Sunday, February 5, 2017

ACT WAZALENDO KUFANYA MJADALA MKUBWA KUHUSU AZIMIO LA ARUSHA

Ikiwa Tanzania inatimiza miaka 50 tangu kutolewa kwa azimio la arusha ambalo lilijadiliwa na kupitishwa na halmashauri kuu ya chama cha TANU iliyoketi Mkoani arusha hatimaye chama cha Uopiunzani nchini Tanzania ACT WAZALENDO kimetangaza kufanya mjadala mkubwa wa kitaifa ambao utafanyika Mkoani arusha tarehe 25 March 2017 ikiwa ni muendelezo  wa maadhimisho hayo ya azimio la arusha.


Akizungumza na wanahabari mapema leo Jijini Dar es salaam Katibu wa itikadi na uenezi na mawasiliano ya umma kutoka chama hicho Bwana Ado Shaibu amesema kuwa Mjadala huo utafanyika kupitia mkutano mkuu wa Kidemocrasia ambapo kwa mujibu wa Ibara ya 29 ya katiba ya chama hicho cha ACT WAZALENDO ya mwaka 2015 kila mwananchi anaruhusiwa Kuhudhuria.

Amesema kuwa Mjadala Huo utakuwa ni Jukwaa la kitaifa kutafakari Mafanikio na mapungufu ya azimio la arusha na nafasi yake katika Tanzania ya leo,huku akisisitiza kuwa mkutano huo wa kidemocrasia utajadili nafasi ya siasa za kijamaa na mlengo wa kushoto Barani Africa na duniani katika zama hizi za kukua kwa kasi kwa siasa za mlengo wa Kulia.

Pamoja na hayo mutano huo pia chama hicho kitautumia katika kutafakari dhana ya azimio la Tabora linalohuisha azimio la Arusha katika mazingira ya karne ya 21.
Mbali na viongozi wa chama cha ACT WAZALENDO chama hicho kimewaalika viongozi mbalimbali wa kisiasa duniani na vyama mbalimbali,wawakilishi wa asasi za kiraia,wanazuoni,na wanaharakati kutoka ndani nan je ya nchi,ambapo chama hicho kimeshatoa mwaliko na kufanya mazungumzo na vyama vya Labour (Uingereza),Economic Fredom Fighter-EFF(Africa ya kusini)Die Linke(Ujerumani),na Syriza(Ugiriki)ili viongozi wao washiriki na kutoa mada kwenye mkutano huo.

Shaibu amesema kuwa chama hicho pia kimewaalika waliokuwa wanachama wa wa Taasisi ya Ruvuma Development Asociation (RDA) na wanachi wengine wa kawaida walioishi wakati wa azimio la arusha ili watoe uzoefu wao.

No comments: