Thursday, July 6, 2017

MKONGWE WA MUZIKI WA BAND TANZANIA SHABANI DEDE AMEFARIKI DUNIA LEO ASUBUHI


Mwanamuziki mkongwe wa Band ya Msondo Ngoma Shaaban Dede amefariki dunia mapema leo asubuhi akiwa anapokea matibabu katika Hospitali ya Muhimbili.

Mtoto wa marehemu Hamad Dede amethibitisha kifo cha Shaaban Dede akisema mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu Mbagala, DSM na kwamba ratiba na taratibu zote zitatangazwa mara baada ya kukamilika.

No comments: