Thursday, June 30, 2016

SABASABA SPECIAL---TEMBELEA KOKOLIKO FASHION WAPO SABASABA KUKUPA BIDHAA BORA NA NZURI

 Aisha salim khoja ni miongoni mwawanawake wajasiriamali Tanzania ambae anatumia muda mwingi kujitangaza anawakaribisha watanzania wote kutembelea banda lake la KOKOLIKO  fashion linalipatikana ndani ya mabanda ya TWCC anabidhaa nyingi na nzuri anawakaribisha watanzania wote na wageni toka mataifa yote duniani kutembelea banda lake kuona bidhaa alizowaandalia.

Anamashati mazuri ya batiki vikapu vizuri alivyotengeneza kwa mikono yake.pia anapatikana Tanga unaweza kuwasiliana nae na popote africa anaweza kukuletea mzigo. 

Pia ukiacha shughuli hizi za kutengeneza mabatiki lakini pia anafanya kazi kama.kufundisha utengenezaji wa batiki na ujasilia mali kwa mabinti na wanawake wote, pia ni event organizer na anafanya fashion shows mbalimbali, pia yupo Tanga internatinal trade mark, na ni filamu producer.

Pia anasema kuwa changamoto anazokutana nazo ni upatikanaji wa masoko na anapenda kuwashauri tan trade wawe wanapanga mambo mapema na sio mpaka siku ya tukio ndo wanaanza kufuatilia vitu kama wafanya biashara wamechelewa kutoa vitambulisho imealazimu wao kulipa kama watu wengine wanao kuja kwenye maonyesho wakati wao ni wafanya biashara wa humo humo ndani.

KAULI ZA TCRA NA WAZIRI KIGWANGALA KUHUSU KIPINDI CHA USHOGA CHA CLOUDS TV HIZI HAPA

WhatsApp-Image-20160630 (14)

5
7

WABUNGE,JOSEPH MBILINYI,KUBENEA NA MILLYA NAO KULIONA BUNGE WATSAP WAFUNGIWA

Leo hii kamati ya haki,maadili na madaraka ya bunge leo inataraji kusoma taarifa ya shauri la Mbunge Joseph Mbilinyi baada ya kutoa ishara ya matusi bungeni na kunaswa na kamera za bunge!
Tunataraji Mbunge Mbilinyi kupewa adhabu kali ili iwe fundisho kwa vizazi na wabunge wa aina yake ndani na nje ya bunge!
Kwakuwa Joseph Mbilinyi alitoa ishara ya matusi kwa bunge na wabunge tulitegemea chama chake cha CHADEMA kingempa adhabu lakini wamenyamaza kimya!

Joseph Osmond Mbilinyi (Sugu) – Vikao 10
Joseph Mbilinyi (Mb) amekiri kunyoosha kidole cha kati juu wakati akitoka bungeni baada ya kusika mbunge amemtusi mama yake. Mh. Mbilinyi amejitetea kuwa ni kweli alinyoosha kidole cha kati juu baada ya kumsikia mbunge wa CCM akimtusi mama yake mzazi hivyo kupata short temper na kujikuta akitenda kosa hilo.

Pia Joseph Mbilinyi amesema kuwa alinyoosha kidole cha kati juu kama kupinga kile kilichokuwa kinafanyika na mbunge huyo wa CCM, alipoulizwa na Kamati ya Maadili inayoongozwa na Mh. Mkuchika, Mh. Mbilinyi alisema kuwa kunyoosha kidole cha kati juu hakina maana ya moja kwa moja hivyo kwa uelewa wake yeye alikuwa anapinga kitendo cha mbunge wa CCM.
Kamati ya maadili imeridhika kuwa kitendo cha Joseph Mbilinyi (Mb) kuonesha kidole cha kati juu ni kosa na kutoheshimu mamlaka ya Spika wa bunge baada ya kupitia matoleo ya maana mbalimbali ya (Kuonesha kidole cha kati juu) nchi tofauti tofauti.
Maazimio ya Kamati ya Maadili
Bunge limeazimia kuwa mbunge wa Mbeya Mh. Joseph Osmond Mbilinyi asimamishwe kuhudhuria vikao 10 vya bunge la 11 kuanzia kikao cha leo Juni 30 mpaka hapo adhabu itakapokuwa imekamilika. Bunge limepitisha kwa kauli moja adhabu hiyo.
Saed Kubenea – Vikao Vitano
Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea amepewa adhabu ya kutohudhuria bungeni vikao vitano mfululizo vya bunge la 11 kwa kosa la kutoa habari za uongo akiwa bungeni juu ya sakata la kiwanja cha Waziri wa Ulinzi Mheshimiwa Hussein Mwinyi kuwa ana mkataba wa kujenga nyumba za JWTZ

James ole Millya – Vikao vitano
Mbunge wa Simanjiro Mh. James Ole Millya amesimamishwa kutohudhuria vikao vitano vya Bunge kwa kosa la kusema uongo bungeni kuhusu Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu , sera ,bunge , kazi ,vijana , ajira na walemavu Jenista Mhagama kuwa na undugu na Yusuph Mhagama.

WAFANYAKAZI WA ABANA WAANDAMANA KUDAI MIL 400 WANAZODAI

ma1Wafanyakazi wa kiwanda cha kuchapisha vitabu cha ABANA Printers ltd,kilichopo kata ya Mapinga wilayani Bagamoyo mkoani Pwani,wakiandamana kudai mishahara na mafao yao wanayodai kwa kipindi cha miaka miwili na nusu ambayo yamefikia mil 400 .
(Picha na Mwamvua Mwinyi) 

SERENGETI BOYS YAPAA, MCHAWI MWEUSI ATAMBA


 


Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ imeondoka saa 9.45 alfajiri ya leo Juni 30, 2016 kwa ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia kwenda Visiwa va Hame-Shelisheli kwa ajili ya kuwavaa wenyeji katika mchezo wa marudiano kuwania nafasi ya kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana.

Serengeti Boys inaondoka na matumaini makubwa ya kuiondoa Shelisheli katika mbio hizo baada ya kuvuna ushindi mnono wa mabao 3-0 katika mchezo wa kwanza uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Jumapili ya Juni 26, 2016. Ili ifuzu, Serengeti Boys inahitaji kusimama imara katika matokeo hayo ama kwa kupata sare ya aina yoyote, kushinda au ikitokea kupoteza, basi isifungwe zaidi ya mabao 2-0.

Lakini Kocha Mkuu wa vijana hao, Bakari Shime maarufu kama Mchawi Mweusi kutoka Tanga, amesema, “Nawaheshimu Shelisheli, lakini vijana wangu hawawezi kuwapa nafasi hata kidogo wapinzani wetu. Hapa tulishinda, na kwako tunakokwenda tunakwenda kushinda. Vijana wangu wa Serengeti Boys wako vizuri. Nawapenda na wao wanatupenda makocha wao na viongozi wote wa TFF.”

THE MBONI SHOW YAWAFUTURISHA WATOTO YATIMA DAR, MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA SULUHU AWAPONGEZA

The mboni show yawafuturisha watoto Yatima Dar,Makamu wa Rais Mama Samia awapongeza
Kipindi cha The Mboni Show, chini ya Mtangazaji wake, Mboni Masimba ambacho kinachorushwa kupitia televisheni ya Taifa ya TBC, Jioni ya jana ya Juni 29.2016 wameweza kufuturisha wageni Watoto Yatima 268 kutoka katika baadhi ya vituo vya Mkoa wa Dar es Salaam kwa lengo la kuwafariji na kuwasaidia kama ilivyo kwa desturi ya waandaaji wa kipindi hicho huku Mama mgeni rasmi akiwa Makamu wa Rais Mama Samia Hassan Suluhu.

Akizungumza katika tukio hilo mara baada ya kufuturisha Watoto hao pamoja na wageni mbalimbali Mwanadada Mboni ameeleza kuwa, wamekuwa wakifanya hivyo mara kwa mara hii ni kutokana na kurudisha fadhila kwa jamii kwa kidogo kinachopatikana hivyo amewaomba wadau wengine kujitokeza kufanya jambo kama hilo kila inapohitajika kwa jamii.

Kwa upande wake, Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu amepongeza tukio hilo la Mwanadad Mboni Masimba kwani ni la kuigwa hivyo ni lazima jamii imuunge mkono kwa kujilea kwake.

"Nakupongeza Mboni na timu yako kwa kuwakumbuka watoto hawa. Tukio kama hili kuliandaa linahitaji gharama na kujitolea haswa. Tupo pamoja nawe na juhudi zako tunaziona nakupongeza sana." alibainisha Makamu wa Rais Mama Samia.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Paul Makonda, alimpongeza Mboni Masimba kwa shughuli hiyo kwani inasadia katika kukumbuka jamii hasa watoto hao ambao wengi wao wanalelewa katika vituo vya Yatima.

Katika tukio hilo lililofanyika katika ukumbi wa Karimjee uliopo Posta jijni Dar es Salaam mbali na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh. Paul Makonda, Pia viongozi wengine kadhaa walijumuika akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Kinondoni, Mh Ali Hapi na viongozi wa dini Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum pamoja na Kaimu Mufti wa Tanzania aliyemwakilisha Mufti Mkuu pamoja na Mabalozi akiwemo Balozi wa INDIA.

Pia wadau wa kipindi hicho cha The Mboni Show, watu maarufu, Wasanii, Wanahabari na wadau wengine wakiwemo wadhamini waliofanikisha shughuli hiyo.
DSC_8510Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu akiwasili kwenye tukio hilo la la kufuturisha watoto zaidi ya 268 lililoandaliwa na Mwanadada Mboni Masimba (kulia) anayeendesha kipindi cha The Mboni Show, kupitia televisheni ya TBC. Tukio hilo limefanyika jioni ya Juni 29.2016 katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam.
DSC_8508
Baadhi ya wadau wakiwasilia kwenye tukio hilo kumpa kampani Mwanadada Mboni Masimba
DSC_8539
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika tukio hilo
DSC_8532Meza kuu, Mama yake Mzazi, Mboni Masimba( kushoto), Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu na Mboni Masimba wakifuatilia tukio hilo

LIVE-- TANZANIA WOMEN CHAMBER OF COMMERCE (TWCC) KWENYE MAONYESHO YA SABASABA
NI kampuni inayojihusisha na kuendeleza biashara za wanawake wajasilia mali wa Tanzania. TWCC ni shirika lisilotengeneza faida na fedha inayopatikana uzungushwa na higaiwa kama gawio. Pia inajihusisha na vitu vingi kama kutoa mafunzo ya kibiashara kwa wanawake wote,pia wanatumia kuwajengea uwezo wa kutumia mikopo mbalimbali ili kuweza kuendesha biashara zao, kuwapeleka sehemu mbalimbali za maonyesho kama saba saba nane nane na matamasha ya kimataifa ili kuweza kujifunza ushindani wa kibiashara,pia wanasidia wanawake wote hata kama sio wanachama ila kwa upande wa fursa zinatolewa kwa wanachamma kwanza.

TWCC inashirikiana na mashirika mbalimbali ya kiserikali na yasiyo ya kiselikali ili kuweza kupata misaada mbalimbali baadhi ya mashirika hayo ni kama UN woman,CRDB, MNB pamoja na wizara mbalimbali kama vizara ya viwanda na biashara pamoja na wizara inayojihusisha na wanawake.

Ndani ya banda lao lililopo sabasaba kuna mkusanyiko wa wafanya biashara toka mikoa mbalimbali kama, Moshi Arusha Tanga Dar es salaam na mikoa mingine wanachama,na wote wamekuja na biashara tofauti tofauti ikiwa ni kazi za mikono yao wenyewe na baadhi ya bidhaa hizo ni sabuni, dawa za madoa,batiki, mikeka, na bidhaa nyingine nyingi ikiwemo nafaka.

Akizungumza na mwandishi wa Mtandao huu ambao umeweka kambi katika maonyesho ya saba saba Jijini Dar es salaam amesema kuwa Changamoto kubwa walio nayo ni fedha kampuni inakuwa na wakati mgumu kwa kuwa kwenye maonyesho kama hayo inabidi iwafadhili toka mikoa wanayotoka mpaka hapa walipo na pia kuwafundisha pamoja na kuendesha semina jinsi ya kuwasaidia wanawake wengi zaidi na kitu kingine ni kukosa masoko ya uhakika kwa ajili ya wajasilia mali hao.

TWCC inawashauri wanawake Tanzania kuweza  kujiunga ili kuweza kusaidiwa kujipeleka mbele Zaidi pia inawashauri mabinti wadogo kuja kwa wingi na kuachana na dhima ya kuajiriwa ni bora waweze kujiunga huku ili kutimiza ndoto zao. hao yote yamesemwa na MWAJUMA HAMZA Deputy executive director wa TWCC. na anawashuri watanzania wote kuweza kutembelea banda lao lililopo karibu na wizara ya mali asili na utalii kwa kuweza kuwaunga mkono wakina mama wa kitanzania ili kuweza kuwapa uwezo wa kutangaza soko la nyumbani

LIVE-- TANZANIA WOMEN CHAMBER OF COMMERCE (TWCC) KWENYE MAONYESHO YA SABASABA
NI kampuni inayojihusisha na kuendeleza biashara za wanawake wajasilia mali wa tanzania. TWCC ni shirika lisilotengeneza faida na fedha inayopatikana uzungushwa na higaiwa kama gawio. Pia inajihusisha na vitu vingi kama kutoa mafunzo ya kibiashara kwa wanawake wote,pia wanatumia kuwajengea uwezo wa kutumia mikopo mbalimbali ili kuweza kuendesha biashara zao, kuwapeleka sehemu mbalimbali za maonyesho kama saba saba nane nane na matamasha ya kimataifa ili kuweza kujifunza ushindani wa kibiashara,pia wanasidia wanawake wote hata kama sio wanachama ila kwa upande wa fursa zinatolewa kwa wanachamma kwanza.

TWCC inashirikiana na mashirika mbalimbali ya kiserikali na yasiyo ya kiselikali ili kuweza kupata misaada mbalimbali baadhi ya mashirika hayo ni kama UN woman,CRDB, MNB pamoja na wizara mbalimbali kama vizara ya viwanda na biashara pamoja na wizara inayojihusisha na wanawake.

Ndani ya banda lao lililopo sabasaba kuna mkusanyiko wa wafanya biashara toka mikoa mbalimbali kama, Moshi Arusha Tanga Dar es salaam na mikoa mingine wanachama,na wote wamekuja na biashara tofauti tofauti ikiwa ni kazi za mikono yao wenyewe na baadhi ya bidhaa hizo ni sabuni, dawa za madoa,batiki, mikeka, na bidhaa nyingine nyingi ikiwemo nafaka.

Akizungumza na mwandishi wa Mtandao huu ambao umeweka kambi katika maonyesho ya saba saba Jijini Dar es salaam amesema kuwa Changamoto kubwa walio nayo ni fedha kampuni inakuwa na wakati mgumu kwa kuwa kwenye maonyesho kama hayo inabidi iwafadhili toka mikoa wanayotoka mpaka hapa walipo na pia kuwafundisha pamoja na kuendesha semina jinsi ya kuwasaidia wanawake wengi zaidi na kitu kingine ni kukosa masoko ya uhakika kwa ajili ya wajasilia mali hao.

TWCC inawashauri wanawake Tanzania kuweza  kujiunga ili kuweza kusaidiwa kujipeleka mbele Zaidi pia inawashauri mabinti wadogo kuja kwa wingi na kuachana na dhima ya kuajiriwa ni bora waweze kujiunga huku ili kutimiza ndoto zao. hao yote yamesemwa na MWAJUMA HAMZA Deputy executive director wa TWCC. na anawashuri watanzania wote kuweza kutembelea banda lao lililopo karibu na wizara ya mali asili na utalii kwa kuweza kuwaunga mkono wakina mama wa kitanzania ili kuweza kuwapa uwezo wa kutangaza soko la nyumbani

Wednesday, June 29, 2016

KIKOSI CHA TWIGA STARS KIPYA CHATANGAZWA-MAJINA HAYA HAPA


Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Mpira wa Miguu ya Wanawake Tanzania, Nasra Juma ametangaza majina ya wachezaji 23 watakaounda kikosi cha Twiga Stars.

Kikosi hicho kinatarajiwa kwenda Kigali, Rwanda Julai 15, 2016 kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya timu ya taifa ya Rwanda ikiwa ni mwaliko maalumu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Rwanda (Ferwafa).

Wakati Ferwafa likiingiza mchezo huo wa Julai 17, 2016 kwenye orodha ya michezo inayotambuliwa na Shirikisho la Mpira na Miguu la Kimataifa (Fifa), lakini Mheshimiwa Rais wa Rwanda Paul Kagame kuwa sehemu ya burudani ya burudani mbele ya wageni wake ambao ni wakuu mbalimbali wanaounda Umoja wa Nchi za Afrika (AU) ambao watakuwa na mkutano wao nchini Rwanda.

Mbali ya soka kama burudani, pia Rais Kagame atatumia mchezo huo kama hamasa kwa wakuu wa nchi ili kutoa kipaumbele kwenye soka la wanawake ambako kwa sasa ni ajira ambayo inakwenda sambamba na kuitikia wito wa kupambana na changamoto za malengo ya millennia (MCC) ambayo pia yanataka wanawake wapate nafasi.

DUNIA TUUNGANE KUWATETEA WAPALESTINA WANATESEKA-SHEIKH JALALA

Kiongozi Mkuu wa kiroho wa Waislam Dhehebu la SHIA ITHNASHERIYA Tanzania Sheikh HEMED JALALA (Katikati) akifafanua jambo kuhusu maswala ya mateso na dhuluma yanayoendelea kurepotiwa kutoka nchi ya palestina ambapo amewataka watanzania na dunia kwa ujumla kuungana kwa pamoja kuhakikisha kuwa wanawatetea wananchi wa Palestina wanaonyanganywa haki yao ya kukaa kwa amani katika nchi yao

Na Exaud Mtei (Dar es salaam)
Wakati report za mateso na dhuluma zikiendelea kurepotiwa duniani zikiyahusisha mataifa ya pelestina na israel ambapo taarifa zimekuwa zikendelea kuonyesha jinsi Taifa la palestina wananchi wake wanavyopata mateso kutoka kwa taifa la israeli hatimaye  Kiongozi Mkuu wa kiroho wa Waislam Dhehebu la SHIA ITHNASHERIYA Tanzania Sheikh HEMED JALALA ameibuka na kuvitaka vyombo husika vikimeno umoja wa nchi za ulaya,umoja wa nchi za Africa,umoja wa nchi za kiarabu na dunia nzima kwa ujumla kuonyesha dhamira ya dhati ya kulisaidia Taifa la palestina na kuondokana na mateso wanayoyapata kutoka kwa taifa la Israeli mateso ambayo yamekuwa yakiendelea kwa  miaka mingi sasa.
Sheikh JALALA akizungumza na wanahabari mapema leo Jijini Dar es salaam ikiwa ni kuelekea uazimisha siku ya QUDS duniani ambayo ni siku maalum ya kukumbuka mateso wanayokumbana nayo wananchi wa palestina amesema kuwa imefikia wakati sasa dunia kwa pamoja kuungana bila kujali Dini na itikadi zake na kupigania haki ya wapalestina kwani wanaoteseka kule sio waislam pekee bali ni wananchi wote na hata wale wasio na dini.


Akieleza sakata linaloendelea katika nchi hiyo ya palestina amesema kuwa mateso yamekuwa yakiongezeka kadiri siku zinavyosogea ikiwa ni pamoja na nyumba za wananchi kuvunjwa,makanisa na misikiti kuharibiwa,mauaji ya kila kona,na kuharibiwa kwa mashamba yao ambayo wamekuwa wakulima wa mazao ya mizaituni jambo ambalo amesema kuwa linaonyesha wazi ni mipango ya wazi ya kuwamaliza wapalestina na kuwaondoa kabisa katika ardhi yao jambo ambalo amesema halifai kunyamaziwa na walimwengu wote.
Profesa ABDUL SHARIFU ni mstafu wa chuo kikuu cha Dar es salaam ambapo katika mkutano huo na wahabari naye alipata nafasi ya kueleza chanzo cha mgogoro kati ya mataifa hayo mawili na jinsi gani kwa sasa unaathiri maisha ya wana palestina kwa ujumla
Ameogeza kuwa mkakati uliopo hapo kwa sasa ni mkakati wa kufutwa kabisa kwa upalestina na kuwaondoa kabisa katika ardhi yao na katika nchi yao wakati ni wazi kwa nchi hiyo ni nchi yao halali na wanastahili kuishi kwa Amani kama mataifa mengine.
Akielezea jinsi dunia inavyotakiwa kuungana amesema kuwa katika kuwapigania wapelestina waweze kupata Amani yao sio maswala ya kidini wala kiitikadi bali ni jambo la kibinadamu ambalo halina dini wala kabila na ni jambo la utu la kutetea haki za wanadamu wenzetu ambao wanateseka mikononi mwa waisrael.
Pamoja na wito huo na kilio cha SHEIK JALALA pia ametoa wito kwa watanzania wote wakiwemo viongozi wan chi  kutokana na historia nzuri iliyopo tangu kipindi cha baba wa Taifa Mwalimu NYERERE la kuwa taifa lenye  mahusiano mazuri kwa wapalestina amelitaka taifa kufwata nyayo za Baba wa taifa na kuamua kuwasemea wapalestina na kuhakikisha kuwa wanapata haki yao wanayostahili.
NICE MUNISI ni mmoja kati ya watanzania wachache waliowahi kunafya ziara katikia nchi ya palestina na kujionea ukubwa wa mgogoro huo ambapo hapa akisimumua ushughuda wake kuhusu yale aliyojionea nchini palestina ambapo amesema kuwa alichokiona ni mateso makubwa sana wanayokumbana nayo wananchi wa palestina na dhuluma kubwa kutoka kwa Taifa la ISRAEL hivyo akaendelea kuunga mkono Juhudi za kuunganisha dunia ili kuwatetea wananchi hao amabo hawana hatia lakini wanakumbana na mateso makubwa
Katika kuonyesha kukerwa na maswala yanayoendelea nchini palestina Sheikh JALALA amewataka watanzania wote kwa ujumla kutoka kwa umoja wao siku ya ijumaa ya tarehe 1,mwezi wa Saba kufanya matembezi ya Amani ya kuonyesha dunia kuwa watanzania tunapinga kwa pamoja dhuluma wanayofanyiwa wapalestina katika ardhi yao matembezi ambayo yatafanyika katika Jiji la Dar es salaam.

Mgogoro wa Mataifa ya palestina na Irael ni mgogoro mkubwa ambao kwa sasa umechukua miaka mingi na umekuwa ukikuwa mwaka hadi mwaka huku taifa la palestina likionekana kuumizwa Zaidi na mgogoro huo kutokana na madhara makubwa yanayowakumba wananchi wake likiwemo wananchi kuuawa,wengine kukosa makazi pamoja na maelefu ya wananchi wa palestina kufungwa katika magereza ya Israeli kwa sababu ambazo sheikh JALALA amezitaja kuwa hazina mashiko.

SABABU KUU TANO ZA MBUNGE WA CHADEMA KUVULIWA UBUNGE LEO HUKO ARUSHA NA MAHAKAMA

Kesi iliyokuwa ikiunguruma kuanzia  Februari 29 ,2016 katika Mahakam Kuu jijini Arusha imetolewa hukumu leo hii
Katika shauri hilo aliyekuwa mgombea ubunge wa CCM jimbo la Longido Dkt Kiruswa  alifikisha mahakamni shauri hilo la kupinga matokeo ya ushindi dhidi ya mbunge wa Longido Mh.Onesmo Nangole.
Akisoma hukumu hiyo,Jaji Mwagesi  alisema kuwa mlalamikaji ndugu Kiruswa aliwakilishwa na Wakili msomi Dr.Masumbuko Lamwai na Wakili Haraka.Katika shauri hilo,dai la msingi la mlalamikaji bwana Kiruswa lilikua ni:
1.Kutumika kwa lugha ya matusi na kashfa wakati wa kampeni kutoka kwa mh Onesmo Nangole.
2.Kuwepo kwa wapiga kura kutoka nchi jirani ya Kenya walioletwa na Mh Nangole
3.kutumika kwa magari ya Chadema kwenye kusindikiza na kubebea masanduku ya kupigia kura
4.Mkurugenzi wa Uchaguzi kutangaza matokeo baada ya mgombea wa CCM kutolewa nje.
5.Kutokea kwa vurugu ndani ya chumba cha kuhesabu matokeo
Kutokana na madai hayo na kwa kuzingatia kanuni,sheria na ushahidi uliotolewa pamoja na vielelezo na mashahidi wa pande zote mbili,Jaji kutoka mahakama kuu Bukoba Mh.Jaji Mwagesi alisema;”Kutokana na kuzingatia viini vyote vya shauri hili kama vilivyosikilizwa na kwa mujibu wa sheria,Natamka kwamba;
Mahakama hii imetengua shauri hili na kwa kujiridhisha kwamba mchakato mzima haukuwa wa haki na huru hivyo mahakama inaamuru uchaguzi urudiwe upya.

MBUNGE WA UKONGA MWITA WAITARA-AFUTURISHA WAPIGA KURA KWAKE

lo1Waziri Mkuu wa zamani na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa,akizungumza katika Futari iliyoandaliwa na Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara(Chadema) kwa wananchi wa jimbo hilo nyumbani kwake Kivule Dar es Salaam juzi.
lo2Waziri Mkuu wa zamani na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa,akizungumza na waandishi wa habari baada aya kushiri Futari iliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara(Chadema),nyumbani kwake Kivule Dar es Salaam juzi.
lo3Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara(Chadema), akizungumza katika Futari aliyowaandalia wananchi wa jimbo hilo nyumbani kwake Kivule Dar es Salaam juzi.
lo4Wananchi wakifuturu Futari iliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara(Chadema),nyumbani kwake Kivule Dar es Salaam juzi.
lo5Wananchi wakifuturu Futari iliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara(Chadema),nyumbani kwake Kivule Dar es Salaam juzi.
lo6Wananchi wakifuturu Futari iliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara(Chadema),nyumbani kwake Kivule Dar es Salaam juzi.

PBZ Yaadhimisha Sherehe za Miaka 50 kwa Kusaidia Jamii na Kutembelea Hospitali ya Kidongochekundu.


Wafanyakazi wa PBZ wakijumuika na Mkurugenzi Mtenda wa PBZ Ndg Juma Ameir katika kutoa huduma kwa wateja ikiwa ni shamrashamra za kuadhimisha miaka 50 ya PBZ tangu kuazishwa kwa benki hiyo wakiwa katika Tawi la Malindi Zanzibar. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar Ndg Juma Ameir akitowa huduma kwa Wateja wa PBZ katika tawi la PBZ Malindi, Pbz imetimisha miaka 50 tangu kuazishwa kwa kwake Zanzibar. 
Wateja wa PBZ wakipita huduma za Kibenki katika Tawi la PBZ Malindi Zanzibar. 

Tuesday, June 28, 2016

TGNP WAENDESHA WARSHA KWA VIONGOZI WA NGAZI YA JAMII NA JAMII KWA UJUMLA KUPEANA UZOEFU WA CHANGAMOTO WAKATI WA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YAO

Meneja wa idara ya maarifa na utafiti na uchambuzi GLORIA SECHAMBO akimwakilisha mkurugenzi mtendaji wa Mtandao wa jinsia Tanzania TGNP wakati akifungua warsha ya siku moja ya viongozi mbalimbali wa ngazi za jamii ambao ni mjuuisho wa madiwani,na viongozi wa vituo mbalimbali vya maarifa Jijini Dar es salaam kujadili kwa pamoja utekelezaji wa majukumu yaliyotokana na michakato mbalimbaliiliyofanyika katika jamii.

Wakati akizungumza alipokuwa anafungua mkutano huo amesema kuwa Kwa kufikiri zaidi jinsi ya kuweza kuwabana na kuwafanya viongozi wa jamii na wanajamii kwa ujumla walikuja na Bunge la jamii ambalo ni sehemu ya kuwapa nafasi wanajamii kukutana kuibua hoja zao na kuwafikishia viongozi wao na kuyafanyia maamuzi kwa pamoja njia ambayo amesema kuwa inasaidia sana kwa wanajamii kuwawajibisha viongozi wao na kudai uwajibikaji nchini ambapo warsaha hiyo imewakutanisha viongozi hao na wanajamii hasa wa maeneo ya kipunguni,mwananyamala na mabibo kupeana uzoefu tangu mfumo huo uanze.


Viongozi mbalimbali na wanaharakati waliokutanishwa kwa pamoja na TGNP ili kujadili maswala mbalimbali yakiwemo Elimu,Afya,Mapambano Dhidi ya ukatili wa jinsia ngazi ya jamii,ikiwa ni pamoja na kubainisha maswala ya uchechemuzi kupanga mikakati ya kuimarisha mapambano katika maendeleo ya maji,elimu na ukatili wa kijinsia.
Afisa Programe kutoka TGNP ANNA SANGAI akizngumza na wanajamii hao wakiwemo viongozi mbalimbali wa ngazi za jamii wakati wa Warsha hiyo iliyofanyika makao makuu ya ,mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP Jijini Dar es salaam leo kwa lengo la kubadilishana uzoefu kuhusu kazi zao katika maeneo yao ya kila siku

WATEJA KUTOKA MITANDAO YOTE KUFURAHIA HUDUMA YA TIGO PESA NDANI YA TANZANIAMkuu wa Kitengo cha Huduma za Kifedha kutoka Tigo, Ruan Swanepoel akiongea kuhusu uzinduzi wa kampeni mpya iitwayo NITIGOPESA, ambayo 
watumiaji wa huduma za kifedha kutoka mitandao mingine wanaweza kutuma na kupokea pesa kutoka kwa watumiaji wa TigoPesa kwa bei ile ile na wafanyabiashara wanaopokea malipo kwa njia ya Tigopesa sasa wanaweza wakalipwa na wateja wa mitandao mingine bila gharama za ziada, Kushoto ni Meneja Chapa wa Tigo William Mpinga
.

MAJALIWA AMWAKILISHA MAGUFULI MKUTANO WA SADC

NAM1Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa akishiriki akatika Mkutano wa  Viongozi  Wakuu wa  Nchi  na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika ( SADC) uliofanyika kwenye hoteli ya Grand Palm  mjini Gaborone Botswana Juni 28. Waziri Mkuu alimwakilisha Rais John Pombe Magufuli kwenye mkutano huo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
NAM2Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Rais wa Afrika ya Kusini Jacob Zuma (wapili kulia)  kuingia kwenye ukumbi wa Mikutano wa hoteli ya Grand Palm mjini Gaborone kuhudhuria mkutano wa Wakuu wa Nchi  na serikali wa  Jumuiya yaMaendeleo kusini mwa Afrika ( SADC ) kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli Juni 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

MATUKIO YA PICHA BUNGENI DODOMA LEO

aks1Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Tulia Ackson akitoka nje ya ukumbi wa Bunge mara baada ya Kuahirisha shughuli za Bunge mapema leo.
( Pichazote na Frank Mvungi-Dodoma)
aks2Mwenyekiti wa Kamati maalum ya maandalizi ya mechi ya kati ya wabunge ambao ni wapenzi wa timu yaSimba na wapenzi wa timu ya Yanga Mhe. John Kadutu akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo mjini Dodoma uliolenga kuhamasisha wadau mbalimbali kujitokeza kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutatua tatizo la madawati ambapo kamati hiyo inaratibu maandalizi ya mechi kati ya timu wapenzi wa timu ya Simba na wapenzi wa timu ya Yanga itakayofanyika mwezi Agosti 2016 kwa lengo la kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutatua tatizo la madawati hapa nchini kwa kuhamasisha wadau kuchangia madawati yatakayo gawanywa katika Halmashauri zote nchini.
aks3Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwasilisha  Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Ununuzi wa Umma wa Mwaka 2016 (The Public Procurement Amendment Bill 2016) Leo Bungeni Mjini Dodoma.
aks4Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo (Kushoto) akiteta jambo na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Dkt.Medard Kalemani leo Bungeni Mjini Dodoma.
aks6Mwenyekiti waTimu ya Bunge (Bunge Sports Club) Mhe. William Ngeleja akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mechi kati ya wabunge ambao ni wapenzi wa timu ya Simba na wapenzi wa timu ya Yanga itakayofanyika mwezi Agosti 2016 kwa lengo la kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutatua tatizo la madawati hapa nchini kwa kuhamasisha wadau kuchangia madawati yatakayo gawanywa katika Halmashauri zote nchini.
aks5Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. George Simbachawene (Kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Dkt. Angella Kairuki Bungeni Mjini Dodoma leo wakati wa kipindi cha maswali na majibu.
aks8Makamu Mwenyekiti wa Kamati maalum ya maandalizi ya mechi kati ya wabunge ambao ni wapenzi wa timu ya Simba na wapenzi wa timu ya Yanga itakayofanyika mwezi Agosti 2016 Mhe. Mussa Azzan Zungu akitoa ufafanuzi juu ya umuhimu wa mechi hiyo yenye lengo la kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutatua tatizo la madawati nchini, kulia ni Mwenyekiti wa (Bunge Sports Club) Mhe. William Ngeleja.