Wednesday, July 12, 2017

WANAHARAKATI WASHAURIWA KUTUMIA VIZURI VYOMBO VYA HABARI KATIKA KUTATUA CHANGAMOTO ZINAZOIKABILI JAMII.

Mtandao wa kijinsia wa TGNP umeendesha semina kwa wanaharakati wake ambapo wameshauri kutumia vizuri vyombo vya habari ili kupaza sauti juu ya changamoto zinazoikabili jamii ili hatua stahiki zifuatwe katika kuzitatua changamoto hizo.
Muhariri wa gazeti la Mwanahalisi Bi. Pendo Omary akitoa elimu kwa wanaharakati jinsi ya kutatua changamoto mbali mbali zinazoikabiri jamii kwa kutumia vyombo vya habari.
Ushauri huo umetolewa leo na muhariri wa gazeti la mwanahalisi,ambaye pia ni mwanaharakati wa mtandao huo Bi.Pendo Omary  wakati wa semina ya mafunzo iliyoendeshwa na mtandao huo katika ofisi zake za mabibo Jijini Dar es salaam.

Bi. Pendo amesema kuna fursa nyingi za kutumia kwenye vyombo vya habari ambazo wanaharakati wanaweza kuzitumia katika kuzungumzia kero ama changamoto ili taasisi husika au serikali iweze kuzipata na kuzitatua kwa wakati.
Wanaharakti mbalimbali wakifuatilia semina kwa umakini iliyoandaliwa na Mtantao wa jinsia TGNP. iliyofanyika mapema jana jijini Dar es salaam
''kuna fursa nyingi sana kupitia vyombo vya habari ambazo zitaweza kusaidia katika kupaza sauti juu ya  mambo mbali mbali ikiwemo unyanyasaji na ukandamizwaji wa wanawake ambapo ndipo sehemu kubwa inatuhusu kama wanaharakati''alisema.

Akizitaja fursa hizo kuwa ni pamoja na uandishi wa barua kwa wahariri na maoni uchapishwa katika kurasa za magazeti na kusomwa na watu wengi katika jamii,Bi. pendo pia alielezea juu ya upigaji simu moja kwa moja wakati wa vipindi vya redio kuwa ni njia inayosaidia katika kupaza sauti juu ya changamoto zinazoikabili jamii lakini pia ni  moja ya njia ya kuendeleza mapambano juu ya mambo  tofauti ikiwemo unyanyasaji na ukandamizaji wa wanawake.
Muhariri wa gazeti la Mwanahalisi Bi. Pendo Omary akitoa elimu kwa wanaharakati mbalimbali jana jijini Dar es salaam
Aidha,aliwaasa wanaharakati kutokua waoga wa kuzungumza ukweli kupitia vyombo hivi kwani ni jukwaa lao katika kufikisha taarifa zinazolenga kuibua changamoto katika jamii zao licha ya kuwa na ukandamizwaji wa uhuru wa kujieleza,rushwa zinazotolewa na baadhi ya viongozi ili kuwaziba midomo wananchi na hata kuhojiwa na vyombo vya usalama pindi watapofahamu kuwa zimetolewa taarifa ambazo hazikupaswa zitoke.


Pia,Bi pendo aliwatahadhalisha wanaharakati hao kutotoa taarifa zenye lengo la kejeli,uchochezi baina ya mtu na mtu au kikundi,kumdhalilisha mtu kwa lengo la maslahi binafsi au kundi la watu kwani kitendo hiko kitaweza kuhatarisha usalama wake na lengo la fursa ya matumizi ya vyombo vya habari itakuwa haijatimizwa.







No comments: