KUELEKEA MCHEZO WA KESHO KATI YA YOUNG AFRICANS, N'GAYA CLUB


 


Maandalizi ya mchezo wa kesho wa kimataifa kati ya Young Africans ya Tanzania na Ng’aya ya Comoro, yamekamilika kwa asilimia 100.

Timu zote zipo Dar es Salaam, ambako Young Africans wao wameweka kambi kwenye Hoteli ya Zimbo iliyoko Kariakoo kwenye makutano ya mitaa ya Ndovu na Nyamwezi, Dar es Salaam.

Kwa upande wa timu ya N’gaya, yenyewe imefikia Hoteli ya Kaluganje iliyoko Mtaa wa Gerezani, Kariakoo wakati waamuzi kutoka Uganda, pamoja na Kamishna wa mchezo wanatarajiwa kutua leo.


Mchezo wa marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Young Africans ya Tanzania na Ngaya ya Comoro hatua ya awali utachezeshwa na Waamuzi kutoka Uganda ambano ni Alex Muhabi Nsulumbi atayekapuliza filimbi uwanjani, akisaidiwa na Ronald Kakenya na Lee Okello wakati Mwamuzi wa Akiba atakuwa Brian Nsubuga Miro huku Kamishna akitokea Afrika Kusini ambaye ni Monnyenyone Lucas Nhlapo.

Mchezo huo utafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kama ambavyo Young Africans walithibitisha CAF majuma mawili yaliyopita kabla ya terehe ya mchezo huo ambayo ni Februari 18, mwaka huu.

Tumepata taarifa kuwa kuna baadhi ya watu wana mpango wa kuonyesha mabango yenye ujumbe wa kukashifu Serikali na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na wadau wengine.

Tunachukua fursa hii kuonya wanafamilia ya mpira wa miguu wanaotaka kujihusisha na mipango hiyo, kuacha mara moja kwani vyombo vya dola vitakuwa makini kuangalia aina yoyote ya utovu wa nidhamu uwanjani...…………………………………………………………………………........................

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)


About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.