BURUDANI

QUICK ROCKA AMJIBU RUFFA ALIPOSEMA SWITCHE WANATUMIA KAZI ZAKE BILA KUMLIPA

Kwenye Uherd leo July 10, 2017 mtangazaji Soudy Brown ameinasa hii ya Quick Rockakudaiwa kutomlipa Producer wake wa zamani Luffa kwenye baadhi ya kazi alizofanya kabla hajaondoka na kutoshirikishwa wakati nyimbo hizo zinapotoka ukiwemo wimbo wa OMG.
Soudy amewatafuta Luffa na Quick Rocka:>>>”Ndio mara ya kwanza na sijui kwa nini. Tangu niondoke, project zangu wanatumia wanavyotaka wao. Mimi lazima wanipe taarifa lakini wanazingua kiukweli.” – Luffa.
Kwa upande wa Quick Rocka alipotafutwa alikuwa na haya ya kuyasema:>>>”Hayomalalmiko mbona mimi hajaniambia chochote? Kwa nini anakuja kulalamika kwenye media na anajua mimi nina ofisi, mbona hajakuja kunambia? Unajua kuna vitu vingine hutakiwi kuviongea. Mimi sitaki kuchafua chochote kuna vitu vingine tunaviacha kama vilivyo.” – Quick Rocka.

About vicent macha

Post a Comment
Powered by Blogger.