Thursday, July 27, 2017

LIPUMBA AKITOA SABABU ZA WABUNGE VITI MAALUM WA CUF KUTIMULIWA

Baada ya jana Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Job Ndugai kuridhia kufutwa Uanachama kwa Wabunge 8 CUF. Mwenyekiti wa CUF, Ibrahim lipumba amesema kuwa waliwafukuza wanachama hao kwa kuwa walikihujumu Chama hicho.

Prof. Lipumba ameyazungumza hayo leo wakati akizungumza na wana habari huku akisema kuwa Katiba inasema kuwa Msemaji Mkuu wa mambo ya CUF ni mwenyekiti CUF Taifa.
“Tulifanya maamuzi ya kuwafukuza uanachama Wabunge wa Viti Maalum wanane, na tulifanya hivyo kwasababu wamekuwa wakikihujumu chama. Katiba inasema Msemaji Mkuu wa mambo ya CUF ni Mwenyekiti wa Taifa,” amesema Prof. Lipumba.
“Wao wakajenga mazingira ya kwamba Freeman Mbowe wa Chadema awe Msemaji wa CUF, alafu wanadiriki kukaa na viongozi wa Chadema na mwenyekiti anasema ye ni Makamu Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani ametumwa na Mwenyekiti wake wa Kanda ya Pwani Bw. Fredrick Sumaye kuzindua operesheni ondoa msaliti Buguruni na wabunge wa CUF wapo. Kubenea anasema hawa viongozi wa CUF tumewakaribisha tu hiki ni kikao cha Chadema hao viongozi wa CUF kwamba wao ndio wanaendesha Operesheni ya ondoa msaliti Buguruni,” alisisitiza Prof.

No comments: