Wednesday, July 26, 2017

Watanzania wahamasishwa kutumia Rajisi ya kwetu(Domain),kila mtanzania aanze kutumia .TZ mitandaoni

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ambandusi Ngonyani akizungumza na wanahabari pamoja na wageni mbalimbali waliohudhuria katika mkutano huo Jijijini Dar es salaam leo.Picha na Exaud Mtei
Katika kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa na Utambulisho wa Kudumu hasa katika mitandao,serikali imewataka watanzania kujenga utamaduni wa kutumia Rajisi ya Tanzania (Domain) ambayo ni .TZ badala ya kuendelea kutumia Domaini za mataifa mengine bila kunufaika na matumizi hayo.

Akifungua mkutano wa Jumuiya ya watoa Huduma kwenye mitandao ulioshirikisha wamiliki wa Rajisi mbalimbali Africa kama .ke, .tz,.uk na nyingine Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ambandusi Ngonyani amesema kuwa Nchini ya Tanzania imekuwa nyuma sana katika kutumia Rajisi yake ya nyumbani ambayo ni .TZ ukilinganisha na mataifa yanayotuzunguka kama Kenya na mengine jambo ambalo linatajwa kuendelea kupoteza utambulisho wa Taifa letu katika mitandao.
Naibu Waziri huyo amesema kuwa mpaka sasa nchini Tanzania watumiaji wa mtandao ambao wamejisajili katika matumizi ya Rajisi ya nyumbani yani .TZ wanafikia elfu 14 ukilinganisha na majirani zetu Kenya ambao wanafika elfu 60, ambapo amewaasa watanzania kijijengea utamaduni wa Kutumia utambulisho wa nyumbani.
Ameeleza kuwa matumizi ya Rajisi ya Nyumbani yana manufaa makubwa sana kwa watanzania hasa wafanyabishara ambao wanafanya biashara kimataifa kwani itawajengea kuaminika na wateja wao kwa kuwa wanatambulika nchi wanayotoka tofauti na kutumia Rajisi za mataifa mengine ambapo wateja watashindwa kuelewa wewe unatoka nchi gani kutokana na Rajisi yako.
Mkurugenzi Mtendaji wa TZNIC ambao ndio wanaohodhi Rajisi ya .TZ akizungumza na wanahabari kuhusu mambo mbalimbali yatakayojadiliwa katika mkutano huo
Akizungumzia Rajisi ya Tanzania na matumizi yake amesema kuwa kwa sasa Rajisi ya .TZ ambayo ndiyo Rajisi maalum ya watanzania inatolewa na TZNIC ambao wanatoa kwa gharama za zisizozidi elfu 25 kwa mwaka ambapo amesema kuwa Gharama hizo ni kwa lengo la kusaidia kujiendesha wakati wanaanza kwa kuwa bado hawaajaanza kupata matangazo huku akiweka wazi kuwa kadiri muamko wa watanzania utakavyozidi kuwa mkubwa gaharama hizo zitapungua kwa kiasi.

Akizungumza nje ya Mkutano huo Mkurugenzi Mtendaji wa TZNIC ambao ndio wanaohodhi Rajisi ya .TZ Eng.Abibu Ntahigiwe amesema kuwa Lengo kuu la mkutano huo ni kujenga ushirikiano wa karibu baina ya wamiliki wa Rajisi afrika pamoja na kubadilishana uzoefu kuhusu maswala ya mitandao,ambapo mkutano huo unafanyika Tanzania ukiwa ni mkutano wa  Tano kufanyika Barani Africa.

No comments: