MICHEZO

TAIFA STARS YAWEKA HISTORIA COSAFA,YATWAA NAFASI YA TATU
Taifa Stars imefanikiwa kushika nafasi ya tatu katika michuano ya Kombe la Cosafa baada ya kuichapa Lesotho kwa mikwaju ya penalti.

Stars imeibuka na ushindi wa mikwaju 4-3 dhidi ya Lesotho baada ya dakika 90 za bila kufungana.

Katika michuano hiyo inayopigwa nchini Afrika Kusini, Shiza Kichuya ndiye aliyekuwa wa kwanza kupiga na kukosa.

Hata hivyo baadaye Lesotho walipoteza penalti mbili, moja ikigonga mwamba na nyingine kipa Said Mohamed ‘Nduda’ akikoa moja.

Waliofunga upande wa Stars ni Himid Mao, Simon Msuva, Abdi Banda na Raphael Alpha aliyema malizia kazi.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.