Wednesday, July 5, 2017

MANJI ASOMEWA MASHTAKA AKIWA HOSPITALINI

Leo July 5 2017 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ililazimika kuhamia kwa muda  katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete(JKCI) iliyopo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, na kumsomea mashtaka saba ya uhujumu uchumi, mfanyabiashara Maarufu Yusufu Manji na wenzake watatu. Hatua hiyo imefikiwa baada ya Manji kushindwa kufika mahakamani kwa ajili ya kusomewa mashtaka kutokana na kulazwa katika taasisi hiyo.

Akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, jopo la Mawakili Waandamizi wa serikali wakiongozwa na Mutalemwa Kishenyi, Nassoro Katuga na Tulumanywa Majigo.
Washtakiwa hao wanadaiwa walijipatia bidhaa isivyo halali mnamo Juni 30,2017 katika maeneo ya Chang’ombe A Temeke Jijini Dar es Salaam walikutwa na askari polisi wakiwa na mabunda 35 ya vitambaa vinavyotumika kutengeneza sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) zenye thamani ya Sh milioni 192.5 ambazo zilipatikana isivyo halali.
Katika shitaka jingine inadaiwa washtakiwa hao walikutwa na mhuri wa serikali wa JWTZ isivyo halali Juni mnamo 30,2017 ambao umeandikwa” Mkuu wa Kikosi 121 kikosi cha JWTZ” bila ya kuwa na uhalali na kwamba kitendo hicho kinahatarisha uchumi na Usalama wa nchi.
Washtakiwa hao hawakutakiwa kujibu mashtaka hao Kwa sababu makosa hayo hapo chini ya uhujumu uchumi na Usalama wa taifa. Hata hivyo, upande wa mashtaka uliwasilisha hati ya pingamizi la dhamana kutokana Kwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma(DPP).
Katika hati hiyo, DPP alidai,ikiwa washtakiwa hao watapewa dhamana wanaweza kuhatarisha Usalama na maslahi ya nchi na Kwa mujibu wa sheria kulingana na shtaka la 1 na 2, mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kisheria ya kutoa dhamana Kwa washtakiwa hao.
Hata hivyo, hoja hiyo ilipingwa na upande wa utetezi ukiongozwa na Wakili Hudson Ndusyepo alidai kuwa mashtaka hayo yanaiondolea mahakama kuwafikiria wateja wake dhamana.
Kutokana na kuwepo Kwa mabishani ya kisheria,Hakimu Shaidi alisema masuala yanapaswa kuongelewa kwenye mahakama yenye mamlaka kisheria Kwa sababu DPP hajaipa mamlaka ya kisheria ya mahakama ya Kisutu kusikiliza maombi ya dhamana. Kutokana na hali hiyo, kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 19,mwaka huu Kwa ajili ya kutajwa.

No comments: