Saturday, February 11, 2017

JUKATA WAIBUKA,WAPONDA HATUA ZA KUPAMBANA NA MADAWA YA KULEVYA,WASEMA KATIBA INAVUNJWA,SASA WAANZA RASMI KUDAI KATIBA MPYA

 Na Mwandishi wetu-Dar es salaam
Wakati sakata la Madawa ya kulevya nchini Tanzania likiendelea kushika vichwa vya habari katika magazeti na Vyombo mbalimbali nchini Huku vigogo kadhaa wakiendelea kufanyiwa uchunguzi juu ya Tuhuma hizo hatimaye Naye mwenyekiti wa Jukwaa la katiba nchini Tanzania JUKATA Bwana Deus Kibamba ameibuka na kukosoa Vikali hatua zinazochukuliwa na Viongozi wa serikali juu ya watuhumiwa wa madawa hayo.

Akizungumza na wanahabari Juu ya kukwama kwa mchakato wa katiba mpya nchini na Jinsi ya kuuanzisha Upya Deus amesema kuwa hatua ya kutaja majina ya viongozi na watu wenye heshima katika jamii bila kuwa na ushahidi wa moja kwa moja na kabla vyombo husika vya kitaalam havijadhibitisha kuhusika kwao ni mwendelezo wa kuwaficha wahusika halisi wa madawa ya kulevya nchini na pia hatua hiyo inaendelea kupoteza ushahidi halisi wa wahusika.


Amesema kuwa pamoja na kuwa maamuzi hayo yanachukuliwa na watu ambao katiba haiwapi mamlaka ya kufanya hivyo lakini pia maamuzi hayo yanavunja ibara Zaidi ya tano katika katiba ya Tanzania ikiwemo kukiuka Staha za wahusika kwani kuwataja pamoja na kuvuruga uchunguzi lakini pia ni unawavunjia heshima waliyojijengea katika jamii na ikiwa watakutwa hawana hatia  hakuna sabuni itakayofaa kuwasafisha .


Ameongeza kuwa kumwita mtu aje Kituo cha polisi kwa ajili ya kumfanyia mahojiano hawezi kuacha kusafisha nyumba yake hata kama anahusika atajiandaa kwa kuhakikisha kuwa nyumba inakuwa safi,huku akihoji mamlaka halali za kushughulika na madawa ya kulevya nchini ziko wapi kwa kuwa kazi hiyo sasa inafanywa na watu ambao hawakupewa mamlaka ya kufanya hivyo.

KUHUSU RAIS KUKUBALI KUKOSOLEWA

Katika hatua nyingine JUKATA pamoja na kulaani watu wanaotumia lugha za matusi kuwakosoa viongozi wakuu wa nchi lakini hatua ya kuwakamata na kuwaweka ndani watu kwa makosa ya kukosoa kwa lugha nzuri bila matusi ni kinyume cha katiba ya Tanzania huku wakisisitiza kuwa hakuna kiongozi bora duniani asiyekubali kusikia mawazo ya kukosolewa kutoka kwa  wananchi wake.

Kibamba amesema kuwa uvumilivu wa kisiasa unahitajika sana katika nchi kipindi hichi  ambacho nchi inaongozwa na serikali mpya kwa kuwa kumekuwa na matukio ambayo yanatisha ikiwemo watu kupotea bila kujulikana walipo,na wengine kukutwa wakiwa wamefariki katika viroba na serikali kushindwa kutoa maelezo yaliyokamilika kuhusu matukio hayo.
Aidha katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo wa JUKATA amesema kuwa kulingana na matukio mbalimbali yanayoendelea kutokea nchini sasa ni wazi kuwa nchi inahitaji katiba mpya sasa na sio siku nyingine hivyo wao kama JUKATA wameanza Rasmi mchakato wa kufufua harakati za kupata katiba mpya nchini.

Moja kati ya mambo ambayo ameyataja kuwa wameanza nayo katika kufufua mchakato huo ni pamoja na kufanya mkutano mkuu wa katiba ambao utafanyika kuanzia Tarehe 2 hadi 3 mwezi wa Tatu ambao utawashirikisha wadau mbalimbali wa katika nchini, pamoja na uzinduzi wa Filamu mpya ya Dakika 20 itakayokuwa inaonyesha mchakato mzima wa katiba mpya.
Katika hatua nyingine JUKATA wametuma wito wa kufanya mazungumzo na Rais Wa Jamhuri Ya muungano wa Tanzania Mh Dr John Pombe Magufuli kwa ajili ya kujadili naye maswala mbalimbali yanayohusu Katiba mpya nchini pamoja na kumshauri Mambo kadhaa ya kupata katiba Mpya.

No comments: