SIASA

KUKAMATWA KWA MBUNGE MDEE,ACT WAZALENDO WAIBUKA NA HILI LEONi siku nne tu zimepita tangu Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi kuagiza kukamatwa kwa Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (CHADEMA) akidaiwa kutoa kauli za kumkashifu Rais.

Leo July 8, 2017 Ngome ya Vijana wa Chama cha ACT Wazalendo imelaani na kupinga walichodai tabia ya baadhi ya viongozi wateule wa Rais kuwaweka kizuizini viongozi wa kisiasa.

Mwenezi wa Ngome hiyo, Karama Kaila amesema hadi sasa kuna viongozi kadhaa wa kisiasa wameshikiliwa katika vituo vya Polisi kwa sababu ya amri za Wakuu wa Mikoa na Wilaya.

“Ngome ya Vijana wa Chama cha ACT Wazalendo inalaani na kupinga vikali tabia ambayo inaonekana kuzidi kumea mizizi siku za hivi karibuni ya baadhi ya viongozi wateule wa Rais hususan Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kutumia vibaya Sheria ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa kwa kumrisha kukamatwa na kuwekwa kizuizini kwa saa 48 viongozi wa kisiasa ambao wanaonekana kuwa na maoni tofauti na viongozi hao.” – Karama Kaila.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.