Friday, February 3, 2017

Wanataaluma ya ualimu watakiwa kujipanga zaidi


Taasisi ya inayoongeza thamani ya mwalimu Teacher Juction  Imewataka wanataaluma ya ualimu kujipanga katika yakati hizi ambazo ualimu ni soko huria kwa kujipambanua na kuachana na akili ya kuwa wataajiriwa sehemu fulani wakati ualimu unafursa kubwa sana. 


Akizungumza katika semina fupi iliyoandaliwa na TEACHER  katika chuo cha vikindu mkoani pwani ,Mwenzeshaji mtendaji  wa shule sekondari ya Mwandege Boys ENOCK MRISHA Amesema  endapo walimu watajidhatiti katika taaluma yao suala ajira haitokuwa tatizo kwakua wanafursa nyingi ,ni vyema wakajua sasa ualimu umeingia katika soko huria.

Mwezeshaji mtendaji wa shule ya Mwendege boys  bwana MRISHA ameongeza kuwa waajiri wa waalimu wa shule binafsi wanakuwa na wasiwasi  kwa kuporwa walimu wazuri na hiyo ameifananisha walimu wa shule za binafsi wanavyokuwa na wasiwasi kufukuzwa hivyo amewataka wanachuo kujianda kuuzika sio kuuzinika kusomea ualimu.

Kwa Upande mwalimu mkuu  wa shule  ya sekondari ya Centennial Christian Seminali bwana PIUS BALIHUTA ameeleza kuwa ni vyema wananchi pamoja na walimu kuondoa dhana ya kuwa baada kukosa kila kimbilio liwe ualimu ambapo dhana hiyo inapunguza ufanisi wa kuwa mwalimu bora.

Hata hivyo Taasisi ya inayoongeza thamani ya mwalimu TEACHER JUCTION  pamoja na wakuu washule wanaofanya kazi nao Wamewataka walimu watarajiwa walioko vyuoni  kujiandaa kuwa walimu watakaoshindana katika soko huria,hivyo waone umuhimu TEACHER JUCTION kujiunga ili iwasaidie kuwauza katika shule binafsi.

No comments: