Monday, January 23, 2017

Ujumbe maalum kutoka Ngome ya Vijana ACT WAZALENDO kuhusu Uchaguzi Mdogo wa Jana


Ngome Ya Vijana Taifa ACT Wazalendo inapenda kuwashukuru na kuwapongeza Viongozi wote wa Ngome Ya Vijana kwa ngazi zote toka Tawi hadi Taifa pamoja na vijana wote wa ACT Wazalendo kwa kazi kubwa mliyoifanya katika chaguzi hizi za marudio na kufanikisha kufika hapa tulipofikia kama chama mpaka sasa.

Tunapenda kuwashukuru kwa umoja wenu na ushirikiano mkubwa mliouonyesha kwa chama chetu cha ACT Wazalendo hasa katika kipindi hiki kwa jinsi mlivoweza kutumia nguvu,muda na mali zenu mkisukumwa na uzalendo halisi kwa ajili ya nchi yetu kupitia kwa chama chetu cha ACT Wazalendo.

Lakini pia kama Ngome Ya Vijana Taifa tunawapongeza na kuwashukuru viongozi wote na wanachama wote wa ACT Wazalendo kwa jinsi mlivojitoa kwa hali na mali katika ushiriki wa chama chetu cha ACT Wazalendo katika chaguzi hizi na hatimaye kufika hapa tulipofika.
Hata hivo kwa moyo wa shukrani kabisa tunawashukuru Watanzania wote mliotuelewa na kutuamini ACT Wazalendo na kufikia kutupa kura za ndio ambazo zimezidi kutupa moyo na hamasa kubwa kwamba mnatuelewa na kuonyesha kwamba mpo pamoja nasisi kuhakikisha tunairudisha nchi yetu ya Tanzania katika misingi yake.
Na ama kwa hakika ninyi Watanzania pamoja na ACT Wazalendo,kwa pamoja, tutairudisha nchi yetu katika misingi yake.
Mwisho tunampongeza kila anayeitwa kwa jina la ACT WAZALENDO kwani licha ya muda mfupi wa ACT Wazalendo kujikita katika siasa za Tanzania kama chama cha siasa,Na sasa kuwa chama chenye miaka miwili tu katika siasa za Tanzania tumeonekana kukubalika na kueleweka kwa Watanzania kwani muitikio wa Watanzania kuonyesha kutuelewa na kutukubali umeongezeka zaidi ambapo kura tulizopata katika chaguzi hizi zimeonekana kupanda zaidi kulinganisha na kura tulizowahi kupata hapo nyuma huku vyama vikongwe japo vimeshinda kura zao zimeonekana kuporomoka wakati za kwetu zikipanda.
Uzalendo na Umoja wetu ACT Wazalendo kama mojawapo ya misingi yetu itatufikisha na watatuelewa tu.
Edna Sunga
Katibu Vijana Taifa ACT Wazalendo
23 Januari,2017.

No comments: