Wednesday, January 11, 2017

Benki ya KCB yatoa mafunzo kwa ajili ya wanawake wajasiriamali nchini inayoitwa “2jiajiri

Baadhi ya wanawake wajasiriamali waliohudhuria mafunzo ya ujasiriamali yalitolewa na Benki ya KCB mkoani Dar es salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya KCB Tanzania Godfrey Ndalahwa, akiongea na wanawake wajasiriamali waliohudhuria mafunzo ya ujasiriamali yaliyotolewa na benki hyo mkoani Dar es salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya KCB Tanzania Godfrey Ndalahwa akizungumza na baadhi ya wanawake waliohudhuria mafunzo ya ujasiriamali yaliyotolewa na benki hyo mkoani Dar es salaam.
Mkuu wa Masoko na Mawasiliano ya Umma wa benki ya KCB Bi. Christine Manyenye akiongea na wanawake wajasiriamali waliohudhuria mafunzo ya ujasiriamali yaliyotolewa na benki hyo mkoani Dar es Salaam.

Benki ya KCB Tanzania yatoa mafunzo kwa ajili ya wanawake wajasiriamali inayoitwa 2JIAJIRI. Programu hii inalenga kumkomboa mwanamke mjasiriamali kutoka katika matatizo yanayosababisha biashara yake ishindwe kuendelea. Programu hii itaongeza ajira nchini kwa wanawake na hivyo biashara zao zitapanuka na kuwa na uwezo wa kuajiri wengine. Mafunzo haya yataendeshwa na wataalamu kutoka Tanzania Entrepreneurship and Competitiveness Center -TECC waliobobea katika masuala ya kijasiriamali, kifedha na ushindani wa biashara
“Mpango huu ni endelevu na tumepanga kufundisha wajasiriamali 315 nchi nzima. Leo tunafundisha wajasiriamali 100 katika makundi mawili tofauti. Mafunzo haya ni bure kabisa, KCB Bank itagharimia gharama zote. Tunachokihitaji kutoka kwao ni mahudhurio ya siku zote tatu na usikivu wa hali ya juu.” Alisema Godfrey Ndalahwa, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB.


Bw. Ndalahwa aliendelea kwa kusema kuwa mafunzo hayo yatafanyika mikoa yote ambako benki ya KCB ina matawi, Dar Es salaam, Mwanza, Morogoro, Arusha, Moshi na pia Zanzibar. Na tunalenga wanawake wajasiriamali wadogo na wa kati ambao tayari wanaendesha biashara lakini wanataka kuziimarisha zaidi. Lengo ni kuwawezesha kudhibiti vipengele vya uzalishaji na mgawanyo wa mapato na faida {control over factors of production and distribution of income and benefits) lakini zaidi ni kuwawezesha kuyatawala maisha yao kiuchumi na kijamii.

“Matatizo tunayotarajia kutatua kutoka kwa wanawake wajasiriamali ni elimu ya kifedha, kufikia huduma za kifedha, Ukosefu wa dhamana, kutokujua vizuri masuala ya kisheria, uelewa finyu wa sera za serikali na kiuchumi, njia hafifu za kuendesha biashara endelevu, ukosefu wa mtaji na utaalamu wa kuanzisha biashara kubwa” alisema.

Mkurugenzi aliongeza kwamba baada ya mafunzo hayo benki itawapatia wanawake wajasiriamali hao maafisa watatu watakaotembelea bishara zao na hii ni kwa wale tu ambao watahudhuria mafunzo ya siku tatu yote na kuonyesha nia ya kubadilika/kuendelea kibiashara). Maafisa hao watakua ni afisa fedha, afisa sheria na afisa masoko.

Alimaliza kwa kuwaambia wanawake wajasiriamali “JIULIZE KWANINI uhangaike wakati benki ya KCB tupo!”

No comments: