.

Majibu ya Zitto Baada ya kuibuka mjadala alivyoungana na Mwenyekiti wake wa zamani Mh Mbowe

Na Zitto Kabwe
Leo asubuhi nimeungana na ndg Freeman Aikaeli Mbowe kwenye mkutano wake na waandishi wa habari kuhusiana na wito uliotolewa kwake na Mkuu wa Mkoa wa Dar Es salaam kwenda Polisi. Nimehudhuria mkutano wake kuonyesha solidarity kwa Kiongozi mwenzangu wa Chama cha Siasa cha Upinzani nchini kuhusiana na tuhuma dhidi yake na uvunjifu mkubwa wa Sheria za nchi katika masuala ya utoaji haki.

Chama chetu Act Wazalendo kinapoona kuwa chama kingine cha upinzani kipo kwenye tishio au Kama kuna dalili za uonevu dhidi ya wanachama wa Chama kingine siku zote tunachukua nafasi ya anayeonewa. Kila siku tunasema, tukikuta mwenye nguvu anapigana na mnyonge tunamsaidia kwanza mnyonge kisha Ndio tunauliza ugomvi unahusu nini. Hatimaye mfumo wa haki unachukua mkondo wake.
Chama chetu kinaamini kuwa ' an attack on one opposition party is an attack to all '.
Tunasisitiza kuwa ni lazima vita dhidi ya madawa ya kulevya ipiganwe kwa kuzingatia misingi ya haki. Sisi wengine ni waathirika wa kuzushiwa na kutuhumiwa mambo ya uongo kisiasa, lazima tukatae wengine kutuhumiwa kisiasa. It is a matter of Principles.
Mkuu wa Mkoa yeyote nchini hana mamlaka ya ku summon mtu kituo cha polisi. Sheria ya Makosa ya Jinai, Sheria ya Jeshi la Polisi na Sheria ya Tawala za mikoa hazimpi mamlaka Mkuu wa Mkoa kuagiza watu kwenda Polisi. Wanaokwenda wanajipeleka tu.
Mkuu wa Mkoa ana namna bora zaidi ya kupambana na wauza madawa ya kulevya bila kupiga mayowe kwani kwa mayowe hayo anaweza kuwa Ndio anawakimbiza wahusika kutoka mikono ya sheria na kukamata wasiohusika.
Manipulation is never sustainable and history has proven just that

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.