.

SIASA

Breaking News--CUF YA MAALIM YAPIGWA CHINI MAHAKAMANI


Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam leo August 4, 2017 imetupilia mbali pingamizi la Wabunge 8 wa Viti Maalumu waliofutwa uanachama na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Prof. Ibrahim Lipumba ya kutaka wabunge wateule 8 wasiapishwe na Bunge.

Uamuzi huo, umetolewa na Jaji Lugano Mwandambo ambaye amesema ametupilia mbali pingamizi hilo la zuio la kuapishwa kwa Wabunge hao 8 na kwa mantiki hiyo, Wabunge wapya walioteuliwa kuziba nafasi zao wanaweza kuapishwa.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.