Wednesday, August 2, 2017

Tigo yafungua duka kubwa, la kisasa Dodoma

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Tanzania, Simon Karikari akikata utepe kuzindua duka jipya la kisasa lililofunguliwa leo mkoani Dodoma, Wengine kutoka kulia ni Mkuu wa usimamizi na masuala ya kiserikali wa Tigo,Sylvia Balwire, Meneja usimamizi wa wateja wa Tigo kanda kaskazini, Vitalis Stephen na kushoto ni George Lugata mkurugenzi wa Tigo kanda kaskazini.

Meneja  usimamizi wa wateja wa Tigo kanda kaskazini, Vitalis Stephen akimuonesha Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Tanzania, Simon Karikari baadhi ya simu zinazouzwa kwenye duka jipya la kisasa lililozinduliwa leo mkoani Dodoma . Pembeni ni mkuu wa huduma kwa wateja wa Tigo Dodoma,Scolastica Kisori.

Mteja akipata huduma mara baada ya uzinduzi wa duka jipya la kisasa lililofunguliwa leo mkoani Dodoma,

Mteja akipata huduma mara baada ya uzinduzi wa duka jipya la kisasa lililofunguliwa leo mkoani Dodoma,
 Dodoma,  Agosti 1, 2017- Kampuni inayoongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali, Tigo Tanzania imeendelea kuishi kulingana na ahadi yake ya kuwapatia  wateja huduma wanazozifikia kwa urahisi zaidi kwa huduma za Tigo kwa kufungua duka la huduma kwa wateja ambalo ni jipya  lililofamnyiwa ukarabati  mkubwa   leo katikati ya jiji la Dodoma .

Akizungumza kwenye sherehe ya uzinduzi wa duka, Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Simon Karikari alisema duka iliyofanyiwa ukarabati ikiwa ni mkakati wa  upanuzi wa kampuni wa kuzileta bidhaa na huduma zake sehemu moja.

 Duka hilo jipya lililokarabatiwa miongoni mwa vitu vilivyomo ni pamoja na  sehemu ya watu mashuhuri (VIP) kwa ajili ya kuhudumia wateja ambao ni VIP na wale wanaohitaji huduma za ufuatiliaji wa  kasi, kaunta  zimeongezwa na eneo la  kufanyia majaribio  ambapo wateja wanaoingia wanaweza kufurahia uzoefu wa kwanza wa kujifunza jinsi ya kutumia bidhaa za Tigo kama vile simu za kisasa (smartphones) na bidhaa na huduma nyingine za mtindo wa maisha ya kidijitali kama vile  Tigo Pesa ambazo zinatolewa na kampuni. 

'Tigo imepania  kutumia  rasilimali zake zote ikatika  kuhakikisha kuwa wateja wetu wanapata huduma za daraja la juu  duniani, kuhakikisha ufanisi, wakati halisi wa majibu kwa maswali yao katika maduka yetu yote 52 ya huduma za wateja yaliyopo nchini, "alisema Karikari, na kuongeza  kuwa duka hilo  mpya Iimewekwa  vifaa vya kisasa, likihudumiwa na wafanyakazi waliopata mafunzo sawasawa na ambao ni wachapa kazi  ambao wako  tayari   kutoa huduma bora kwa idadi ya watu inayoongezeka kwa haraka jijini humo.

Akizungumza juu ya uendeshaji wake, Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini, George Lugata alisema kuwa duka hilo jipya la Tigo mpya litakuwa wazi siku zote saba za wiki.
"Kimkakati kuwepo kwa duka hilo eneo la katikati ya jiji kunafanya iwe rahisi kufikiwa na wakazi wa mji wa Dodoma, maeneo jirani  na watu wanaotembelea kitovu hicho cha nchi, " aliongeza Lugata.

Aliendelea kufafanua zaidi kuwa duka kubwa, la kisasa limekuwa pia linaenda bega kwa bega na mkakati wa Tigo kupeleka  huduma kwa  wateja kwa wakazi wa Dodoma kama mji ambao  unatarajia kuwa ‘ mlipuko’  wa idadi ya watu kufuatia uamuzi wa serikali kuhamishia shughuli zake za kiutawala  kutoka Dar es Salaam , na hivyo  kufanya mji wa Dodoma makao makuu ya nchi.
     
Duka lipo mkabala na mzunguko wa CDA kwenye sakafu ya chini ya Jengo la  CDA Barabara ya Uhindini katika Manispaa ya Dodoma,  na linatarajiwa kuhudumia  wateja zaidi ya 300 kwa siku.

No comments: