.

BURUDANI

PETER MSECHU - MIMI NAFUMANIWA KILA KUKICHA TUMBO SIO SABABU YA KUSHINDWA KAZI

Mwimbaji wa Bongofleva Peter Msechu amefunguka kuhusu wanaosema juu ya mwili wake kuwa amejiachia sana na kunenepa kupita kiasi huku wengi wakimshauri kupunguza mwili kwa kufanya mazoezi jambo ambalo analipinga.

Akiwa kwenye XXL ya Clouds FM Peter Msechu amedai kuwa yeye ni Brand na mtu yeyote mwenye mtazamo wa kibiashara amuone wafanye biashara ili kupunguza maneno mengi huku akisema pia kuwa ukimya wake kwenye muziki ni kutokana na kuwa na shughuli nyingine zinazomuingizia kipato tofuati na muziki.
“Watu wanaongea kuhusu mwili wangu, Msechu ni brand tusiongee sana kama unaweza na una Gym njoo tukae chini tufanye kazi pamoja. Kila kukicha natumiwa massage hawa wanaouza madawa wananiambia wana shida ‘Nataka unywe dawa utapungua’ mara ‘Sasa hivi huwezi kazi utakimbiwa na wanawake’. Jamani! Mimi nafumaniwa kila kukicha kama unaamini siwezi kazi, uliza wale ninaofumaniwa nao.
“Vitu ambavyo watu hawajui kuwa mimi napata kazi nyingi sana nje ya muziki. Nafanya sound engineering na ku-train vocal. Unaweza kushangaa show yangu ya mwisho Fiesta ilikuwa mwaka juzi, ndio maana unaona najisogeza sana.” – Peter Msechu

About vicent macha

Post a Comment
Powered by Blogger.