Monday, July 24, 2017

ACT YAWAKUMBUKA NGULI WA SOKA 1980-81

ACT Wazalendo yawakumbuka mashujaa Wa Soka Tanzania

Kata ya Kigoma imememaliza vikao vya kupanga majina ya Mitaa na imeamua kutoa mitaa 25 Kwa ajili ya kikosi cha #TaifaStars kilochoshiriki AFCON 1980. Wachezaji na makocha wote watapata mitaa kwenye eneo la Mji Mwema. Namshukuru Sana Diwani wa Kata ya Kigoma Ndugu Hussein Haidary Kalyango Kwa kufanikisha hili. Nitajithidi wachezaji wote waliohai na walimu wao wahudhurie shughuli maalumu ya kuzindua mitaa yenye majina yao. 

Kata Hii pia imetoa jina Kwa Prof. Abdulrahman Mohamed Babu kwa mchango wake kwenye umajumui wa Afrika na ukombozi wa Afrika. 

Kikosi cha Taifa Stars ya mwaka 1980 hiki hapa

Athumani Mambosasa 
Juma Pondamali 
Taso Mutebezi 
Jelah Mtagwa 
Leodgar Tenga 
Mohamed Kajole 
Husein Ngulungu 
Mtemi Ramadhan 
Juma Mkambi 
Omari Hussein 
Mohamed Masewa 
Thuweni Ally 
Peter Tino 
Ahmed Thabit 
Charles Boniface 
Salim Amiri 
Adolf Richard 
Zamoyoni Mogela 
Martin Kikwa 
George Kulagwa 

Uzinduzi wa Mitaa Hii ya Mashujaa wetu utafanyika Juumamosi ya Kwanza ya Mwezi wa Tisa ambapo kutachezwa Mechi kati ya Timu ya Manispaa ya Lake Tanganyika SC na Timu ya Bukavu Dawa ya DRC. 

Zitto Kabwe 
Kigoma Mjini

No comments: