Monday, January 16, 2017

Msajili wa mahakama ya kimbari ya Rwanda amtembelea Waziri Mwakyembe

Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt Harrison  Mwakyembe akizungumza wakati alipokutana na ujumbe wa Msajili wa Mahakama ya Masalia ya Kesi za Mauaji ya Kimbari yaliyotokea nchini Rwanda Dkt. Olufemi Elias aliekaa kulia kwa Mhe. Waziri Mwakyembe

Msajili wa Mahakama ya Umoja wa Mataifa ya Masalia ya Kesi za Mauaji ya Kimbari yaliyotokea nchini Rwanda Dkt. Olufemi Elias akizungumza na Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe alipokutana nae ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt Harrison  Mwakyembe akizungumza wakati alipokutana na ujumbe wa Msajili wa Mahakama ya Masalia ya Kesi za Mauaji ya Kimbari yaliyotokea nchini Rwanda Dkt. Olufemi Elias aliekaa kulia kwa Mhe. Waziri Mwakyembe

Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe amekutana na kufanya mazungumzo na Msajili mpya wa iliyokuwa Mahakama ya Umoja wa Mataifa ya Masalia ya kesi za mauaji ya Kimbari  yaliyotokea nchini RWANDA (UNITED NATIONS RESIDUAL MECHANISM FOR INTERNATIONAL CRIMINAL TRIBUNAL- UNMICT)  Dkt. Olufemi Elias.

Ugeni huo wa Msajili Dkt. Olufemi Elias kumtembelea Mhe Waziri Mwakyembe ofisini kwake jijini Dar es salaam ulikuwa kwa ajili ya kumsalimia na kujitambulisha rasmi kwake kwamba yupo nchini na ameshaanza kazi yake kama msajili wa mahakama hiyo.

Ugeni huo wa msajili ulimtaarifu Mhe Waziri kuwa maktaba ya mahakama hiyo iliyoko mjini Arusha inaweza kutumiwa na wasomi wa sheria nchini hasa wale wanaotaka kufanya utafiti katika masuala ya mauaji ya kimbari ya Rwanda .
Akizungumza katika kikao hicho, Mhe Waziri amepongeza ujio wa msajili huyo na timu yake na kumuahidi ushirikiano zaidi katika kuhakikisha anatekeleza vizuri kazi zake akiwa hapa nchini.

Kuhusu uwezekano wa kutumia maktaba ya mahakama hiyo Mhe. Wazri alielezea kuvutiwa kwake na mpango huo na kuahidi kuwa atakuwa balozi mzuri ambaye atafikisha ujumbe huo kwa shule na vitivyo vya sheria nchini ili viweze kutumia rasilimali hiyo kwa ajili ya kuboresha sekta ya sheria nchini.  


No comments: