Sunday, January 8, 2017

Sehemu ya hotuba ya ndg. Zitto Kabwe katika uchaguzi mdogo Kata ya Isagehe, Kahama Mjini


Serikali ihangaike na Mabadiliko Sekta ya Madini

".......Wananchi wa Isagehe nimekuja kwenu si kwa Bahati mbaya, nipo hapa kama nyumbani Kabisa.
Mnatambua wazi kukua kwangu kisiasa kulichangiwa kwa kiasi kikubwa na watu Wa kahama ambapo Isagehe ni sehemu yake. Leo ninataka kuwakumbusha jambo moja ambalo tulifanya pamoja na kuleta mabadiliko kwa watu wa Kahama na maeneo mengine yenye migodi ya dhahabu.

Kama mnakumbuka nilipoibua hoja ya Buzwagi mwaka 2007, tulipoibua hoja ya ufisadi Wa Mgodi wa Buzwagi, wakati huo ilikuwa kila mgodi kwenye mkataba unatoa dola 200,000 kwa mwaka kwenye Halmahauri yenye mgodi kama mapato ya ndani. Na ninyi wakati ule mlikuwa katika maeneo matatu ambayo ni Ushetu,Msalala na Kahama mjini majimbo yalikuwa mawili halmashauri Ilikuwa moja. 

Hivi sasa mna Halmashauri tatu; Halmashauri yenu ya Mji wa Kahama yenye mgodi mmoja wa Buzwagi, Halmashauri ya Msalala yenye mgodi wa Bulyanhulu na Ushetu ambayo haina mgodi ingawa napo kuna dhahabu nyingi tu.

Baada ya mapambano yale kuhusu Buzwagi iliundwa Kamati ya Bomani ambayo pia tulikuwa na mmoja wa wabunge wa Kahama ndg. Ezekiel Maige. Kamati ya Bomani iliyoundwa na Rais Kikwete ilizalisha Sera mpya ya Madini ya mwaka 2009 na Sheria mpya ya Madini ya mwaka 2010. Baada ya kufanya mabadiliko makubwa ya sheria ya Madini mwezi April 2010 ikaonekana sasa makampuni yote yatalipa ushuru Wa huduma asilimia 0.3, ya mapato ambayo kampuni inayapata badala ya kulipa dola laki 2 hii matokeo yake ni nini? 

Hivi sasa leo hii kahama mnapokea zaidi ya $1.5m kwa mwaka. Nzega, Geita na Tarime nao wanafaidika na matunda ya kazi iliyoibuliwa na mbunge, sio wa Chama tawala bali wa upinzani. Ndio faida ya mfumo wa vyama vingi hiyo na Ndio maana nawasihi mumchague diwani kutoka upinzani hapa Isagehe ili kwenda kuongeza usimamizi wa fedha zenu kule baraza la madiwani. Naowaomba mumchague diwani kutoka Chama Chetu cha ACT Wazalendo ambacho mbunge wake aliwaletea mabadiliko chanya.

Lakini Mimi bado nina masikitiko makubwa licha ya kazi kubwa tuliyoifanya wakati ule chini ya Rais Kikwete ya kuleta sera na sheria mpya ya madini lakini nchi bado hainufaiki na madini yetu.
Nimeambiwa Buzwagi wanafunga mgodi Mwaka huu ( ingawa habari nyengine zinasema mashapo yameongezeka na hivyo kuna miaka mingine 5 ya kuchimba). Wamechimba Dhahabu imeisha na sasa wanafunga, kule Tulawaka wameshafunga mgodi,itakayofuata ni North Mara baadae Geita na mwisho kabisa Bulyanhulu. Nimeambiwa Geita na North Mara zitamaliza dhahabu kipindi cha urais wa Rais Magufuli na Bulyanhulu Ndio Ina miaka Kama 20 Hivi mbele. 

Resolute Nzega na Tulawaka huko Biharamulo wameshafunga migodi.
Tokea tumeanza kuchimba dhahabu kwa makampuni makubwa ( uchimbaji mkubwa ) tumeshauza nje dhahabu yenye thamani ya $20.5bn ambazo ni sawa na zaidi ya shilingi trilioni 45. Bajeti ya Tanzania ya mwaka huu 2016/17 ni shilingi 29 trilioni. Hivyo utaona kiasi gani tangu mwaka 1997 uchimbaji mkubwa wa Madini ulipoanza nchi yetu imeuza nje. Lakini mauzo hayo nje yanafaidisha nchi?
Kwa Mauzo hayo na matrilioni hayo, Tanzania imepata $800 milioni tu Kama mapato ya kodi na ushuru mbali mbali. Sisi katika nchi licha ya kuuzwa kwa  dhahabu zote  tumepata trilioni moja na nusu tu kwa miaka yote, chini ya asilimia 4 ya mapato yote ambayo makampuni ya dhahabu yameuza katika migodi yote.

Katika hali hii ndiyo maana ninamshangaa Rais Magufuli toka ameingia madarakani amekuwa mkali, amekuwa akipambana na mafisadi, amekuwa akitumbua na kutumbua na kutumbua, lakini hatumsikii Rais Magufuli akitekeleza mabadiliko yaliyowekwa katika sekta ya madini ili nchi inufaike na Raisilimali zake mpaka Leo nchi inaendelea kunyonywa. Rais yeye tumemsikia kwenye matamko 2 kuhusu Madini; magwangala na mchanga.

Tulimwambia Rais Magufuli weka wazi mikataba hii ya madini wananchi waione lakini mpaka Leo Mwaka umekatika katika Uongozi wake Rais hajazungumza wala hajashughulika nae jambo ambalo linapoteza mabilioni ya shilingi za kitanzania. Rais analikalia kimya anawaogopa wazungu wanaonyonya nchi kazi yake Rais ni kutumbua watu wadogo wadogo. Rais sasa ajishughishe na mambo makubwa ya nchi.

Leo hii nimepita katika barabara ya Kakola kuja Kahama. Hii  ni barabara inayounganisha migodi mitatu mikubwa lakini haina hata Lami. Haikuwa na lami kabla ya Uhuru mpaka leo hii ni aibu na uonevu kwa wananchi na ACT tukiwa na madaraka katika nchi hii tutaiita barabara ile ' Barabara ya unyonyaji ' ( Exploitation Road ) kwa kuwa Mali zao zinapitishwa pale lakini wenyewe hawanufaiki. Barabara inayounganisha migodi mikubwa ya dhahabu nchini Geita, Bulyanhulu na Buzwagi haina lami ni aibu kubwa Sana.

Tumemwambia Rais na serikali yake ahangaike na mambo haya makubwa ili ninyi wanyonge mnufaike lakini hakuna muelekeo. Licha ya Mtangulizi wake kumuwekea njia ya mabadiliko hayo ya Sheria ya Madini  Rais Magufuli kazi yake ilikuwa ni kuisimamia tu na mambo yangenyooka.
Sasa kwa ajili ya kumkumbusha kuwa hamkubaliani nae watu Wa Isagehe mnapaswa kumuonyesha mfano kuwa hamkubaliani nae juu ya masuala haya na hii mtaidhihirishia dunia kwa kuichagua ACT Wazalendo tarehe 22 January mwaka 2017.

Nimalizie kwa jambo la mwisho  kubwa sana la kitafa lakini si kubwa sana
Leo hii sisi tupo hapa tunaongea na ninyi kwa sababu kuna uchaguzi mdogo Mwaka Jana mwezi Wa Sita Mkubwa mmoja alikuja na amri ya kuzuia mikutano ya hadhara mpaka 2020 hakuna mikutano ya hadharavyama vya siasa vimeundwa na katiba na sheria na inaturuhusu kufanya mikutano.
Tusipofanya mikutano ninyi mtajuaje kama chama tawala kinavurunda,? Ndiyo maana ya mfumo Wa vyama vingi lakini bwana Mkubwa yule akazuia mikutano na baadhi ya watu wakamuunga mkono.

Lakini mungu nae ana yake kuna kampeni je atazuia mikutano ya kampeni? Mungu amemuonyesha kuwa kuna Mkubwa zaidi yake licha ya yeye kuwa Mkubwa katika nchi yake
Lakini wananchi kwanini haki hii ya kiraia zikanyagwe,Rais  anapata wapi uwezo huu Wa kusema hakuna kufanya siasa wapi anapata halafu viongozi wengine wanamuangalia
Haki ya kufanya mikutano ni haki yetu ya kikatiba haipaswi tusubiri chaguzi ndogo ndiyo tuje kuzungumza na ninyi.
Lazima tuje kuwaambia mambo yanapokuwa hayapo sawa leo vyakula vimepanda bei ukame unakuja kuna baa la njaa tunasema kwa kuwa kuna uchaguzi Mdogo,kama hakuna mambo haya tusingeyasema eti kwa kuwa bwana Mkubwa mmoja kaamua.

Leo hii kuna wabunge wamewekwa ndani miezi na dhamana haitoki kila siku mbunge anapelekwa mahakamani na kurudishwa tu hakuna dhamana
Huyu mtu amechaguliwa na watu wake wananchi zaidi ya laki tatu lakini huyu mtu mmoja kwa kuwa ana jeshi,Magereza usalama Wa Taifa mizinga na risasi mahakama unamchukua kiongozi huyu kutoka Magereza unampeleka mahakamani na kumrudisha mahabusu kisa unamkomoa
Leo inawezekana tukaliona hili ni sawa kwa sababu kafanyiwa mtu Wa chama kingine kafanyiwa Lema ni Wa Chadema eti haituhusu!
Ninawaambia.wakifanikiwa kwa Lema watafika kwa kila mmoja wetu na wote tutawekwa ndani kama hatukemei mambo haya lakini haya yanafanyika hata viongozi wastaafu nao hawastuki wamekaa kimya
Ndugu zangu wana Isagehe juzi Rais alikuwa Bukoba ambapo watu wameharibikiwa Nyumba zao wamepoteza ndugu zao na mbaya zaidi wananchi mbali mbali wakawasidia lakini Rais  badala ya kuwafarriji anawaambia kila mmoja atabeba mzigo wake  haya si maneno ya kiongozi Wa serikali kuwaambia watu wake

  
Niwakumbushe tulikuwa na mtu anaitwa Cleopa Msuya katika bajeti ya kwanza ya Rais Mwinyi Msuya akiwa.Waziri Wa.fedha akazungumza bungeni kuwa halo ngumu kila mmoja aubebe mzigo wake huyu aliondolewa ofisini baada ya Siku tatu

Mnamkumbuka Mramba aliposema watanzania watakula majani ilimradi ndege inunuliwe leo yupo wapi?
Leo Rais anaenda Bukoba anawaambia kuwa ni watu Wa majanga tu kwamba tetemeko.lao ukimwi wao kunyauka migomba no wao na kisha anawaambia wataubeba mzigo wao hii si kauli ya kiongozi.
Sisi watanzania tumeumbwa na viongozi wetu wameumbwa kuwa wanyenyekevu,ndiyo maana ninashaangaa Mwinyi yupo wapi?,Mzee Mkapa yupo wapi Kikwete yuko wapi kwanini wako kimya
Viongozi wastaafu wako wapi kumuonya huyu Rais  Magufuli ambaye anashindwa kuwa mnyenyekevu mbele ya wananchi waliompa kura huyu anakula Bure,anavaa bure analala bure kwa kodi zetu sasa madaraka yamempanda kichwani anawadharau wananchi wake

No comments: