Thursday, July 6, 2017

WANENE ENTERTIMENT KUSAINI MKATABA NA ZIFF WA KUDHAMINI KIPENGELE CHA VIDEO BORA YA AFRIKA MASHARIKI

Kampuni ya Wanene Entertainment kwa kushirikiana na Tamasha la nchi za Jahazi (ZIFF) wamesaini makubaliano ya kudhamini kipengele cha video bora ya Afrika Mashariki, ambapo mshindi wa kipengele hicho atapata fursa ya kurekodiwa na kutengenezewa video bure na kampuni ya Wanene Entertainment.

Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Masoko kutoka ZIFF Isihaka Mlawa amesema ZIFF wanayofuraha kubwa kwa kampuni ya Wanene Entertainment kudhamini kipengele cha video bora ya Afrika Mashariki, itakayo zishirikisha nchi tatu za Tanzania, Uganda na Kenya.
 Mlawa ameeleza kuwa kwa miaka mingi ZIFF ilikuwa imejikita upande mmoja wa filamu, ndiyo maana wakaamua kuanzisha kipengele hicho ambapo kwa mwaka jana alishinda Fid Q na  video yake ya Walk it Off ambayo ilirekodiwa nje ya Tanzania, ila kwa mwaka huu video zote zilizo chaguliwa zimerekodiwa na kufanyiwa video na waandaaji na waongozi kutoka kwenye nchi zao.
Mlawa amewataja wasanii wanao shindanishwa katika kipengele hicho cha Video Bora ya Afrika Mashariki kuwa ni Rayvanny kutoka Tanzania na wimbo wake ya Natafuta Kiki, Darasa na wimbo wake ya Muziki na Jux na wimbo wake ya Umenikamata, kutoka Uganda ni Eddy Kenzo na wimbo wake ya Jubilation, Sheebah Karungi na wimbo wake wa Nkwatako pamoja na A Pass na wimbo wake wa Gamululu, huku kutoka Kenya msanii Everlast na wimbo wake  Gudigudi, Aviril na wimbo wake wa Uko, Nai Boi na wimbo wake wa Problem huku  Nyashinski akishindanishwa kwa wimbo wake wa  Now You Know.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Wanene Entertainment Darsh Pandit ameeleza kuwa wameamua kudhamini kipengele hicho ili kuyatangaza maeneo ya Tanzania na Afrika kwa ujumla kwani video itafanyika hapa nchini, pia itakuwa ni sababu ya wasanii kutoka nje kuja kufanya kazi kwenye mazingira ya Tanzania.
Pandit ameongeza kuwa wamejipanga kufanya video nzuri kwa mshindi atakayeshinda tuzo hiyo kwani wanavifaa vya kisasa kwa ajili ya kazi hiyo.
Wanene Entertainment wanajihusisha na masuala mbalimbali ya uzalishaji wa video na audio, matangazo na kusimamia wasanii ambapo msanii Chin Bees ni moja ya wasanii ambao wamefanya kazi na kampuni hiyo na video yake ya Pepeta. 

No comments: