Wednesday, November 30, 2016

WATUMISHI OFISI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA WAPIGWA MSASA

Mshauri Mwelekezi wa Masuala ya Jinsia kutoka “Women Fund” Profesa Ruth Meena akitoa mada.

 Mshauri Mwelekezi wa Masuala ya Jinsia kutoka “Women Fund” Profesa Ruth Meena (kulia), akiwasilisha mada juu ya jinsi ya kuingiza masuala ya jinsia katika mpango kazi wa taasisi wakati wa kikao kazi cha watumishi kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kilicho fanyika leo katika Ukumbi wa ofisi za Bunge jijini Dar es Salaam.
 Mafunzo yakitolewa.

Sheikh Hemed Jalala--Tumuenzi Mtume Muhammad s.a.w. kwa kuwa na huruma kwa watu wote

Kiongozi Mkuu wa kiroho wa waislam wa dhehebu la Shia
ITHNASHERIYA Tanzania Sheikh 
HEMED
JALALA wa pili kutoka kutoka kushoto akiongoza matembezi ya amani yaliyokuwa na lengo la kuadhimisha kifo cha Kiongozi wa waislam Mtume 
Mtume Muhammad s.a.w.
Picha na Exaud Mtei
Waislam wa Thehebu la Shia Ishnasheriya leo wamefanya maandamano ya Amani Jijini Dar e salaam maaandamano yaliyokuwa na lengo la kuadhimisha kifo cha kiongozi wao Mtume 
Mtume Muhammad s.a.w. ikiwa ni hatua ya kuadhimisha mambo mazuri aliyoacha duniani kiongozi huyo huku ikiwa ni Zaidi ya Miaka 1400 iliyopita tangu kifo chake.

Maandamano hayo yamefanyika Jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Kiongozi Mkuu wa kiroho wa waislam wa dhehebu la Shia ITHNASHERIYA Tanzania Sheikh HEMED JALALA na kuhudhuriwa na mamia ya waumini wa dhehebu hilo.


Akizungumza na wanahabari wakati wa maandano hayo ya Amani Jijini Dar es salaam Sheikh Jalala amesema kuwa Mtume Muhammad s.a.w. ambaye wanaadhimisha kifo chake ni kiongozi ambaye alitenda haki kwa watu wote na kuwa na huruma kwa watu wote bila ubaguzi wa aina yoyote hivyo ni jukumu la wanadamu hususani watanzania kujifunza kuishi kwa Amani na upendo Bila kubaguana .
Sheikh Jalala amesema kuwa lengo kuu la matembezi hayo ambayo yameanzia Boma Jijini Dar es salaam Hadi Kigogo ni kuwaonyesha watanzania kuwa kuna haja ya kuwa na huruma ambayo alikuwa nayo Mtume Huyo ambayo ilimfanya kuwapenda wanadamu wote wakiwemo waislam na wakristo na kukaa nao meza moja bila kujali Imani zao,ambapo amesema watanzania tunatakiwa kuwa na Roho hiyo ili kudumisha Amani iliyopo.

Aidha katika hatua nyingine Sheikh Hemed Jalala ametoa wito kwa viongozi wa dini ya kiislam wakiwemo Masheikh,Maimam kuiga huruma ya Mtume Muhammad s.a.w. kwa kukaa na wachungaji,maaskofu,mapadre,na viongozi wa dini mbalimbali Tofauti na zao kwa lengo la kujenga umoja na mshikamano kama wanadamu.


LHRC NAO WAMVAA MAKONDA WAKEMEA UDHALILISHAJI NA UKIUKWAJI WA MISINGI YA KISHERIA NA HAKI ZA BINADAMU


 Ndugu Wanahabari,

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu ni shirika lisilo la kiserikali ambalo si la kisiasa wala kibiashara lenye kujibidiisha katika kutetea, kulinda na kuendeleza haki za binadamu na utawala bora nchini. Kituo kimekuwa kikifuatilia mwenendo wa serikali na taasisi zake ili kuhakikisha utendaji wa serikali unafuata misingi ya sheria na haki za Binadamu kwa lengo la kuhakikisha kuwa utendaji wa serikali unakuwa na tija kwa wananchi wake.

Ndugu Wanahabari,
Tangu Serikali ya awamu ya tano iingie madarakani, takribani mwaka mmoja sasa, kumekuwa na jitihada za lazima za serikali yenyewe katika kupambana dhidi ya rushwa na ubadhirifu,nakuimarisha uwajibikaji  vitu ambavyo  ni vichocheo muhimu katika ustawina maendeleo ya  nchi.Kwa upande mwingine kumekuwa na ongezeko la uwazi katika utekelezaji wa baadhi ya shuguli za serikali jambo ambalo kwa mapana yake ni zuri pia.

Hata hivyo jitihada hizo zimekuwa na kasoro mbali mbali za kiutendaji , kiufundi na kisheria ambazo zimekuwa zikitajwa mara kadhaa na wadau mbalimbali ikiwemo Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu. Kikubwa zaidi katika haya yote ni ukiukwaji mkubwa wa Haki za Binadamu katika matamko na,hatua mbalimbali zinazochukuliwa na serikali kuanzia ngazi ya serikali za mitaa mpaka serikali kuu. Mambo haya ambayo kwa nadharia yanaonekana ni mepesi ni hatari zaidi katika ustawi wa nchi ya kidemokrasia na sisi kama watetezi wa haki za Binadamu hatutaacha kuyakemea vikali ili kujenga jamii yenye haki na usawa.

vitendo hivyo ambavyo serikali imeendelea kuvifumbia macho.
Ndugu Wanahabari,
Ninyi mmekuwa mashahidi kwani ni mara nyingi tumetoa matamko kukemea kauli zisizo afya kwa ustawi wa utawala wa sheria na Haki za Binadamu, lakini viongozi wa serikali wameendelea kuziba masikio na kuendelea kuvunja sheria na kukiuka haki za Binadamu, ili hali wakiongoza kama miungu watu.

Tuesday, November 29, 2016

Wakati Lema akirudi Rumande,Tizama kilichotokea Mahakamani leo

2Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema leo amefikishwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ambapo alirejeshwa rumande kufuatia pingamizi lililowekwa na upande wa Jamhuri kuhusu rufaa yake iliyokuwa imekatwa.
Mahakama iliwataka Mawakili wa Lema kuwasilisha notisi ya rufaa na si rufaa.
Kwa upande mwingine baada ya wafuasi wa mbunge huyo wamejitokeza mahakamani wakiwa wamevalia fulana zenye maandishi ‘Justice 4 Lema’ ikiwa ni njia ya kuishinikiza mahakama kumuachia mbunge huyo kwa wao wanaoa kuwa haki haitendeki.
Kesi la Mbunge Godbless Lema imehirishwa hadi Disemba 2 mwaka huu.

KAMPUNI YA ITEL YAWAKUMBUKA WATOTO WA KITENGO MAALUM SHULE YA MSINGI AIR WING DAR ES SALAAM

Wawakilishi kutoka katika kampuni ya simu ya ITEL Tanzania wakiongozwa na Afisa masoko wa kampuni hiyo Charles charle  wa katikati na Asha Mzambili ambaye ni afisa masoko msaidizi wa ITEL wakiwasili katika viwanja vya shule ya msingi ya Airwing iliyopo Jijini Dar es salaam wakati kampuni hiyo ilipotoa misaada ya vifaa mbalimbali kwa wanafunzi wa Kitengo maalum kilichopo.

 Katika shule hiyo vifaa mbalimbali vimetolewa na kampuni hiyo vikiwemo madaftari kwa ajili ya wanafunzi ,mabegi,na vifaa vingine ambavyo vitawasaidia wanafunzi wa shule hiyo ambao wana mahitaji maalum.
Vifaa mbalimbali vya shule Vilivyotolewa na Kampuni ya ITEL Tanzania leo kwa ajili ya wanafunzi wa Kitengo maalum ambao wana ulemavu wa akili wanaosoma katika shule ya msingi Airwing Jijini Dar es salaam 
Mwanafunzi Linus Alphonce wa shule ya Msingi Air wing Jijini Dar es salaam ambaye yupo kitengo maalum akipokea vifaa mbalimbaloi kutoka kwa mwakilishi wa Kampuni ya ITEL Sarphon Asajile wakati kampuni hiyo ilipokuwa ikitoa msaada mbalimbali katika shule hiyo 

Mwanafunzi Yasin Membe ambaye anasoma katika shule ya msingi Airwing kitengo maalum akipokea msaada wa vifaa mbalimbali kutoka kamouni ya ITEL Tanzania leo Jijini Dar es salaam 
Afisa masoko wa kampuni ya Itel Tanzania Charles Charle akizungumza na wanahabari leo Jijini Dar es salaam wakati kampuni hiyo ilipofika katika shule ya msingi Airwing Primary kwa ajili ya kuta msaada wa vifaa mbalimbali vya kimasomo kwa wanafunzi wanaosoma katika kitengo maalum shuleni hapo ambapo afisa Huyo amesema kuwa kampuni ya ITEL imejipanga kuendelea kuwasaidia watoto hao wenye uhitaji maalum na wataendelea kuwasaidia kila wakati huku akiwataka watanzania wengine kuwa na moyo wa kutoa kidogo wanachopata kwa watanzania wanaohitaji msaada wao.

Aidha amesema kuwa Msaada walioleta leo una thamani ya shilingi laki Tano ambapo umenunua vifaa mbalimbali kama Mabegi kwa wanafunzi hao,madaftari,Mathematical set,na vifaa vingine vidogo vidogo kwa ajili ya kuwasaidia watoto hao katika masomo yao.
Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Air wing Mwalimu Fabiola Malisa akitoa shukrani zake kwa kampuni ya Itel kwa kuwakumbuka watoto hao wenye uhitaji katika shule yake,
Katika shukrani zake amesema kuwa Tangu  Sera mpya ya elimu ipitishwe na kuwataka watoto wote kupelekwa shule kumekuwa na ongezeko kubwa la watoto wa aina hiyo katika shule yake ambapo walitoka watoto hamsini na sasa sabini hiyo akawataka watanzania mbalimbali kuendelea kuwakumbuka watoto hao katika misaada ili kuwapa moyo na kuwafariji 

Mtanzania wa Kwanza Kupanda Mlima Evarest Katika Mwaka 2012. Na Muafrika wa Tatu Kupanda Mlima Huo Mkubwa Duniani

Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said (Mpaka Basi) akiwa na mgeni wake Ndg Wilfred Moshi wakiwasili katika viwanja vya Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar, kutembelea na kujionea shughuli za Mkutano wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Ndg Wilfred Moshi ni Mtanzania wa Kwanza kupanda Mlima Mkubwa Duniani wa Evarest ukiwa na Mita 8,848, Mtanzania huyo Ndg Wilfred Moshi amepanda mlima huo mwaka 2012. akiwa ni Mwaafrika wa Tatu kupanda mlima huo na mwafrika wa Pili mweusi kupanda mlima huo Duniani kwa ukubwa.

Ndg Wilfred Moshi akiwa Zanzibar kwa matembezi na kuangalia Utalii wa Zanzibar na kupata nafasi kutembelea Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar kwa mualiko wa Mhe Mwakilishi wa Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said.
Ndg Wilfred Moshi akitambulishwa kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar akiwa Mgeni wa Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said (Mpaka Basi) akisalimia Wajumbe wa Baraza wakati wa kutambulishwa kwake.

ACT WAZALENDO WAMSHTAKI RC MAKONDA TUME YA MAADILI


TUME YA MAADILI IMUWAJIBISHE RC MAKONDA KWA   UDHALILISHAJI    WA WATUMISHI    NA WANANCHI.                 

                                     
NGOME  ya Wanawake ya Chama cha ACT Wazalendo imeshtushwa na kuhuzunishwa na kauli zisizo za kiuongozi na zsizozingatia kanuni za Maadili ya Utumishi wa Umma zinazoendelea kutolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.

Jana, katika mkutano anaouita wa kutatua kero kwa wakazi wa Dar esSalaam , Bwana Makonda ameendelea kushindwa kutatua kero na badala yake kuongeza kero ya kudhihaki, kudhalilisha kukejeli na kutukana hadharani wananchi anaowaongoza na watumishi anaowasimamia kitendo ambacho ni kinyume na maadili ya Watanzania.

Kitendo cha Mkuu wa Mkoa Makonda  akiwa katika eneo la Mabwepande, Wilaya ya Kinondoni Mkoani Dar es Salaam kumtolea lugha ya udhalilishaji Afisa Ardhi wa Manispaa ya Kinondoni Bi Rehema Mwinuka kwa kumtamkia kuwa; *"Hawa ndio vichaa tunaohangaika nao, toka hapa".* hakikubaliki na kimetusikitisha Sana na tunakilaani kwa nguvu zetu zote.

MADAKTARI NCHINI WAMETAKIWA KUITISHA MIKUTANO YA KIJAMII ILI KUJADILI MAGONJWA


Katibu Mtendaji wa Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA), Fabian Magoma  (kulia), akizungumza katika Kongamano la 33 la siku tano la Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA) linaloendelea Hoteli ya Kebby Mwenge jijini Dar es Salaam leo asubuhi. Kushoto ni  Mwenyekiti wa TPHA anayemaliza muda wake, Daktari Bingwa  Elihuruma Nangawe.

Dk. Manase Frank akitoa mada kwenye kongamano hilo.

 Profesa Andrew Swai akitoa mada.
 Wadau wa sekta ya afya wakifuatilia kwa karibu mada zilizokuwa zikitolewa katika kongamano hilo.
 Kongamano likiendelea.
 Dk. Andronicus Aloyce Rwelamila kutoka Hospitali ya Tumbi Kibaha (kushoto) na Muuguzi wa Hospitali hiyo, Mary Gowele wakiwa kwenye kongamano hilo.
 Kongamano likiendelea

Usikivu katika kongamano hilo. Kushoto ni Mwenyekiti wa TPHA, Dk. Elihuruma Nangawe

 Profesa Japhet Kileo (kulia), akiuliza maswali kwenye 
kongamano hilo.
 Dk. Mwanahamisi Magwangwara (kushoto), akizungumza wakati akijibu maswali mbalimbali kutoka kwa wadau wa sekta ya afya katika kongamano la 33 la siku tano la Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA) linaloendelea Hoteli ya Kebby Mwenge jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni mtoa mada, Profesa Andrew Swai. 
Dk.Chilolo Edward (katikati), akijibu maswali kuhusu changamoto ya waendesha bodaboda. Kushoto ni Profesa Andrew Swai na Dk. Manase Frank. 
Mkurugenzi wa Shirika la Wanawake katika Jitihada za Maendeleo (WAJIKI), Janeth Mawinza akielezea changamoto ya matumizi ya pombe katika Manispaa ya Kinondoni.

Monday, November 28, 2016

UJUMBE KUTOKA CHAMA CHA CPC CHA CHINA WATUA NCHINI KUJIFUNZA KAZI ZA CCM

 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),  Mkoa wa Dar es Salaam Ramadhani Madabida (kushoto), akimkabidhi Ilani ya CCM kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015,  Mkurugenzi wa Idara ya Mahusiano ya Kimataifa, Maendeleo na Mafunzo wa Chuo cha Viongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China, Jia Bo,  Dar es Salaam leo asubuhi, ambaye yupo nchini na wajumbe wenzake sita kwa zaiara ya siku saba ya kichama kukitembelea Chama Cha Mapinduzi (CCM).
 Mkutano ukiendelea.
 Wajumbe hao wakisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida.
 Makada wa CCM wakijumuika na wajumbe wenzao kutoka china.
 Mratibu wa Masuala ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Pindi Chana (kushoto), akizungumza na wajumbe hao.
 Madabida akiwakaribisha wajumbe hao.
Karibuni wajumbe kutoka China.

Mtikisiko yaacha gumzo jijini Mbeya

Mr blue akiwapagawisha wakazi wa Mbeya waliohudhuria katika  tamasha la Mtikisiko lililoandaliwa Na kampuni ya simu za Mkononi Tigo Tanzania, wakishirikiana Na Ebony Fm lililofanyika katika uwanja wa CCM Ruanda Nzowe(Shule ya Msingi Mwenge) mwishoni wa wiki iliyopita.

Shangwe zikiendelea 

Roma Mkatoliki akiwapagawisha wakazi wa Mbeya waliohudhuria katika  tamasha la Mtikisiko lililoandaliwa Na kampuni ya simu za Mkononi Tigo Tanzania, wakishirikiana Na Ebony Fm lililofanyika katika uwanja wa CCM Ruanda Nzowe(Shule ya Msingi Mwenge) mwishoni wa wiki iliyopita.

Haya ndiyo yaliyojiri kwenye soko la hisa wiki hii kuisha Ijumaa tarehe 25 Novemba 2016.

Mauzo ya Soko
Idadi ya mauzo imepungua kwa asilimia 87% na kufikia TZS 0.5 Bilioni kutoka TZS 4 Bilioni wiki iliyopita.
Idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa pia imepungua kwa asilimia 85% hadi Laki Moja (101,809) kutoka Laki Sita (671,618) wiki iliyopita.

Hata hivyo kushuka kwa mauzo ya hisa kunaweza kuhusianishwa na ongezeko la mauzo ya hati fungani. 

Wiki hii hati fungani nne (4) zimeuzwa na kununuliwa kwenye soko kwa thamani ya TZS 22.1 Bilioni, ambalo ni ongezeko la asilimia 33% ya thamani ya mauzo katika soko la hati fungani kutoka mauzo ya wiki iliyopita ambapo hati fungani sita (6) ziliuzwa na kununuliwa kwa thamani ya TZS 16.6 Bilioni

Kampuni tatu zilizoongoza kwa idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa ni zifwatazo:
1.     DSE kwa asilimia 37.74%
2.     TBL kwa asilimia 21.39%
3.     CRDB kwa asilimia 13.33%

Ukubwa wa Mtaji wa Soko
Ukubwa wa mtaji wa soko umeshuka kwa wastani wa asilimia 2.5% hadi Trilioni 20.4 kutoka Trilioni 20.9 wiki iliyopita.
Ukubwa wa mtaji wa makampuni ya ndani umeendelea kubaki kwenye kiwango kile kile cha Trilioni 8.1 wiki hadi wiki.

Viashiria (Indexes)
Sekta ya viwanda imeendelea kubaki kwenye wastani ule ule wa TZS 5,031 wiki hadi wiki.

Sekta ya Huduma za Kibenki na Kifedha imeshuka pointi 0.52 kutokana na kupungua kwa bei za hisa za DSE kwa asilimia 1.59%.

Sekta ya Huduma za Kibiashara wiki hii imeendelea kubaki kwenye wastani ule ule wa TZS 3,157 sawa na wiki iliyopita.

Ingawa idadi ya mauzo ya hisa imeshuka kwa asilimia 87%, idadi ya mauzo ya hati fungani imeongezeka kwa asilimia 33%.

Sunday, November 27, 2016

“Wanaofanyiwa Ukatili wa Jinsia wafike Polisi kitengo cha Dawati la Jinsia na Watoto” ASP Matarimbo

Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Polisi wa Kinondoni ASP Fatuma Matarimbo akitfundisha somo la Jinsia katika Warsha ya Mafunzo katika kuadhimisha siku 16 za kupinga Ukatili wa Kijinsia-Mtaa/ wa Udoe/Masjid Udoe, Kariakoo-Bilal Muslim Mission of Tanzania, leo Dar es salaam.

Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Polisi Kinondoni ASP Fatuma Mitarimbo ameitaka jamii ya Kitanzania kwenda katika Dawati la Jinsia na Watoto ili kupunguza matatizo mbalimbali yanayosababishwa na Ukatili wa Kijinsia.
“Jeshi la Polisi nchini lina vituo 417 vya Dawati la jinsia na Watoto Tanzania nzima, na watu wote wanakaribishwa katika vituo hivyo kuja kutoa taarifa ya matatizo yao ya Ukatili wa Kijinsia ili matatizo hayo tuweze kuyapunguza katika jamii yetu” amesema Mitarimbo.

ASP Mitarimbo amesema hayo leo katika Warsha ya mafuzo kwa Wajane, katika kuadhimisha siku ya 16 za kupinga Ukatili wa Kijinsia, katika Mtaa wa Udoe (Masjid Udoe), Bilal Muslim Mission of Tanzania, Kariakoo Dar es salaam.

Warsha hiyo iliandaliwa na Chama cha Wajane Tanzania / Tanzania Widows Association (TAWIA), ikishirikiana na WilDAF pamoja na Bilal Muslim Mission of Tanzania. ikiwa na Kauli mbiu"Funguka, pinga Ukatili wa Kijinsia, Elimu salama kwa wote"
Kuna aina kuu nne ya Ukatili wa jinsia ambayo ni Ukatili wa Mwili, ukatili wa Kisaikolojia, ukatili wa Kingono na ukatili wa Kiuchumi. “katili wa Kijinsia ni Kitendo chochote kinachoweza kumsababishia mtu mwingine kuwa na madhara, madhara hayo yanaweza kuwa madhara ya kimwili, kingono, kisaikolojia na Kiuchumi” amesema Mitarimbo

Aidha ASP Mitarmbo ametoa wito kwa Jamii kutoa taarifa katika Jeshi  Polisi kitengo cha Dawati la jinsia na Watoto, Misikitini, Makanisani, kwa Viongozi wa Dini na taasisi zinazohusika na kuzuia na kupambana na Ukatili wa Kijinsia ili kupunguza ukatili nchini" amesema ASP Mitarimbo

Chimbuko la kuadhimisha siku 16 ya kupinga ukatili wa kijinsia ni kutokana na mauaji ya kinyama kwa akina dada watatu ambao ni wa Kilamabela ambao walikuwa wanaishi katika nchi ya Dominika, waliuuwa mwaka 1960, chanzo cha kuuwawa kilisababishwa na Wanaume zao ambao walikuwa wanapinga uongozi wa mbaya wa kiongozi wao Leonard Tujilo.

Kwa upande wa Jeshi la Polisi Tanzania tangu mwaka 2009, Jeshi la Polisi liliona kwamba ukatili wa Kijinsia umeshika usikani/ unakuwa, ukatili wa kijinsia ukawa ni chanzo cha makosa, ni chanzo cha watoto wetu kuzagaa mitaani, ni chanzo cha ndoa nyingi kutengana/kuvunjika na ni chanzo kikubwa sana cha kupoteza baadhi ya vioungo.
Hapo jeshi la polisi likasema hapana, likawa linatafuta namna ya kupunguza vitendo kama hivi, kwani mara nyingi vitendo kama hivyo vinafanyika kwa siri,hivyo jeshi la polisi likaona umuhimu wa kufungua Dawati la jinsia na watoto ili kuwapa nafasi akina mama, baba na watoto kuja kulalamika na kutoa dukuduku lao na kunapolisi ambao wamefundishwa vizuri na hawawezi kuja kutoa siri.Kulia ni Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Polisi wa Kinondoni ASP Fatuma Mitarimbo akimuelezea mambo ya Kijinsia Mkurugenzi wa Chama cha Wajane Tanzania / Tanzania Wisows Association (TAWIA) Madam Rose Sarwatt.