Monday, January 9, 2017

KAULI YA DAVID KAFULILA WA CHADEMA LEO KUHUSU UKATA WA FEDHA MTAANI


Leo kwenye kipindi cha Tuongee Asubuhi Startv nimejulisha watazamaji kwamba ukata wa pesa mtaani sio sababu wa kukatika kwa pesa za dili tu . 
Bali usimamizi duni wa uchumi. Kwa mujibu wa ripoti ya Bank Kuu ya robo mwaka , kuanzia Juni 2016 -Septemba 2016, Ujazo wa fedha kwenye uchumi uliongezeka kwa 913bn wakati kipindi kama hicho mwaka jana ujazo uliongezeka kwa zaidi ya 3000bn. yaani ujazo wa fedha mwaka jana ulikuwa zaidi ya mara3 ya mwaka huu.
 Na Ripoti hiyo ya BOT( quartely economic review), imesema sababu ni kukosekana mikopo kwa sekta binafsi nchini. sasa sekta binafsi duniani kote ndio injini ya uchumi, na inaendeshwa kwa kukopa bank, kama mikopo kwa biashara inaporoka kiasi hicho unajengaje uchumi? mikopo ya biashara sio pesa za dili. ni halali kwajili ya biashara. 
sasa uamuzi wa sasa kwamba serikali inataka kukopa bank za ndani kiasi cha 1200bn baada ya kukosa mikopo huko Ulaya , utazidisha ukata mifukoni kwasababu hatua hiyo itasababisha bank za ndani kuzidi kupunguza mikopo kwa biashara za ndani na kuzorotesha biashara na hivyo mzunguko wa fedha kuzidi kupungua. huo ndio ukweli kuhusu kwanini mtaani hakuna pesa.

No comments: