BIASHARA

JINSI YA KUTUMIA UBER VIZURI - MAELEKEZO YA SAFARI YAKO NYINGINE YA UBERUber imejitolea kutoa huduma ambayo ni rahisi na nzuri kwa abiria na madereva. Sehemu ya kuunda uzoefu huu rahisi ni kutoa maelekezo kuhusu jinsi madereva na abiria wanapaswa kufanya na kutendeana safarini. Hiyo ndiyo maana Uber imetoa Maelekezo yao yaliyosasishwa ya Jamii, mwongozo huu sio tu wa 'jinsi ya' kwa madereva washiriki wa Uber, bali pia kwa abiria wa Uber.
Hii ndio mara ya kwanza Uber imechapisha sera inayoelezea ni kwa nini abiria wanaweza kupoteza uwezo wao wa kupata Uber. Hii ni muhimu kwa sababu wakati madereva wanatumia Uber wanafanya zaidi ya kuendesha gari tu: wanashiriki gari, nafasi na muda wao na abiria. Na ijapokuwa abiria wengi wanawaonyesha madereva heshima, kwa bahati mbaya sio kila wakati.
Maelekezo yaliyosasishwa ya Jamii ya Uber husaidia kuelezea ni nini Kisichokubalika kwenye safari ya Uber. Nyingi kati ya hizi ni mambo ya kawaida kwa wengi wetu lakini yanapaswa kuzingatiwa - iwe ni kutapika kwenye kiti cha nyuma au kuacha takataka ndani ya gari, orodha iliyo hapa chini ya maelekezo ni moja ambayo kila mtu anayetumia Uber anapaswa kuelewa - madereva na abiria na hata pia wale wanaosafiri pamoja na abiria / marafiki wengine.
Lazima watoto waangaliwe.
Wale walio chini ya umri wa miaka 18 wanaweza kutumia Uber wakisimamiwa na mtu mzima, lakini hawawezi kuwa wenyewe na akaunti ya Uber. Wazazi au walezi wanapaswa kuwa na watoto wao kila wakati.
Kwenda mbele, ikiwa Uber itagundua kwamba mtoto asiyekuwa na mzazi ni mmiliki wa akaunti, akaunti hiyo italemazwa mara moja. Kama Uber itagundua kwamba abiria ana umri wa chini ya miaka 18 lakini mmiliki wa akaunti ni mtu mwingine ambaye amezidisha umri wa miaka 18, Uber itamkumbusha mmiliki wa akaunti hiyo kuhusu sera ya Uber na kulemaza wasifu wake baada ya onyo la pili.

Usalama kwanza
Kufika mwisho wa safari yako ndio kipaumbele cha juu. Hii ndio maana madereva wanapaswa kutii sheria za barabarani kwa mfano, kufuata kasi inayoruhusiwa, kutoendesha kama wamelewa au kutumia dawa na kutotumia simu wanapokuwa wakiendesha gari. Madereva wanapaswa kupumzika kila wakati ikiwa wamechoka.
Abiria wanapaswa kutekeleza jukumu lao la kuvaa mikanda ya viti na kutojaribu kuwabeba watu zaidi wakati hakuna mikanda ya kutosha ya viti. Abiria wanapaswa pia kujiepusha kubeba vileo au mihadarati ndani ya gari na hawapaswi kumwomba dereva kwenda kwa kasi ya juu kuliko kasi inayoruhusiwa.

Wape abiria na madereva nafasi yao ya binafsi
Ijapokuwa mazungumzo ya kirafiki hayana madhara yoyote wakati wa safari, heshima inapaswa kudumishwa kila wakati. Abiria na madereva wanapaswa kupeana nafasi ya binafsi na hawapaswi kufanya yule mwingine ajihisi vibaya. Uber ina sheria ya 'hakuna vitendo vya kimapenzi', inayomaanisha hakupaswi kuwa na vitendo vya ngono kati ya madereva na abiria. Hiyo ni pamoja na kuchezeana na kugusana. Migusano yoyote ya kimwili kama vile kumgonga au kujaribu kumuumiza dereva yamepigwa marufuku.

Heshima
Heshima ni muhimu, hakuna wakati wowote abiria au madereva wanapaswa kutoheshimiana. Magari yanayotumika kwenye app ya Uber ni ya madereva washiriki na wanajivunia kuweka magari yao katika hali nzuri kwa ajili ya starehe ya abiria. Abiria wanapaswa kuheshimu magari wanayoyatumia na wanapaswa kuacha magari hayo katika hali ambayo waliyapata.
Tabia ya ukaidi kama vile kuharibu gari haitakubaliwa. Kutumia lugha mbaya imepigwa marufuku pia. Kuwa na fujo au ubaguzi kunaweza kusababisha abiria kupigwa marufuku kutumia app hii. Uber haibagui kwa misingi ya jinsia au umbari na abiria yeyote ambaye hashiriki mtazamo huu hakaribishwi kutumia app hii.

Maoni yanatusaidia sisi wote kuimarika.
Kutoa maoni huwezesha Uber kujua abiria ameridhishwa au kutoridhishwa na nini, hiyo ndio maana madereva na abiria wanapaswa kutoa maoni ya safari yao kila wakati. Wakati watu wanajua kuwa wanatathminiwa wanakuwa makini zaidi kuhusu tabia zao na wanawajibika kwa hatua zao. Ajali, ada isio sahihi ya nauli au mabishano yanapaswa kuripotiwa kwa kubofya kitufe cha msaada kwenye app. Kuna timu ya usaidizi kwa wateja ambayo iko tayari kusaidia kila wakati.
Baada ya kujua kuhusu ukiukaji Uber itawasiliana na dereva ili kuchunguza. Kulingana na hali ya tatizo, akaunti ya abiria inaweza kusitishwa kwa muda wakati wa uchunguzi. Iwapo hoja hiyo itahusisha makosa makubwa yanayohusisha ukatili, makosa kadhaa ya ngono, unyanyasaji, ubaguzi au shughuli ambazo ni kinyume cha sheria, akaunti hiyo inaweza kulemazwa na mamlaka kufahamishwa. Uber itatoa maelezo yoyote ambayo mamlaka itayahitaji ili kuwasaidia katika uchunguzi wao.
Uber inajitahidi kuunda mazingira salama na mazuri kwa abiria na madereva washiriki. Maelekezo haya ni muhimu na hutekelezwa kwa faida za wale wote ambao wanatumia Uber. Madereva na abiria wanahimizwa kujifahamisha Maelekezo haya ya Jamii.

                                                                                 
-Mwisho-

Kuhusu Uber
Misheni ya Uber ni kuwasaidia watu kusafiri kwa kubofya kitufe tu - mahali popote na kwa ajili ya kila mtu. Tulianza mwaka wa 2009 ili kutatua tatizo rahisi - unawezaje kusafiri kwa kubofya kitufe? Miaka sita na zaidi ya safari bilioni mbili baadaye, tumeanza kukabiliana na changamoto nyingine kubwa zaidi: kupunguza msongamano na uchafuzi katika miji yetu kwa kuwabeba watu zaidi katika magari machache.

Mtandao wa Uber unapatikana sasa katika zaidi ya miji 475 katika nchi 75 katika mabara 6. Ili kuomba usafiri, lazima watumiaji wapakue app ya bure ya Android, iPhone, Blackberry 7, au wajisajili kwenye tovuti ya Uber www.uber.com/go. Ikiwa una maswali tembelea www.uber.com

Mtandao wa Jamii:
Twitter: @Uber_Tanzania | Facebook: /UberTanzania |Instagram: @Uber_Tanzania
Kwa maelezo zaidi:
Janet Kemboi - Uber Communications East Africa
Barua pepe: jkemboi@uber.com

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.