BYEEEE---HII NDIYO WIZARA ILIYOAGA DAR ES SALAAM NA KUHAMIA DODOMA LEO

Safari ya Dodoma 
Gari la Jeshi likiwa limebeba vifaa vya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ikiwa ni safari ya kuhamia Dodoma

 SERIKALI KUHAMIA DODOMA

WAZIRI - OFISI YA RAIS,MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA, MHE. ANGELLAH KAIRUKI AFANYA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU OFISI YAKE KUHAMIA DODOMA*

#Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora leo imeanza safari ya kuhamisha kundi la kwanza la watumishi wake kuelekekea Makao Makuu ya Nchi Dodoma.
#Kundi la kwanza limehusisha Uongozi wa Juu wa Wizara,Maafisa Waandamizi na baadhi ya watumishi wengine - Mhe. Angellah Kairuki.
#Jumla ya watumishi 87 watahamia Dodoma katika awamu ya kwanza - Mhe. Angellah Kairuki.
#Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora itafungua rasmi ofisi yake mjini Dodoma tarehe 30 Januari 2017 - Mhe. Angellah Kairuki.
#Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora itakuwa katika jengo la College of Humanities and Social Sciences lililopo (UDOM) kama makao yake ya muda- Mhe. Angellah Kairuki.
#Anuani ya Posta itakuwa;Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,Sanduku la Barua 670, Dodoma- Mhe. Angellah Kairuki.
*IMEANDALIWA NA IDARA YA HABARI (MAELEZO)*


About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.