Saturday, June 3, 2017

ZITTO KABWE AFUNGUKA KUHUSU MAKINIKIA YA DHAHABU


June 3, 2017 Chama cha ACT Wazalendo kimefanya Kongamano kuhusu Rasilimali Madini ambalo limefanyika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa DSM kujadili masuala ya Madini ikiwemo Mchanga wenye madini unaosafirishwa nje ya nchi.
katika Kongamano hilo ambalo mmoja ya walioongea ni Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe ambaye alikuwa na mambo mawili makubwa.
“Ukiwa na Kampuni yako umetoka kokote ulikotoka unaenda Wizara ya Nishati na Madini unapewa Leseni ya kutafuta unakwenda Kakola, Kahama unapewa eneo unatafuta. Unakuta mashapo ya Dhahabu. Ukishayapata unaiambia Serikali Wizara ya Nishati na Madini nimepata. Wanakupa Leseni inaitwa Mineral License, na kama mchimbaji mkubwa inaitwa Special Mining License. Ukishapewa ile leseni rasilimali ile ni mali yako siyo mali ya nchi tena.” – Zitto Kabwe.

No comments: