Sekondari Tambaza kuhudhuriaWorld Thinking Day iliyoandaliwa na Tanzania Girl Guide Association.
WAMA2
Wanachama wa Girl Guide wakiwasili katika Shule ya Sekondari Tambaza  katika kusherekea World Thinking Day  ambao walipokelewa na Mgeni Rasmi Mama Salma Kikwete.
WAMA3
Mama Salma Kikwete akiingia katika ukumbi wa Tambaza Sekondari akiwa na viongozi wa Girl Guide kushoto ni Mama Symphorosa Hangi, Kamishna Mkuu  na kulia ni Mama Matilda Balama na Mkuu wa Shule ya Tambaza.
WAMA4
Picha ya Pamoja na Mgeni Rasmi  na baadhi ya wanafunzi Wanachama na viongozi wa  Girl Guide
WAMA5
Mama Salma Kikwete akiangalia kazi za wakinamama wajasiriamali ambao walifanya maonyesho katika sherehe hizo
PICHA NA YUSUPH BADI
………………………………………………………………………………………………………………….
Na Philomena Marijani- Meneja Uraghbishi na Mawasiliano, WAMA
Chama cha Girl Guide Tanzania kimetakiwa kuweka mikakati ya kuhakikisha inaongeza wanachama watakaojiunga na chama hicho ili vijana wengi waweze kunufaika
Rai hiyo imetolewa mwishoni wa wiki na Mke wa Rais Mstaafu na  Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA, Mama Salma Kikwete wakati wa maadhimisho  ya kilele cha  siku ya  World Thinking Day yenye kauli mbiu ya Ungana, Shirikiana, Sherekea  iliyoadhimishwa na Tanzania Girl Guides Association. Sherehe hizo zilianza kwa maandamano ya wanafunzi Wanachama kutoka Upanga katika Makao Makuu ya Girl Guide Tanzania na kumalizikia  katika Shule ya Sekondari Tambaza ambapo  sherehe rasmi ilifanyika hapo.
Akiongea katika sherehe hizo Mama Salma Kikwete  alipongeza uongozi wa Girl Guide  kwa kufikia mikoa 19 ambapo  mpaka sasa chama kina  wanachama 97,143 na aliongeza kuwa changamoto kubwa waliyonayo ni kuongeza Wanachama zaidi kwani Tanzania ina watu wengi sana.
“Wito wangu kwenu ni kuongeza juhudi ya kuwafikia vijana wengi zaidi kwani sote tunajua umuhimu wa TGGA katika kuwasaidia vijana kujiepusha na changamoto mbalimbali katika makuzi yao. Ni lazima tuweke malengo ya muda mfupi, kati na mrefu ndani ya miaka mitatu ili ifikapo  mwaka 2018 tuwe tumeingiza wanachama zaidi ya 100,000/= Tumieni vizuri shule za msingi na sekondari , nina hakika mtafanikiwa kwa kiasi kikubwa sana. ” Alisema Mama Kikwete
Mama Kikwete pia alishauri uongozi wa Girl Guide Tanzania kubuni mbinu za kukabiliana na changamoto kwa kutumia rasilimali walizonazo.
“Kwa kuwa TGGA ni chama kikongwe, chenye rasilimali kama ardhi ambazo ziko sehemu nzuri kibiashara  naamini kwamba ikitayarishwa mipango mizuri  mnaweza kupata wabia wenye tija au mkawekeza kama chama kwa kushirikiana na mabenki. Mtakusanya kodi ambazo zitasaidia uendeshaji na kuongeza uwekezaji. ”Alisema Mama Kikwete.
Akielezea maana ya World Thinking Day Mkufunzi wa Taifa wa Tanzania Girl Guide Association, Mama Magreth Olumbe alisema kuwa sherehe hii ilianza rasmi mwaka 1926 ambayo ni siku ya; kuwakumbuka Girl Guide wote duniani na hasa wale walio kwenye mazingira magumu;kuongelea mambo yanayowagusa wasichana kwa mfano mimba za utotoni, kuolewa katika umri mdogo; na kukumbuka mwanzilishi wa Chama Lord Baden Powell na mke wake Olave Baden Powell.  
Akisoma risala kwa Mgeni Rasmi, Kamishna Mkuu wa  Tanzania Girl Guides Association, Mama Symphorosa Hangi alisema kuwa katika kuadhimisha  World  Thinking Day walikuwa na wiki mbili za kutoa huduma kwa jamii ikiwemo kuwatembelea wagonjwa katika hospitali ya Ocean Road na kutoa chakula, mavazi   na nauli za kuwarudishwa makwao wale waliokuwa wameruhusiwa baada ya matibabu. Aliongeza pia walitumia muda huo kuhamasisha wasichana wengine kujiunga na chama cha Tanzania Girl Guides ili nao waweze kupata fursa ya kujikwamua kifikra kwa kupitia mafunzo yanayotolewa na chama.
Chama cha Girl Guides Tanzania (TGGA) kilianzishwa hapa nchini mwaka 1928. TGGA ni chama kisicho cha serikali na ni cha kujitolea chenye lengo la kuwaendeleza watoto wa kike na wanawake kwa ujumla kushiriki katika maswala ya kijamii na kiuchumi kwa kupitia elimu na mafunzo yanayotolewa kwa kuzingatia kanuni za Girl Guides pamoja na kuwajenga kimaadili.

BWENI LA WAVULANA SHULE YA SEKONDARI IYUNGA JIJINI MBEYA LATEKETEA KWA MOTO


Muonekano wa bweni la Wavulana katika shule ya sekondari Iyunga jijini Mbeya mara baada ya kuteketea kwa moto uliosababishwa na hitilafu ya umeme majira saa3 asubuhi ambapo hakuna mwanafunzi yeyote aliyejeruhiwa kutokana na ajali hiyo ya moto. .
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Nyirembe Munasa mwenye suti akisaidiana na kikosi cha Zima moto kuuzima moto ulioteketeza Bweni la wavulana katika shule ya sekondari ya Iyunga jijini Mbeya linalolaza wanafunzi 95 February 29 mwaka huu ambapo hakuna  
 
 
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Nyirembe Munasa akizungumza na Walimu pamoja na wanafunzi (hawapo pichani )katika shule ya sekondari Iyunga jijini Mbeya mara ya baada ya kukumbwa na tukio la kuungua kwa moto kwa mabweni ya wavulana ya (Mkwawa) February 29 mwaka huu.
Kamati ya ulinzi na Usalama wilaya ya  Mbeya na baadhi ya viongozi wakitizama athari zilizotokea mara baada ya mabweni ya wavulana katika shule ya sekondari Iyunga jijini Mbeya kuungua moto uliosababishwa na hitilafu ya umeme February 29 mwaka huu .
Afisa elimu Mkoa wa Mbeya Charles Mwakalila akizungumzia athari zilizojitokeza mara baada ya mabweni ya wavulana katika shule ya sekondari ya Iyunga jijini Mbeya ambayo yaliteketea kutokana na hitilafu ya umeme majira ya saa3 asubuhi wakati wanafunzi wakiwa madarasani .
 
Baadhi ya wanafunzi waliofanikiwa kuokoa vifaa vyao kwa masaada wa watu wa zima moto wakiwa nje wakisubiri utaratibu mara baada ya bweni lao kuteketea kwa moto.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa  nje kusbiri utaratibu mara baada  waliofanikiwa kuokoa baada ya bweni lao kutektea kwa moto.Picha na David Nyembe