Saturday, July 8, 2017

TANZIA - JENERALI MSTAAFU JOSEPH NKAISSERY AMBAE ALIKUWA WAZIRI WA USALAM WA KENYA AMEFARIKI DUNIA


Waziri wa usalama nchini Kenya Jenerali Mstaafu Joseph Nkaissery amefariki dunia.

Waziri huyo amefariki dunia saa chache baada yake kulazwa katika hospitali ya kibinafsi ya Karen kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu.
Taarifa za kifo chake zimetangazwa na mkuu wa utumishi wa umma Bw Joseph Kinyua mwendo wa saa kumi na moja alfajiri.
“Ni kwa huzuni kubwa na mshangao kwamba tunatangaza kifo cha ghafla cha Waziri wa Usalama wa Ndani Jenerali Mstaafu Joseph Nkaissery,” taarifa ya Bw Kinyua imesema.
“Taifa litaendelea kupashwa habari zaidi punde maelezo yatakapopatikana.”
Jenerali Joseph Kasaine ole Nkaissery, 67, amefariki siku chache baada ya mwanasiasa mkongwe G.G. Kariuki aliyekuwa seneta wa jimbo la Laikipia kufariki dunia.

No comments: