Thursday, February 16, 2017

Jana Waziri Mwakyembe alitishia Kukifuta chama cha wanasheria Tanganyika TLS,Sasa Hii ni Kauli ya Julius Mtatiro Muda Huu


Hakuna sheria wala kanuni kwenye Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) ambayo inazuia wakili ambaye ni mwanachama au kiongozi wa chama cha siasa kuwa Rais wa TLS.


Ndiyo maana huko nyuma makada wengi wa CCM wameongoza TLS na tunawajua kwa majina. Leo wamesikia Tundulisu ni mgombea wanakuja na hoja ya kitoto, kuwa TLS inataka kugeuzwa kuwa chama cha siasa.
Upuuzi! Hebu angalia logic zifuatazo. 

1. Wakuu wa wilaya na mikoa wote ni makada wa CCM na wanatuongoza hata sisi tusio CCM?

2. Rais Magufuli ameteua makada wa CCM kuwa maDED na maDAS wa Halmashauri wakati hiyo ni kazi ya andamizi, ya kitaalamu na weledi kuliko ukada na bado hatukumsikia Mwakyembe akitishia kuzifuta Halmashauri hizo?
Kwa hiyo TLS ikiongozwa na kada wa CCM siyo chama cha siasa, ila ikiongozwa na kada wa chama cha upinzani ni dhambi kubwa na hairuhusiwi, huu ni upuuzi wa kiwango cha PhD.
3. Dk. Tulia Ackson amekuwa kada wa CCM na wakati huo huo akiwa Naibu mwanasheria Mkuu wa serikali, ndiye aliongoza mawakili wa serikali kutetea uamuzi wa kutokaa mita 100 kulinda kura huku akiwa na mgongano wa maslahi.
4. Jaji Mkuu mstaafu Ramadhani, kamaliza tu kipindi chake kakimbilia kugombea urais kupitia CCM, haikuwa shida.
5. Msemaji wa JWTZ akiwa bado jeshini ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Msemaji wa CCM
6. Kikatiba na kisheria; wanasheria wa serikali, majaji, wanajeshi n.k. hawapaswi kujihusisha na siasa lakini CCM imekuwa ikiwafanya kuwa makada wa chama hicho tangu wawapo kazini au mara wanapostaafu, hiyo siyo dhambi.
TLS ambayo sheria na kanuni zake hazikatazi makada wa vyama kuiongoza, eti ndiyo inapigwa mkwara.
Ujumbe wangu kwa mawakili wote wasomi, mwezi ujao nendeni Arusha mkamchague Tundulisu halafu tunamsubiri Mwakyembe aifute TLS kisha yeye na serikali waunde TLS mpya ya makada wa CCM.
A big shame to this crawling country. Futeni hadi Tanzania tuhamie Kenya!
Mtatiro J,

16 Feb 2017.
Bonyeza Link ya chini uone alichokisema Mwakyembe Jana

Mwakyembe atembelewa na Uongozi wa TLS

No comments: