POLISI DAWATI LA JINSIA WAPOKEA MSAADA WA VIFAA KWA AJILI YA UHIFADHI WA TAKWIMU ZA UKATILI WA MTOTO

Mkuu wa kitengo cha Dawati la Jinsia nchini Tanzania Afande DCP Maria Nzuki akipokea Msaada wa Vifaa mbalimbali vya kuhifadhia Takwimu za ukatili wa watoto kutoka kwa Viongozi wa Jukwaa la Utu wa mtoto CDF pamoja na wanunuzi wa Vifaa hivyo ambao ni UNFPA
 Na Exaud Mtei
Wakati Report mbalimbali za mashirika ya kibinadamu zikionyesha ongezeko la ukatili wa watoto nchini Tanzania hatimaye Jeshi la polisi nchini kupitia dawati maalum la Jinsia wameanza rasmi matumizi ya mbinu za kidigitali kukabiliana na hali hiyo inayotajwa kuongezeka siku hadi siku.

Leo Jijini Dar es salaam Jeshi la polisi kupitia kitengo maalum cha Dawati la Jinisia wamepokea msaada wa vifaa mbalimbali vya kisayansi vya ukusanyaji wa Takwimu kuhusu ukatili wa Kijinsia vifaaa ambavyo vimetolewa na Jukwaa la utu wa Mtoto –Children’s Dignity Forum –CDF vifaa ambavyo vina thamani Zaidi ya million sabini za kitanzania.
Koshuma Mtengeti ambaye ni executive Director Kutoka CDF aizngumza na wanahabari na wadau wa maswala ya Jinsia wakati wa Makabidhiano hayo leo Jijini Dar es salaam
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo Jijini Dar es salaam Mkuu wa kitengo cha Dawati la Jinsia nchini Tanzania Afande DCP Maria Nzuki amesema kuwa Jeshi la polisi limekuwa kwa kipindi kirefu wakihifadhi takwimu za ukatili wa watoto nchini kwa njia ya makaratasi lakini sasa wameanza mpango maalum wa kutumia vifaa vya kisasa vya kuifadhi data hizo hivyo kukabidhiwa kwa vifaa hivyo leo ni ishara ya kufungua milango kwa wadau wengine wa maswala hayo kujitolea kukisaidia kitengo hicho ili kufanikisha lengo lake.
Mkuu wa kitengo cha Dawati la Jinsia nchini Tanzania Afande DCP Maria Nzuki  akitoa shukrani baada ya kupokea msaada huo
Aidha Afande Nzuki amelishukuru shirika la UNFPA ambao ndio wanunuzi wa vifaa hivyo lakini pia shirika la CDF ambao ndio waliofanikisha kupatikana kwa ufadhili huo huku akiwataka kuendeleza ushirikiano na Kitengo hicho ili kufanikisha ulinzi wa watoto nchini.
Aidha akizungumza na wadau hao wakati wa makabidhiano hayo Koshuma Mtengeti ambaye ni executive Director Kutoka CDF amesema kuwa vifaa hivyo vyenye thamani ya Zaidi ya million 70 vimenunuliwa kwa ufadhili wa shirika la UNFPA ambavyo baadhi yake ni Screen kubwa ya kisasa na kitaalam,Laptop za kitaalam kwa ajili ya kuhifadhi Data hizo,na vifaa vingine vingi.

Baadhi ya Vifaa Hivyo 
Aidha ameongeza kuwa kwa awamu hii vifaa hivyo vitaelekezwa maeneo ambayo yana ukatili wa watoto wa hali ya juu ambapo kwa sasa vifaa hivyo vitaanza kupelekwa maeneo ya Tarime ambapo pia ndipo shirika hilo linapojikita Zaidi kuwasaidia watoto kuepukana na ukatili wa namna yoyote.


Mwakilisho kutoka UNFPA ambao ndio wanunuzu wa Vifaa hivyo Bi Christine Kwayu akizngumza wakati wa hafla hiyo


Picha Ya Pamoja Baada ya makabidhiano hayo


About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.