Tuesday, April 18, 2017

BOHARI YA DAWA (MSD) YAKARABATI GHALA LA DAWA HOSPITALI YA MIREMBE MKOANI DODOMA

 Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD),  Bwana Laurean Bwanakunu (kushoto), akipeana mkono na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati wa hafla ya kukabidhi jengo la kuhifadhia dawa la Hospitali Maalumu ya Mirembe mjini, Dodoma leo lililokarabatiwa na MSD. 

  Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD),  Bwana Laurean Bwanakunu (kushoto), akimkabidhi funguo za jengo hilo Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati wa hafla hiyo.Kulia ni Ofisa Huduma kwa Wateja wa MSD Mkoa wa Dodoma, Innocent Mugisha.
  Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD),  Bwana Laurean Bwanakunu (kushoto), akimuelekeza jambo Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya (wa pili kulia), wakati wa hafla hiyo. Wengine kutoka kushoto ni Meneja wa MSD Kanda ya Dodoma, Helman Mng'ong'o na Mkurugenzi wa Hospitali ya Mirembe, Dkt, Erasmus Mndeme.
 Jengo la kuhifadhiwa dawa katika Hospitali ya Mirembe lililokarabatiwa na MSD.
Picha ya pamoja mbele ya jengo hilo lililokarabatiwa na MSD.


Na Mwandishi Wetu, Dodoma.

Bohari ya Dawa (MSD) imekabidhi Jengo la kuhifadhia dawa la Hospitali Maalumu ya Mirembe,Dodoma iliyoifanyia ukarabati wa paa,dari na mfumo wa umeme.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya jengo hilomjini Dodma leo asubuhi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya amesema inapendeza kwa taasisi za serikali kusaidiana kuboresha huduma na utendaji pale inapowezekana.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa MSD,  Bwana Laurean Bwanakunu amesema mbali na ukarabati huo,watoa ushirikiano kuandaa makabati ya kuhifadhia dawa yenye utaalamu unaohitajika.

Ameongeza kuwa,Hospitali hiyo itaendelea kuhudumiwa kwa upendeleo, ikiwa ni pamoja na kukopeshwa, kutokana na utofauti wa wagonjwa wanaowahudumia.

Mkurugenzi wa Hospitali ya Mirembe Erasmus Mndeme ameshukuru kwa msaada huo na kuomba ushirikiano zaidi na MSD, ikiwa ni pamoja na kupata dawa kwa maelewano na kumalizia maeneo ya ndani ya kuhifadhia dawa.

No comments: