Friday, February 3, 2017

Baada ya Rais Magufuli Kumsaidia Mjane Jana,leo yametokea haya Jijini Dar es salaam

Wanawake mbalimbali ambao ni wajane nchini Tanzania waliojitokeza Mbele ya wanahabari katika Ofisi za Cama cha wajane nchini tanzania TAWIA kumshukuru Rais Wa Tanzania Baada ya kuonyesha kuanza kuwasaidia Wajane nchini Baada ya Jana kumsaidia Mjane aliyemuomba msaada katika siku ya haki duniani
 Na Exaud Mtei Dar es salaam

Baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli jana kuagiza kusikilizwa na kusaidiwa kwa mwanamke mjane ambaye alileta malalamiko yake ya kudhulumiwa mali za Mumewe jana katika maadhimisho ya siku ya Haki Duniani,Hatimaye chama cha wanawake wajane nchini Tanzania TAWIA wameibuka na kutoa ya moyoni kuhusu swala hilo huku pia wakipongeza hatua za haraka zilizochukuliwa na Mh Rais.

Akizungumza na wanahabari Mapema leo Jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Chama hicho Rose Sarwatt amesema kuwa chama hicho kimefarijika sana na hatua za Rais kuanza kuwajali wajane wa nchi hii jambo ambalo walilipigia kelele kwa muda Mrefu katika serikali zilizopita ambapo kwa Serikali ya Awamu ya Tano imeonyesha njia na matumaini mapya kwa wajane.
Aidha pamoja na Pongezi hizo Mkurugenzi huyo ametuma ombi maalum kwa Rais ambapo amesema kuwa kushughulika na Tatizo la mtu mmoja ni sahihi lakini Mh Rais akumbuke kuwa mjane huyo ni mmoja kati ya wajane Zaidi ya laki saba nchi nzima kwa mujibu wa ofisi ya Takwimu ya mwaka 2012 hivyo kumtaka Rais kuanza kuwasikiliza wajane wote nchini ili kupunguza adha kubwa wanayoipata pindi tu ambapo wanaondokewa na wanaume zao ambapo hukumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo kuzulumiwa mali zao.


Mkurugenzi wa Chama hicho Rose Sarwatt akizngumza na wanahabari mapema leo
Aidha wanawake hao wameiomba serikali kuanzisha mahakama ya familia itakayosimamia kesi zote za masuala ya familia ikiwemo kesi za mirathi jambo ambali wamesema kuwa litaondoa msongamano wa kesi za wajane zilizojaa katika mahakama mbalimbali nchini Tanzania ambazo pia zimedumu kwa muda mrefu bila kupata ufumbuzi.

Hata hivyo wajane hao wameomba kufanyiwa kwa marekebisho sheria ya mirathi ya mwaka 1963 ambapo amesema kuwa kama ilivyo kwa sheria nyingine nchini zinazofanyiwa marekebisho kwa dharura na nyingine kutungwa kwa Dharura Kutokana na uhitaji uliopo basi wameomba Mh Rais ifanyike hivyo kwenye sheria hiyo ili kuwapatia haki wajane waliowengi ambao wanakosa haki zao nchini.

Jana katika siku ya maadhimisho ya Haki nchini Tanzania Mwanamke mmoja aliyejitambulisha kuwa ni Mjane Kutokea tanga alijitokeza mbele ya Rais Magufuli na kufikisha kilio chake cha kudhulumiwa haki zake kutokana na kufariki kwa mume wake ambapo baada ya maelezo hayo Mh Rais aliagiza swala hilo kushughulikiwa mara moja na mwanamke huyo kupewa haki yake kisheria

No comments: