Wednesday, August 2, 2017

MGODI WA DHAHABU WA ACACIA BULYANHULU WALIPA MILIONI 226 KWA AJILI USHURU WA HUDUMA KWA HALMASHAURI YA NYANG’HWALE


Kushoto ni Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu Graham Crew akikabidhi hundi ya shilingi milioni 226 kwa Mkuu wa wilaya ya Nyang'wale Hamim Gwiyama kwa ajili ya ushuru wa huduma kwa halmashauri ya wilaya ya Nyang'wale katika ukumbi wa mkutano Nyang’hwale mkoani Geita.
Zoezi la kukabidhi hundi likiendelea.
Mbunge wa Jimbo la Nyang’hwale akizungumza wakati wa zoezi hilo la kupokea hundi hiyo ambapo alisema Wananchi wa Nyang’hwale wana matumaini sana na Mgodi wa Bulyanhulu na wameipongeza Acacia kwa ushirikiano na kwa kutekeleza ahadi ya kulipa ushuru wa huduma malipo yatatumika katika kutekeleza miradi ya wananchi  huku akiimba Acacia iendelee kusaidia miradi mbalimbali mingine.

Baadhi ya Maofisa wa Halmashauri ya Nyang’hwale wakiwa ukumbini.
Kutoka Kulia, Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu Graham Crew, Kaimu Meneja wa Mahusiano ya Jamii Onesmo Kabeho na Afisa Mahusiano ya Jamii Zuwena Senkondo wakiwa kwenye ukumbi wa mkutano Nyang’hwale pamoja na wakuu wa idara za Wilaya ya Nyang’wale.
*****


Mgodi wa Dhahabu wa Acacia Bulyanhulu (BGML) uliopo katika Halmashauri ya Msalala Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga, jana Agosti 1,2017  umekabidhi hundi yenye thamani ya Shilingi Milioni Mia Mbili na Ishirini na Sita, Laki Tisa Ishirini na Nane Elfu na Mia Moja Kumi na Tano na senti Sabini na Sita (226,928,115.76) kwa ajili ya Ushuru wa Huduma kwa Halmashauri ya Nyang’hwale.

 Kiasi hicho cha fedha ni asilimia 33% ya malipo ya ushuru wa huduma kwa ajili ya kipindi cha miezi sita yaani Januari hadi Mwezi Juni mwaka huu wa 2017, kiasi ambacho ni asilimia 0.3 ya ukokotoaji wa ushuru wa huduma wa mgodi huo kwa kipindi husika.

Akikabidhi hundi hiyo, Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu  Graham Crew alisema jumla ya malipo ya ushuru wa huduma kwa kipindi cha miezi sita iliyopita ni shilingi za kitanzania, Milioni Mia Sita Themanini na Saba, Laki Sita na Sitini Elfu, Mia Tisa Hamsini na Sita na Senti Themanini na Nne (687,660,956.84). 

Alisema malipo hayo yamegawanywa katika Halmashauri mbili kwa mujibu wa makubaliano na serikali ambapo Halmashauri ya Msalala inapata asilimia 67% na Nyang'hwale 33% ". Hivyo katika kiasi hicho, Halmashauri ya Wilaya ya Msalala imelipwa shilingi 460,732,841.08, wakati Nyang'hwale imelipwa Shilingi 226,928,115.76”.

 Alisema hadi sasa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu umelipa zaidi ya shilingi Bilioni 10,200,000,000 tangu mwaka 2000 kama kodi ya ushuru wa huduma ambapo Kampuni ya Acacia ilianza kutoa malipo ya ushuru wa huduma wa asilimia 0.3 ya mapato ghafi kwa halmashauri husika mwaka 2014, kutoka kiasi cha Dola 200,000/= kwa mwaka iliyokuwa inalipwa kama kodi ya ushuru wa huduma miaka ya nyuma.

 Aidha Crew alisema Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu unaendelea kuwa na matarajio ya kuchangia kuimarisha sekta ya viwanda kwenye uchimbaji madini katika Wilaya ya Nyang’hwale huku ikiendelea kutekeleza mkakati wa Jamii Endelevu wa Acacia ulioanzishwa mwaka 2016 kwa kushauriana na wadau.

Alisema Utekelezaji wa Mkakati huo umeanza mwaka 2017 ambapo mkakati huo una lengo la kuchangia maendeleo ya " Jamii Endelevu" ambazo zinanufaika na kukua kwa uchumi ndani ya jamii, jamii ambayo inayo miundombinu ya kijamii na inaishi katika mazingira salama yanayopatikana kupitia ushirikiano wa pamoja wa wadau, wa wazi na wa kujenga ili kujenga mahusiano ya kuaminika. 

Nia ya Mkakati huo ni kujumuisha shughuli zake na mipango ya maendeleo ya jamii na kufanya kazi kupitia ushirikiano ili kukidhi mahitaji ya jamii. Tunaona jukumu letu ni kuunga mkono jamii na serikali katika jitihada zao za kufikia maendeleo endelevu na hivyo mkakati wetu unaendana na Malengo ya Maendeleo ya Umoja wa Mataifa (SDGs). 

No comments: