HABARI ZA KIJAMII

KUJUA YALIYOJILI KWENYE RIPOTI YA NUSU MWAKA YA HAKI ZA BINADAMU SOMA HAPARipoti ya nusu mwaka na haki za binadamu iliyozinguliwa leo Jumatatu na Kituo cha Sheria na Haki Binadamu (LHRC) inaonyesha bado hali si nzuri nchini.

Mkurugenzi mtendaji wakituo cha sheria na haki za binadamu Bi. Helen Kijobisimba akiongea na waandishi wa habari kabla ya kuzindua ripoti ya nusu mwaka ya haki za binadamu mapema leo jijini dar es salaam
Akizindua ripoti hivyo leo jijini dar es Salaam, Mkurugenzi wa LHRC, Dk Heleni Kijo-Bisimba amesema inaonyesha kuna ukiukwaji mkubwa wa haki ya kuishi kutokana na watu wengi kuuawa kwa sababu mbalimbali.

Amesema katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Juni, watu kadhaa wameuawa kwa sababu mbalimbali, ikiwamo tuhuma za ushirikina na watu kujichukulia sheria mkononi.

Mtafiti toka kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC) Bw. Fundikila Wazambi akichambua ripoti ya nusu mwaka ya haki za binadamu mapema leo jijini Dar es salaam
"Watu 115 wameuawa wakituhumiwa ni washirikina, kati ya vifo hivyo 23 vimetokea mkoani Tabora ambao unaongoza, ukifuatiwa na  Kigoma wenye vifo 23 na Kagera vifo 11," amesema Dk Kijo-Bisimba.

Baadhi ya waandishi wa habari na wafanyakazi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu wakifuatilia kwa umakini zoezi la uwasilishwaji wa ripoti ya nusu mwaka ya haki za binadamu mapema leo jijini Dar es salaam.
Amesema matukio ya wananchi kujichukulia sheria mkononi nayo yamerudi kwa kasi kwani taarifa za Polisi zinaonyesha kuwa watu 479 wameuawa na wananchi wenye hasira.
mkoa wa Dar es salaam ndiyo unaongoza kwa matukio hayo kwa kuwa na vifo 117 , ukifuatiwa na Mbeya vifo 33, Mara 28 na Geita 26.
"Taarifa ya kipindi hiki inaonyesha ukiukwaji mkubwa wa haki za raia hususani haki ya kuishi, lakini pia ukiukwaji mkubwa wa haki za makundi maalum hasa wanawake na watoto," amesema.

Amesema pia kuna vifo tisa ambavyo vinahusisha vyombo vya dola, ingawa Jeshi la Polisi katika taarifa yake inaonyesha ni mtu mmoja pekee ndiye aliuawa akiwa mikononi mwao.

About vicent macha

Post a Comment
Powered by Blogger.