Saturday, April 30, 2016

MWENYEKITI WA MTAA ATAKAYESHINDA KWA KUFANYA USAFI KATIKA MTAA WAKE KUIBUKA NA MILIONI 50.000.000

????????????????????????????????????
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akiongozana na Mwanamuziki Diamond Plutnamz pamoja na Mkurugenzi wa Vipindi na Utafiti Clods FM Bw. Ruge Mutahaba wakati wa matembezi ya mshikamano kwa ajili ya uzinduzi rasmi wa kampeni ya usafi wa jiji la Dar es salaam itakayofanyika kwa siku 90 ikishirikisha wenyeviti wa mitaa,  wananchi katika maeneo yao, Taasisi za Serikali na Mashirika Binafsi ili kuhakikisha jiji la Dar es salaam linakuwa safi kabisa.
Makonda amewaambia wananchi mara baada ya matembezi hayo kwamba Dar es salaam bila uchafu inawezekana na amenzisha shindano kwa wenyeviti wa mitaa iliyopangwa na isiyopangwa mwenyekiti atakayeshinda kwa usafi katika eneo lake atajishindia shilingi milini 50.000.000 na mwenyekiti atakayekuwa wa mwisho katika eneo lake atapata nafasi ya kutangazwa katika vyombo mbalimbali vya habari kuhusiana na uchafu uliopo katika eneo lake na wananchi wake na pia mazingira hayo machafu yataonyeshwa yakiambatana na picha za mwenyekiti huyo.
????????????????????????????????????
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akiongozana na Mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Raymond Mushi na Mkurugenzi wa Vipindi na Utafiti Radio Clods Bw. Ruge Mutahaba na Mwanamitindo Millen Magesse ambaye pia ameshiriki kikamilifu katika kampeni hiyo
????????????????????????????????????
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akiongozana na Mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Raymond Mushi na Mkurugenzi wa Vipindi na Utafiti Radio Clods Bw. Ruge Mutahaba na Mwanamitindo Millen Magesse ambaye pia ameshiriki kikamilifu katika kampeni hiyo
????????????????????????????????????
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akiongozana na Diamond Plutnamz huku ulinzi ukiwa umeimarishwa wakati wa matembezi hayo yaliyofanyika leo kwa ajili ya kuhamasisha wakazi wa jiji la Dar es salaam kufanya usafi katika maeneo yao.????????????????????????????????????Haya ni miongozi mwa matukio yaliyojiri wakati wa matembezi hayo ya kuhamashiwa wakazi wa jiji kufanya usaifi ambapo kampeni maalum ya siku 90 za kufanya usafi zimezinduliwa na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda.
????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
Wapiga picha waliendelea na ubunifu wa kutafuta picha nzuri kama wanavyoonekana hapa kwenye picha wakiwa kwenye pikipiki wakipiga picha katika matembezi hayo.
????????????????????????????????????
Baadhi ya washiriki wa matembezi hayo wakifanya mazoezi mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam ambako ndiko kampeni hiyo ilikozinduliwa.
????????????????????????????????????
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akishiriki katika mazoezi hayo mara baada ya mtembezi hayo kuwasili katika viwanja vya Leaders Kinondoni jijini Dar es salaam.
????????????????????????????????????
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akisalimiana na viongozi wa dini waliofika katika uzinduzi wa kampeni hiyo ambao ni Sheikh Mkuu wa Dar es salaam Sheikh  Alhadi Mussa Salim na  Askofu  David  Mwasota kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally  Hapi????????????????????????????????????Kikundicha ngoma kikitumbuia katika uzinduzi huo
12Kundi la Yamoto Band likitumbuiza katika zunduzi huo.
13
14Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika uzinduzi huo wakiwa katika viwanja vya Leaders Kinondoni.
15Kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh. Sophia Mjema, Askofu David Mwasota, Sheikh Mkuu wa Dar es salaam Alhadi Mussa Salum na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Hapi wakiwa katika uzinduzi huo.
16Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Paul Makonda akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika kwenye viwanja vya Leaders mara baada ya matembezi ya kuhamasisha wananchi kufanya usafi katika maeneo yao.
IMG_6078Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam wa pili kutoka kushoto na wenyeviti wa wenyeviti wa mitaa kutoka wilaya zote tatu wakifanya ishara ya kufangia ikiwa ni uzinduzi rasmi wa siku 90 za kufanya usafi katika jiji la Dar es salaam kutoka kulia ni Juma Ngemwa Kinondoni, Mbayo Chuma Ilala na Bakiri Makere Temeke.
IMG_6086Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Hapi akizungumza katika uzinduzi huo na kutoa maagizo kwa watendaji na watumishi wa Manispaa ya Kinondoni kuhakikisha wanazingatia na kutimiza malengo kuhakikisha Kinondoni inakuwa safi.

Breaking newz--Samahani kwa baadhi ya Picha- WATUHUMIWA WAWILI WA UJAMBAZI WALIOUA NJOMBE WAUWAWA IRINGA MUDA HUUWATU wawili wanaosadikika kuwa ni majambazi ambao wametokea Njombe wameuwawa katika majibizano ya risasi na polisi baada ya kuvamia Pub ya Mama Siyovelwa iliyopo eneo la mtaa wa Ikulu mjini.Majambazi hao wanasadikiwa kuwa walifanya tukio la ujambazi jana mjini Njombe na kfanikiwa kuua watu wawili na kuiba mali mbalimbali.Habari zaidi zitakujia.HABARI KWA MSAADA WA MZEE WA MATUKIO DAIMA BLOG

Friday, April 29, 2016

DAWA NA VIFAA TIBA KUWA NJIANI MIAKA MINNE BOHARI YA DAWA (MSD) YATOA UFAFANUZIUZI

 Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu akionesha moja ya nyaraka inayoonesha upelekaji wa dawa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam leo, wakati akitoa ufafanuzi kuhusu dawa za shilingi bilioni mbili kuwa njiani kutoka MSD Keko kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili tangu mwaka 2012.
 Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu (kulia), akizungumza katika mkutano huo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala, Victoria Elangwa na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Sako Mwakalobo. 
 Ofisa Uhusiano Mkuu wa MSD, Etty Kusiluka (kulia), akizungumza katika mkutano huo wakati akimkaribisha Mkurugenzi Mkuu wa MSD (kushoto), kuzungumza na wanahabari.Katikati ni Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja na Shughuli za Kanda, Terry Edward.
 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano na wanahabari ukiendelea

TIGO YATOA VISIMA 12 VYA MAJI KWA VIJIJI 12 SINGIDA

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge (katikati)akikata utepe katika makabidhiano ya visima 12 vyenye thamani ya millioni 174 kutoka Kampuni ya Tigo akiwa na Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kaskazini George Lugata(kulia),na kushoto ni mkuu wa mkoa wa Singida  Mhandisi Mathew Mtigumwe, katika kijiji cha Mtinko, mkoa wa Singida juzi. 
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge (katikati)akifungua moja ya bomba katika kisima   katika makabidhiano ya visima 12 vyenye thamani ya millioni 174 kutoka Kampuni ya Tigo akiwa na Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kaskazini George Lugata(kulia),na kushoto ni mkuu wa mkoa wa Singida  Mhandisi Mathew Mtigumwe, katika kijiji cha Mtinko, mkoa wa Singida juzi.
 Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kaskazini George Lugata(kulia) akifungua bomba katika moja ya kisima katika makabidhiano ya visima 12 vyenye thamani ya millioni 174 kutoka Kampuni ya Tigo pembeni yake ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge na kushoto ni mkuu wa mkoa wa Singida  Mhandisi Mathew Mtigumwe, katika kijiji cha Mtinko, mkoa wa Singida juzi.
 

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge (katikati)akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa wakazi wa kijiji cha Mtinko  katika makabidhiano ya visima 12 vyenye thamani ya millioni 174 kutoka Kampuni ya Tigo akiwa na Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kaskazini George Lugata(kulia),na kushoto ni mkuu wa mkoa wa Singida  Mhandisi Mathew Mtigumwe, katika kijiji cha Mtinko, mkoa wa Singida juzi. 
…………………………………………………………………………………………………………
 Kampuni ya simu ya Tigo leo imekabidhi visima 12 vya maji  vyenye thamani ya 174m/- kwa vijiji 12 mkoani  Singida  ikiwa ni kuchangia juhudi za serikali  za kupunguza  uhaba wa maji safi na salama uliopo nchini.Akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano  iliyofanyika kwenye kijiji cha Mtinko wilayani Singida  mkoani Singida, Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini George Lugata  alisema ufadhili huo  umo kwenye mikakati ya kampuni ya kusaidia  jamii katika kunyanyua hali zao za maisha.
Vijiji vitakavyonufaika kutokana na ufadhili huo pamoja na wilaya zake kwenye mabano ni Lulumba (Iramba), Kisana (Iramba), Kisonzo (Iramba), Songambele (Iramba), Kinyeto (Singida Vijijini) na  Damankia (Ikungi). Vingine ni  Muungano (Ikungi), Ighuka (Ikungi), Kamenyanga (Manyoni), Sasajila (Manyoni), Mtinko (Singida Vijijini) and Kinampanda (Kinampanda).
 “Msaada huu ni sehemu ya uwekezaji wa Tigo kwenye miradi ya kijamii  ambayo inaleta tija kubwa kwa jamii. Tuna imani kwamba kupitia visima hivi, Tigo inasaidia  kutatua uhaba mkubwa wa maji  katika eneo hili la mkoa wa Singida  ambalo kwa kiwango kikubwa  limekumbwa na uhaba mkubwa wa mvua katika kipindi cha miaka mine  iliyopita,” alisema Lugata.

 Aidha aliongeza kuwa uhaba wa maji  miongoni mwa  wilaya nyingi za Singida  umesababisha wakiazi wake  kupoteza muda mwinmgi kutafuta  bidhaa hiyo muhimu, jambo ambalo  Tigo inaamini  kuwa hivi sasa litafikia ukomo kutokana na upatikanaji wa visima hivyo.

 Makabidhiano ya visima hivyo yalihudhuriwa na kushuhudiwa na Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge  ambaye aliishukuru Tigo kwa ufadhili huo uliopatikana kwa wakati mwafaka akisema kwamba visima hivyo vitapunguza kwa kiwango kikubwa  uhaba sugu wa maji  uliolikumba eneo hilo  na kuchangia kukua ustawi wa jamii  kijamii na kiuchumi.

 Hata hivyo, alitoa wito kwa wadau wengine wa maendeleo  kuchangia kwenye juhudi kama hizo. Waziri Lwenge alisema, “Tunatoa shukrani za dhati kwa Tigo kwa kutuunga mkono kwenye juhudi zetu za kutatua  uhaba wa maji uliopo Singida na hata kwenye mikoa mingine nchini. Tuna imani visima hivi 12  vitasaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza tatizo hili linaloikabili jamii kwa sasa”.

TAFRIJA YA MCHAPALO BAADA YA TIGO NA SAMAKI SAMAKI KUINGIA UBIA YAFANAWadau wakifurahi usiku wa jana wakati wa hafla ya mchapalo baada ya Tigo na mgahawa wa samaki samaki kuingia Ubia ambapo pande hizo mbili zimekubaliana kufanya kazi pamoja  kwa kuleta  bidhaa/huduma zao kwa wateja wa kila mmoja.
Vinywaji murua kabisa 
Warembo wa Tigo wakiwa tayari kuhudumia wateja na wageni waalikwa wote 
Ulinzi ukiimarihwa kwa  wageni waalikwa na  wateja wote

Dkt. John Pombe Magufuli alitaka Jeshi la Polisi nchini na Ofisi ya Mwendesha Mashitaka kujirekebisha kwa kutekeleza wajibu wao kwa uzalendo

JA3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Makamanda wa Polisi, Wanasheria wa Serikali,  Wafawidhi wa Mikoa na Wakuu wa upelelezi wa Mikoa na Vikosi kabla ya kufungua rasmi Kikao kazi cha Makamanda hao wa Polisi katika Ukumbi wa Dodoma Convention Center
…………………………………………………………………………………………
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amelitaka Jeshi la Polisi nchini na Ofisi ya Mwendesha Mashitaka kujirekebisha kwa kutekeleza wajibu wao huku wakitanguliza maslahi ya taifa.

Rais Magufuli ametoa maagizo hayo leo tarehe 29 Aprili, 2016 wakati akifungua kikao cha kazi cha Makamanda wa polisi wa mikoa, Mawakili wafawidhi wa serikali  wa Mikoa na Wakuu wa upelelezi wa Mikoa na Vikosi, kinachofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa Mikutano wa Dodoma uliopo katika eneo la Tambukareli Mjini Dodoma.

Awali kabla ya kutoa hotuba yake Rais Magufuli aliwapa nafasi Makamanda na Mawakili Wafawidhi hao kutoa maoni yao juu ya changamoto zinazowakabili katika kutekeleza wajibu wa kufanya upepelezi na kuendesha mashitaka, hususani kujua sababu za kuchelewesha kesi za makosa ya jinai, ambapo wamedai ufinyu wa bajeti ndio sababu kubwa ya kucheleweshwa kwa kesi za hizo.

Kufuatia kutajwa kwa changamoto hiyo Rais Magufuli ameahidi kuhakikisha anawatafutia fedha kwa ajili ya kukabiliana nazo, lakini ametaka fedha zitakazotafutwa zitumike vizuri kwa kuwa taarifa zinaonesha Jeshi la Polisi limekuwa likihusishwa na matumizi mabaya ya fedha hali inayoongeza ukubwa wa matatizo yanayokwamisha utendaji wake wa kazi.
Ametolea mfano wa taarifa za matumizi mabaya ya fedha zinazotolewa kwa ajili ya kununulia vifaa na sare za askari, ama mikataba yenye mashaka inayotiwa saini kati ya Polisi na wawekezaji kuwa ni baadhi ya mambo yanayoongeza hali ngumu ya utendaji kazi kwa jeshi hilo.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AFUNGUA MKUTANO WA KUWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI KATIKA NCHI ZA UKANDA WA MASHARIKI NA KUSUNI MWA AFRIKA

M1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifungua mkutano kuhusu kuwezesha wanawake kiuchumi katika nchi za Ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika. Mkutano huo umeandaliwa na Jopo la Ngazi ya Juu la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon alilolituewa Mwanzoni mwa huu, kusaidia kufanya uchambuzi na kutoa mapendekezo ya namna ya kuchagiza kasi ya kuwezesha wanawake kiuchumi ifikapo 2030. Umefanyika Leo April 29,2016 Hyatt Hotel Dar es salaam.
M2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Jopo la ngazi ya Juu la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa la kuwezesha wanawake kiuchumi Baada ya kufungua mkutano kuhusu kuwezesha wanawake kiuchumi katika nchi za Ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika. Mkutano huo unazungumzia kuhusu kusaidia kufanya uchambuzi na kutoa mapendekezo ya namna ya kuchagiza kasi ya kuwezesha wanawake kiuchumi ifikapo 2030. Umefanyika Leo April 29,2016.
(Picha na OMR)

Thursday, April 28, 2016

Chadema yajitoa kura za maoni Katiba mpya
Dk. Vincent Mashinji, Katibu Mkuu wa Chadema (kulia) akiwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Centre Party cha Norway, Knut Olsen, wakitia saini makubaliano ya ushirikiano
Dk. Vincent Mashinji, Katibu Mkuu wa Chadema (kulia) akiwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Centre Party cha Norway, Knut Olsen, wakitia saini makubaliano ya ushirikiano
DK. Vincent Mashinji Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (chadema), amesema kuwa Katiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi ndiyo msingi imara pekee unaoweza kuweka mifumo na taasisi kwa ajili ya maendeleo ya kweli yatakayogusa maslahi ya Watanzania wote badala ya nchi kuongozwa na kauli za viongozi, anaandika Happiness Lidwino.

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO SAID MECKY SADICK AFANYA KIKAO NA WATUMISHI WILAYA YA HAI.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadicky akizungumza na watumishi,wakuu wa idara za Halmashauri na Wenyeviti wa vijiji na vitongoji katika wilaya ya Hai wakati wa kikao cha utamburisho kilichoafnyika katika ukumbi wa KKKT Bomang’ombe.
Baadhi ya viongozi wa Taasisi mbalimbali katika wilaya ya Hai wakiwa katika kikao hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Hai ,Gelasius Byakanwa akizungumza katika kikao hicho.
Baadhi ya watumishi na viongozi mbalimbali wa Dini wakiwa katika kikao hicho.
Mkurugenzi wa Halmshauri ya wilaya ya Hai,Said Mderu akijibu hoja mbalimbali zilizoibuliwa katika kikao hicho.

MKUU WA WILAYA YA MOSHI ,NOVATUS MAKUNGA AAJIONEA ATHARI YA MAFURIKO


Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akizungumza jambo na wataalamu alioongozana nao katika uwanja mdogo wa ndege wa Moshi kwa ajili ya kuruka na ndege ndo ya Shirika la Hifadhi za taifa (TANAPA) kwa ajili ya kujionea hali ya mafuriko.
Mkuu wa wilaya akiwa katika uwanja wa ndege wa Moshi kwa ajili ya maandalizi ya kwenda kujionea hali ya mafuriko katika maeneo mbalimbali.
Mtaalamau anayeshughulikia Majanga kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Canon Masanja (wa tatu toka kulia) akimuelekeza jambo rubani muda mfupi kabla ya ndege kuruka.
Mkuu wa wilaya ya Moshi akiteta jambo na Kaimu meneja wa uwanja mdogo wa ndege wa Moshi ,Fredrick Kimaro muda mfupi kabla ya kwenda kutizama eneo lililo athirika kwa mafuriko.