.

BURUDANI

OMMY DIMPOZ - NAWEZA KUFANYA WIMBO NA MSANII YEYOTE WA WCB


Msanii wa bongo fleva Ommy dimpoz ambaye anamiliki Record Label ya PKP lakini pia ni msanii mpya kisaini kwenye Label ya Rockstar 4000 ambayo inamilikiwa na mwanadada Seven Mosha ambayo ndani yake kuna wasanii kama Ally kiba na Baraka The Prince.

Ommy Dimpoz alisema kuwa anaweza kufanya ngoma na msanii wa WCB endapo atahitajika kufanya hivyo. “Kama itatokea kuna wimbo wa WCB ambao unanihitaji mimi kufanya bila shaka nitafanya kwa kuwa sina shida nao” alisema Dimpoz


Dimpozi aliyasema jana alipokuwa akihojiwa kwenye kipindi cha Friday Night Live cha East Afrika Tv na East Afrika Radio akijibu swali la shabiki wake Esta Tesha toka Arusha.

About vicent macha

Post a Comment
Powered by Blogger.