Thursday, July 6, 2017

IGP SIRRO APOKEA MSAADA WA MAGARI MANNE LEO JIJINI DAR ES SALAAM

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro na Meneja Mkuu wa kampuni ya utengenezaji magari ya Haval, Jianguo Liu wakikata utepe kuashiria kukabidhiwa magari manne yaliyotolewa na kampuni hiyo ikiwa ni juhudi zake katika kulisaidia Jeshi la Polisi kupambana na uhalifu nchini. Hafla hiyo imefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Polisi,Oysterbay,jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro   akisikiliza maelekezo ya jinsi inavyotumika moja ya magari manne waliyokabidhiwa na Kampuni ya utengenezaji magari ya Haval. Anayemuelekeza ni Meneja wa Kampuni ya Kifaru, Mario Gaspari. Hafla hiyo imefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Polisi, Oysterbay, jijini Dar es Salaam .Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro   akikagua moja ya magari manne waliyokabidhiwa na Kampuni ya utengenezaji magari ya Haval. Ambapo aliishukuru kampuni hiyo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi katika vita ya kupambana na uhalifu. Hafla hiyo imefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Polisi,Oysterbay,jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

No comments: