.

AJALI YAUA WATU ZAIDI YA WATATU MOSHI,YUMO MWANDISHI WA HABARI NA MWENYEKITI WA CCM

ajali ccm
Habari tulizozipata hivi punde kutoka mkoani Kilimanjaro zinasema kuwa watu zaidi ya watatu wamefariki dunia akiwemo mwandishi wa habari wa gazeti la Habarileo Anord Swai na mwenyekiti wa CCM wilaya ya Hai katika ajali ya gari dogo.

Ajali imetokea maeneo ya Mwika Mawanjeni mahali panafahamika sana kama Bar Mpya Moshi mkoani Kilimanjaro.

Inaelezwa kuwa ndani ya gari walikuwemo watu sita wakiwemo viongozi wa CCM wakitoka kushiriki sherehe za miaka 40 ya CCM kimkoa yaliyofanyika wilayani Rombo.

Chanzo cha ajali inaelezwa kuwa ni fuso kufeli break na kuligonga gari dogo

Anord SwaiAnord Swai enzi za uhai wake

ajali moshi kilimanjaro
Ajali Kilimanjaro

Picha za ajali ya mkoani Kilimanjaro

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.