Thursday, August 3, 2017

Msajili wa Vyama vya Siasa Apinga Maamuzi ya CUF.....Kasema Hamtambui Maalim Seif Kama Katibu Mkuu CUF



Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amepinga maamuzi ya Chama Cha Wananchi (CUF) kuwafukuza Uanachama Wabunge wawili wa chama  hicho Magdalena Sakaya na Maftaha Nachuma na kusema Maalim Seif hatambuliki kama Katibu Mkuu wa CUF.
Msajili wa Vyama vya Siasa amesema hayo leo wakati akijibu barua iliyowasilishwa ofisini kwake na Katibu Mkuu wa (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad akimtaka msajili wa vyama kuwavua nafasi ya Ubunge viongozi hao.
Kufuatia barau hiyo Msajili wa Vyama Vya Siasa amesema kuwa hamtambui Maalim Seif Sharif Hamad kama Katibu Mkuu wa CUF na kusema yeye anawatambua Mwenyekiti wa CUF, Professa Ibrahim Lipumba pamoja na Magdalena Sakaya kama mtu mwenye dhamana ya Katibu Mkuu wa CUF
Chama Cha Wananchi (CUF) kipo katika mgogoro wa pande mbili upande wa Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif pamoja na upande wa Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Msajili wa Vyama Vya Siasa nchini Profesa Ibrahim Lipumba, kufuatia mgogoro huo mpaka sasa kuna kesi mbalimbali ambazo zimefunguliwa mahakamani kutokana na mvutano wa pande hizo zote mbili.  ==>Hapo chini ni barua ya msaili wa vyama akijibu bara ya Maalim Seif

No comments: