Friday, July 7, 2017

MAKAMU WA RAIS AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUUAGA MWILI WA MAREHEMU SHEBUGE


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha kumbukumbu cha maombelezo ya Marehemu Hassan Rashid Shebuge,nyumbani kwa marehemu Mbagala Rangi Tatu.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili Marehemu Hassan Rashid Shebuge,nyumbani kwa marehemu Mbagala Rangi Tatu.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akitoa salaam za Serikali mara baada ya kutoa heshima za mwisho kwa Marehemu Hassan Rashid Shebuge.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Baba Mdogo wa Marehemu Hassan Rashid Shebuge, Bw. Juma Hassan Shebuge mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Mbagala Rangi Tatu.

Mwili wa Marehemu Karani wa Baraza la Mawaziri, Hassan Rashid Shebuge aliyefariki Julai 06, 2017 katika Hospitali ya Taifa Muhimbini Jijini Dar es salaam alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabuumeagwa nyumbani kwake, Mbagala Rangi Tatu na kusafirishwa kupelekwa nyumbani kwao, Bumbuli Tanga kwa mazishi.

Kabla ya kufikwa na Mauti, inaelezwa kuwa Marehemu Shebuge aliugua ghafla akiwa nyumbani kwake, Mbagala Majimatitu mnamo Julai 03, 2017 na kukimbizwa katika Hospitali ya Rangi tatu ili kupatiwa huduma ya dharula na baadae kuhamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbini kwa matibabu zaidi hadi hapo matuti yalipomfika.

Kwa mujibu wa taarifa ya kitaalam iliyotolewa na madaktari, inaelezwa kuwa Maremu Shebuge alipatwa na shinikizo la damu ambalo limepeleka kupoteza kwake maisha.
Tunamuombea kwa Mwenyezi Mungu, aiweke roho ya Marehemu Hassan Rashid Shebuge mahapa pema peponi, Amin.

No comments: