Tundu Lissu Kakutana na Media Muda Huu,Tizama alichozungumza

 Mwanasheria mkuu wa chama cha Democrasia na maendeleo chadema Mh Tundu Lissu amesema kuwa kesi iliyomfunga Mbunge wa Jimbo la Kilombero, Peter Lijualikali ni kesi ya chuki za kisiasa na hawataikubali huku akisema wameanza mchakato wa Haraka wa kuhakikisha wanakata Rufaa ya Hukumu hiyo ili Mbunge huyo akae nje ya Kifungo.

Kauli hiyo ameitoa leo Jijini Dar es salaam wakati akizungumza na wanahabari kuhusu Hukumu ya kifungo cha miezi sita aliyoadhibiwa Mbunge wa chama hicho Jimbo la Kilombero, Peter Lijualikali
Amesema kuwa Tuhuma dhidi ya mbunge huyu hazikuanza jana wala Juzi bali zimeanza tangu akiwa Diwani kwa kusingiziwa kesi mbalimbali zikiwemo za kupiga watu lengo likiwa ni kutaka kumngoa katika siasa lakini amekuwa akivuka vizuizi hivyo na sasa wameamua kutumia mamlaka ya mahakama na chama cha Mapinduzi kumfunga mbunge huyo.

Lissu amesema kuwa Chadema wameamua kukata Rufaa ya kesi hiyo kwa lengo la kumtetea kisheria kutoka katika kifungo hicho.

Taarifa Zaidi kuhusu mkutano wa Lissu na wanahabari  zitakujia Habari24 tv baadae--------

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.