Sunday, August 13, 2017

TAMKO LA VIJANA WA ACT –WAZALENDO KUADHIMISHA KILELE CHA SIKU YA VIJANA DUNI


LEO  tarehe 12/08/2017 mataifa mbali mbali  duniani yanaadhimisha kilele cha siku ya vijana duniani.Ni zaidi ya miaka 18 sasa tangu umoja wa mataifa uitangaze siku ya August 12 kuwa ni siku maalum ya vijana duniani

.Umuhimu wa vijana katika maendeleo endelevu ya mataifa ndio chanzo kikuu cha kutambulika rasmi kwa siku hii muhimu.
Vijana wa ACT-WAZALENDO tunaungana na vijana wenzetu wote Duniani katika kuazimisha siku hii muhimu yenye kauli mbiu ‘VIJANA NI SEHEMU YA KUTENGENEZA NA KULINDA AMANI’ Sisi sote ni mashahidi na wahubiri wa kauli mbiu hii kwa kuwa tunafahamu hakuna maengeleo endelevu yatakayopatikana bili ya Amani na usalama.Kwa kutambua umuhimu wa siku hii kwa vijana,Ngome ya vijana  ACT-WAZALENDO tunatambua Vijana kuwa sehemu ya kutengeneza Amani na usalama, ni matokeo ya vichocheo vya mambo mengi yatakavyowafanya vijana washiriki katika kutengeneza Amani na usalama wa nchi yetu.
Tunaamini Uhuru wa vijana kujieleza, ushirikishwaji wa vijana katika maamuzi pamoja upatikanaji wa Ajira kwa vijana, ni miongoni mwa mambo muhimu yatakayotupelekea vijana tuwe sehemu ya kutengeneza Amani na usalama wa nchi yetu.
Vijana wa ACT-WAZALENDO,Tunaitaka serikali kwa kutambua mchango wa vijana katika kutengeneza Amani na usalama wa taifa letu,ichukuwe jitihada za dhati za kuhakikisha inatengeneza mazingira rafiki kwa vijana kuendelea kuwa kizazi chenye uhuru wa kujieleza na kuhoji mambo ya msingi katika taifa letu.Kufanya hivi ,si kama kutalisaidia taifa kuwa na viongozi wazuri na wazalendo katika ofisi zetu,bali litaamsha hali ya wahojiwa na wakosolewa kujitathimini na kufanya kazi kwa uzalendo mkubwa.Tunasema haya kwa kutambua namna vijana tunavyonyimwa fursa ya kushiriki katika majukwaa ya kusikiliza na kujieleza kwa kile kinachoitwa marufuku ya mikutano ya kisiasa kwa wasiokuwa viongozi wamaeneo husika.Vijana tusiokuwa wabunge wala madiwani,Hatuna hatuna nafasi ya kujifuza siasa za majukwaani kwa vitendo kwa sasa.
Jambo lingine muhimu ambalo ni kichocheo cha vijana kuwa sehemu ya kutengeneza Amani na usalama wa taifa letu ni Ajira,Agenda hii ya ajira kwa vijana imekuwa ni tatizo sugu na tumewasikia viongozi wetu wakiendelea kulisemea kila siku.Vijana wa ACT-WAZALENDO hatutaki tena kuliongelea suala hili kisisa kwa kuwa tunajua ni namna gani maelfu ya vijana waliomaliza vyuo vikuu hawajafanikiwa kupata ajira kutokana na mazingira halisi ya ufumo wa ajira za serikalini ambazo ndio zinategemewa na vijana wengi.Tunajua serikali imeshindwa na haina uwezo wa kuwaajiri vijana wote wanaomaliza elimu katika ngazi mbalimbali kwa sababu nyingi tunazoelezwa kikiwa pamoja na sababu za kibajeti.
Kwa masikitiko makubwa,hata sekta binafsi ambayo tulianza kuiona kama mkombozi kwa vijana wengi kuajiriwa huko,nayo imeanza kupunguza wafanyakazi kwa kasi ya ajabu kwa sababu mbalimbali ikiwemo za serikali kutoa kauli na misimamo ya kikodi na mengineyo bila kuwapa wafanyabiashara muda wa maandalizi wa kutosha.Sote tunakumbuka sakata la vituo vya kuuza mafuta na maamuzi ya serikali ya matumizi ya EFD.Ni idadi kubwa ya vijana walipoteza ajira zao za kuhudumia vituo vya mafuta na kuishi bila Amani kwa kipindi cha maamuzi haya.Vijana wa ACT-WAZALENDO tunaishauri serikali kufanya tathimini za kina pale wanapotaka kufanya maamuzi yanayohusu sekta binafsi ili walau kuepusha mihangaiko na mataso kwa vijana walioajiriwa katika sekta binafsi.
Kwa kutambua ukubwa wa tatizo la ajira kwa vijana wa kitanzania,sisi vijana wa ACT-WAZALENDO,Leo hii tunaanzisha rasmi kampeni ya kuwahamasisha vijana wenzetu kuingia rasmi katika Kilimo.Kampeni hii tumeipa jina ‘TUAMUE SASA,KILIMO NI AJIRA’.Serikali imeshindwa kutuajiri maofisini,Twendeni shambani tukalime ,Tuzalishe malighafi ,tukiwa matajiri wa malighafi,matajiri wenye viwanda tunavyoambiwa vinaletwa ,watatutafuta wenyewe.Tunawahamasisha vijana kuungana na kwa pamoja kujiandaa kupitia fursa zilizopo katika maeneo yetu kuzalisha mali shambani.
Ngome ya vijana ya ACT WAZALENDO,Inawataka vijana wote nchini kuacha kulia na ajira za serikalini ambazo hazipo.Tuamue sasa,kilimo kukikimbilia.Mashambani twendeni,mali tukazalishe.Hii ndio namna pekee ya kujikomboa kutoka kwenye kilio kikuu cha ajira.Kampeni hii itakayoongozwa na Vijana wa ACT WAZALENDO itapita kwenye mikoa yote inayozalisha mazao ya chakula na biashara ,Kukutana na vijana kuwahamasisha kushiriki katika kilimo kutokana na mazingira waliyopo.Tutaenda TABORA kuwataka vijana waione Tumbaku ndio muokozi wao,Tanga Katani,Tutawaambia vijana wa kusini Korosho ndi ajira yao,Tutawaambia vijana wa Mbeya wajiandae na vitalu vya Mpunga.Vijana wa Singida na Dodoma wajiandae na Alizeti ili wanyeviwanda vya mafuta wawatafute.Tutawafikia vijana wa maeneo yote ya Tanzania.’TUMEAMUA SASA,KILIMO NI AJIRA’
Chama chetu kinaamnini katika siasa za maendeleo,Sisi vijana wa chama tumeamua sasa kuhamasisha maendeleo endelevu ya vijana wa Tanzania kupitia kilimo,Ili waweze kuwa sehemu ya kutengeneza Amani na usalama wa nchi yetu.
Mwisho tunazitaka sekta zote zinazoambatana na Kilimo zitengeneze mazingira rafiki ya kuwasapoti vijana katika shughuli za kilimo ikiwa pamoja na kuwapatia taarifa za fursa za kuwaendeleza vijana katika kilimo zinazopatikana katika taasisi zao kwa wakati sahihi.Tunatoa wito wa Sera za taasisi za fedha na mashirika yanayojihusisha na kilimo kupitiwa upya ili ziweze kuwasaidia vijana katika shughuli za kilimo.MUNGU IBARIKI TANZANIA,MUNGU TUBARIKI VIJANA WA TANZANIA.
Asanteni
LIKAPO B,LIKAPO
Mratibu Vijana Taifa ACT-WAZALENDO



No comments: