Tuesday, February 21, 2017

Serikali yaweka sawa Utaratibu wa kufuta Viroba nchini


Kufuatia kauli ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa aliyotoa tarehe 16/02/2017 huko Mererani, Mkoani  Manyara kuhusu kusitisha utengenezaji, uuzaji na matumizi ya pombe zinazofungashwa kwenye vifungashio vya plastiki kuanzia tarehe 1 Machi 2017; na kufuatia  Tamko la Serikali kuhusu dhamira hiyo lililotolewa Bungeni tarehe 2 Mei, 2016 na kwenye matangazo yaliyotolewa kwenye vyombo vya habari tarehe 01 Desemba, 2016, Ofisi ya Makamu wa Rais  inachukua fursa hii kutangaza utaratibu wa utekelezaji wa maamuzi hayo ya Serikali.

SBL yaanza kuuzaa bia Kenya


Dar es Salaam, Februari 20, 2017- Kwa mara ya kwanza, Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) imeanza kuuza nje ya nchi  bidhaa zake katika  soko la kikanda,  eneo la kwanza  likiwa ni nchi jirani ya Tanzania kwa upande wa Kaskazini, Kenya.

USAJILI WA TIGO KILI HALF MARATHON WAENDELEA JIJINI DAR ES SALAAM

 Mkazi wa jiji la Dar es Salaam, Edger Damian akijisajili kwa njia ya Tigopesa kwa ajili ya mashindano ya Kili Marathon yatakayofanyika Kilimanjaro hivi karibuni. Usajili huo ulifanyika mwishoni mwa wiki.

Msajili wa Kili marathon wa Tigo, Neema Misaji akimpa maelekezo ya kulipa kwa njia ya tigo pesa, mkazi wa Dar es Salaam, Iyan Balegele aliyekuwa akilipia kupitia huduma hiyo mwishoni mwa wiki.

Wananchi mbalimbali wakijisajiri ili kupata tiketi za Kilimarathon kwenye banda la Tigo katika viwanja vya Mlimani city mwishoni mwa wiki.

Wakazi wa Dar es Salaam, Eden Mbunde na Sheila Kombe wakimsubiri Msajili wa Tigo, Viola Mboya aliyekuwa akimalizia usajili wao kabla ya kuwakabidhi tiketi zao mwishoni mwa wiki.

WANAFUNZI WANNE CHUO KIKUU KIU- DAR WAKIFISHWA MAHAKAMANI KWA KUMKASHFU RAIS MAGUFULI WHATSAPP


Wanafunzi wanne wa Chuo Kikuu cha Kampala(KIU) kampasi ya Dar es Salaam, wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, kujibu shitaka la kusambaza picha za kumkashifu Rais John Magufuli kupitia mtandao wa kijamii wa WhatsApp.


Washitakiwa hao ni Amenitha Kongo(19), Maria Tweve (20), Agnes Gabriel(21) na Anne Mwansasu(21), ambapo wamepandishwa mahakamani hapo leo na kusomewa shtaka linalomkabili mbele ya Hakimu Mkazi Catherine Kiyoja.

MAHAKAMA KUU YAZUIA MBOWE ASIKAMATWE

Leo Februari 21, 2017 Mahakama Kuu imeamuru Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe asikamatwe hadi maombi yake kutokamatwa yataposikilizwa siku ya Ijumaa.

Kiongozi huyo wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni tarehe 10 mwezi huu alifungua kesi ya Kikatiba dhidi ya RC Paul Makonda, Kamanda Simon Sirro.

Aidha Mahakama imewaushauri upande wa mlalamikaji kurekebisha hati ya mashtaka kisha wairudishe tena siku ya Jumatatu.

Monday, February 20, 2017

FAUSTIN SUNGURA:MBATIA AJIMILIKISHA MALI ZA CHAMA


Faustin Sungura 

Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi  JAMES  MBATIA pamoja na Katibu mkuu wa chama hicho MARTINI DANDA wamepewa siku tatu kujiuzulu ndani chama hicho kwa madai ya kujimilikisha mali za chama.

            Hayo yameelezwa na aliyekuwa mmoja wa waanzilishi na waasisi wa chama hicho baada ya madai kuwa mwenyekiti wa chama hicho JAMES MBATIA kujimilikisha shamba la hekhari 56 lilipo Kiromo,Bagamoyo Mkoani pwani pamoja na nyumba 2 zilizopo Bunju B ambazo zote ni mali ya chama hicho.

TAMKO LA SERIKALI MCHEZO WA SIMBA NA YANGA


Ndugu Watanzania Jumamosi, tarehe 25/02/2017 saa 10.00 jioni Uwanja wa Taifa tutakuwa na mchezo mkubwa wa kati ya Simba SC na Yanga FC.


Ikumbukwe kuwa mchezo uliopita wa timu hizi uliochezwa kwenye uwanja huu tarehe 1/10/2016 zilitokea vurumai zilizosababisha Serikali kuufungia Uwanja kwa zaidi ya miezi mitatu. Vurugu hizo zilisababisha uharibifu wa miundombinu ikiwemo uvunjifu wa viti, mageti na mbaya zaidi baadhi ya watu walijerehuliwa.

Tunaomba waandishi na wadau wote tushirikiane kuelimisha umma wa wapenda michezo kuwa Michezo ni Furaha, Amani na Upendo.

MEYA WA JIJI LA DAR ES SALAAM AOMBA BUSARA ZA MASHEHE NA WAZEE KATIKA KULIONGOZA JIJI HILO


Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita,akisalimiana na Mwenyeji wake,Daluwesh Dume (katikati) kwenye hafla ya sherehe ya Maulid ya Mtume S.A.W iliyofanyika Mtaa wa Da Estate eneo la Kinondoni jijini Dar es Salaam jana.


 Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita akiwa na Diwani wa Kata ya Kinondoni,Mustapha Muro wakifuatilia kwa umakini sherehe hizo.
 Watoto nao hawakuwa nyuma katika shughuli hiyo.
 
 Mawaidha yakiendelea kwenye sherehe hiyo ya kuzaliwa kwa Mtume Mohamed S.A.W
 

WANACHAMA WA TANZANIA GIRL GUIDS WAFANYA USAFI MAGOMENI KOTA, COCO BEACH DAR

 Walimu na wanafunzi wa shule za Msimbazi na Mongo la ndege ambao ni wanachama wa chama cha Tanzania Girl Guids (TGGA), wakijitolea kufanya usafi katika viwanja vya Magomeni Kota, Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya shamra shamra ya maadhimisho ya wiki ya utoaji huduma kwa wahitaji.


Wanachama hao walioongozwa na Mwenyeikiti wa chama hicho, Profesa Martha Qorro pamoja na Katibu wa Taifa wa TGGA, Grace Shaba walifanya usafi katika viwanja vya Magomeni Kota na Ufukwe wa Coco.Walimu na wanafunzi kutoka shule za Mugabe, Urafiki, Mongo la Ndege na Msimbazi ambao ni wanachama wa TGGA walishiriki ipasavyo kwenye usafi huo.Pia baadhi ya wanachama wa TGGA walikwenda kutoa msaada wa vitu mbalimbali katika Kituo cha Taifa cha Yatima cha Kurasini, Dar es Salaam.

MKUU WA WILAYA YA KINONDONI ATANGAZA VITA NA WAVUVI HARAMU


Mkuu wa wilaya ya kinondoni,Ally Hapi ametangaza vita kwa watu wote wajihusisha na uvuvi haramu Ndani ya wilaya yake,baada ya kufanikiwa kumata nyavu haramu za uvuvi zenye thamani ya milioni 60.

Hapi ametangaza oparesheni hiyo Leo wakati alipokuwa kwenye ziara ya siku kumi katika Kata zote zilizopo kwenye wilaya yake yenye lengo ya kukagua shughuri mbali mbali za maendeleo.

Sunday, February 19, 2017

Utajiri wa Makonda Gumzo Mjini,Mateja waibua Vileo Vipya Dar,Lissu amkingia Kifua Mbowe Polisi,Majaliwa akasirishwa na Kiwanda cha Minjingu,Soma Magazeti Leo Jumatatu Feb 20,2017

MEYA WA DAR ES SALAAM AOMBA VIONGOZI WA DINI KUMUUNGA MKONO

NA CHRISTINA MWAGALA, Dar es Salaam
MEYA wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita amewaomba Mashehe na Wazee wa jiji kumuunga mkono katika shughuli anazofanya ili kuweza kutatua changamoto zilizopo katika jiji hili.

Meya Isaya ametoa kauli hiyo jiji hapa leo wakati wa maulidi ya kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume wao Muhammad Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam ambapo pamoja na mambo mengine amesema kwama jiji la Dar es Salaam bila dua za wazee, mashehe na viongozi wote wadini huwezi kuliongoza kutokana na changamoto zilizopo.

ACT WAZALENDO WAIBUKA NA USHAHIDI JINSI HALI YA CHAKULA ILIVYO MBAYA NCHINI KWA SASA


HALI YA CHAKULA NCHINI BADO NI MBAYA! SERIKALI ICHUKUE HATUA

Jana Jumamosi, Februari 18, 2017, Sekretarieti ya Kamati Kuu ya Chama cha ACT Wazalendo ilikutana katika kikao chake cha kawaida. Pamoja na mambo mengine, Sektetarieti ilipokea, kujadili na kuidhinisha Taarifa kuhusu HALI YA CHAKULA NCHINI kama inavyotolewa hapa chini.

1.       Mtakumbuka Januari 6 mwaka huu, wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Kata ya Nkome mkoani Geita, chama chetu kilieleza kwa undani juu ya tishio kubwa la baa la njaa linaloendelea kuinyemelea nchi yetu. Msingi mkuu wa taarifa yetu ile ulikuwa ni taarifa na takwimu mbalimbali za Serikali yenyewe juu ya hali ya chakula nchini. Baada ya Chama chetu kutoa taarifa husika, tuliiona Serikali kwa kila namna ikihaha kujikita katika kukanusha zaidi taarifa tulizozitoa, badala ya kujikita katika kutatua hali mbaya ya Chakula nchini katika wilaya mbalimbali zaidi ya 50 nchi nzima. Bahati mbaya hali ya chakula nchini haijatengamaa na Chama chetu bado hakijaridhishwa na hatua ambazo Serikali imechukua katika kuzuia tishio hili la baa la njaa nchini.

Saturday, February 18, 2017

MBOWE AWATESA POLISI,WAMSAKA USIKU NA MCHANA BILA MAFANIKIO

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam, limemtaka Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kujisalimisha Polisi mara moja kwa ajili ya Mahojiano yanayohusu vita vya dawa za kulevya baada ya juhudi za kumsaka katika makazi yake kushindikana huku simu yake ya mkononi ikiwa imezimwa 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Simon Sirro amesema Bw. Mbowe aliahidi kwenda mwenyewe juzi tarehe 15, lakini hakwenda lakini jeshi la hilo lilimtafuta usiku na mchana katika makazi yake na kumpigia simu lakini simu yake ilizimwa 
Mbunge wa Mbeya Mjini Mh.Joseph Othman Mbilinyi "SUGU"  amefanya mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa shule ya msingi Mwenge,Jijini Mbeya. Kwenye mkutano huo Sugu ametumia sehemu ya hotuba yake kuwashukuru wana Mbeya kwa kumchagua kuwa kiongozi wao kwa kura nyingi zaidi na kumfanya kuwa Mbunge, Sugu licha ya kuongea mambo kwa mapana kuhusu serikali ya Jpm kwa kuminya haki kwa vyama vya upinzani na kuzungumzia kero ya tabia ya viongozi baadhi kuingilia kazi za wabunge, amempongeza Rais kwa kuingilia suala la vita ya madawa ya kulevya akidai kuwa awali lilikuwa likifanywa kisiasa na sio kukomesha janga hilo. Amesema kupitia Uteuzi wa Kamishna wa kushughulikia madawa ya kulevya kumeleta mwangaza na yeye kama mbunge anamuunga mkono kwa hilo.
Alijibu swali la mwananchi Isaac Nk
oma akiuliza kuhusu Mikakati ambayo Halmashauri ya Jiji na Ofisi yake kama Mbunge juu ya suala la Ajira kwa vijana wengi wanaozidi kuongezeka mitaani wakitokea vyuoni na mashule, Mh.Sugu amesema ,,,"Hilo jambo ni mtambuka sana na jitihada binafsi zinahitajika kwa vijana hao ili wakati serikali ikiendelea na michakato ya ajira basi vijana waache kubweteka na kuwasihi kutumia muda vizuri kujiongeza na kutumia vipaji walivyojaariwa kujipatia riziki zao"

Aidha,wakiongea kwa nyakati tofauti Mh. Joyce Mwalalika Diwani viti maalum, Raphael Mwaitege katibu wa CHADEMA wilaya,Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Mbeya Mh.Joseph Mwachembe China Wa China wamewaasa wana Mbeya kuungana pasipo uoga ku Kukijenga chama na kushirikiana katika shughuli za maendeleo.

Aidha,Mwenyekiti huyo amewaonya vijana wanaotumiwa kisiasa kuharibu Amani kwenye mikutano ya hadhara kwani hata kwenye mkutano huo Vurugu ilitokea na kusababisha tafrani iliyokuja kusuluhishwa kwa Jeshi la Polisi kuingilia kati na kuufanya mkutano huo kuendelea na kumalizika salama.
 Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Mh.Joseph Mbilinyi akiwasili Uwanja wa Shule ya Msingi Mwenge kwa ajili ya Mkutano

MKUTANO WA HADHARA MBUNGE WA SHINYANGA MJINI,ATOA MSIMAMO KUHUSU NJAA,SIKILIZA HAPA

Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele (CCM) amefanya mkutano wa hadhara na kusikiliza kero za wananchi katika viwanja vya jeshi la Zimamoto na Uokoaji Nguzo Nane mjini Shinyanga. 

Mkutano huo ulioanza kwa wananchi kueleza kero zao kwa mbunge umehudhuriwa na mamia ya wakazi wa Shinyanga. 

Miongoni mwa kero zilizotawala mkutano huo ni kero ya bei ya maji kubwa,migogoro ya ardhi,jeshi la polisi kudaiwa kuwaonea waendesha bodaboda kwa kuwachapa viboko na uwepo wa mitaro isiyopitisha maji. 

Tatizo la njaa nalo likachukua nafasi yake huku wananchi wakiomba serikali iwapatie chakula cha bei nafuu kwani sasa kuna mfumuko wa bei za vyakula. 

Akizungumza wakati wa kujibu hoja za wananchi wa Shinyanga,mbunge huyo wa jimbo la Shinyanga mjini,Stephen Masele alisema ni vyema busara ikatumika kwa jeshi la polisi kuhusu ukamataji wa waendesha bodaboda huku akiwasisitiza waendesha bodaboda kuzingatia sharia zausalama barabarani. 

Mbunge huyo pia alisema wananchi wa jimbo la Shinyanga wanakabiliwa na njaa  hivyo kuna kila haja kwa serikali kutoa chakula kwa wananchi

KIPINDUPINDU CHAPIGA HODI JIJINI DAR ES SALAAM CHAUA MTU MMOJA WENGINE 12 WALAZWA HOSPITALI

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

 Na Dotto Mwaibale

WAKATI jiji la Dar es Salaam likiwa katika  mapambano ya kukabiliwa na dawa za kulevya jiji hilo limekumbwa na ugonjwa wa kipindupindu ambapo mtu mmoja aliyetajwa kwa jina la Ramadhan Kiumbo (maarufu kwa jina la Popo) mkazi wa Kibada Kigamboni amefariki kutokana na ugonjwa huo.

Friday, February 17, 2017

Hali ilivyokuwa baada ya waziri NAPE kuwasili Kariakoo leo Kufanya Msako


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (katikati) akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa Idara ya Habari - MAELEZO, Dkt. Hassan Abbas (kushoto) pamoja na maafisa wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), wakia katika oparesheni maalum ya kushtukiza la kukamata wafanyabiashara wanaodurufu kazi mbalimbali za sanaa nchini, katika eneo la Karikoo jijini Dar es salaam leo.

STAA ALI KIBA AKABIDHIWA TUZO YAKE YA MTV EMA

Hatimaye Alikiba amekabidhiwa tuzo yake ya MTV EMA – Best African Act aliyoshinda mwaka jana.
Staa huyo wa Aje amekabidhiwa tuzo hiyo nchini Afrika Kusini alikoenda kwaajili ya ziara yake ya huko.

TFF WATUMA SALAM ZA RAMBIRAMBI KIFO CHA BONNY


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetuma salamu za rambirambi kwa Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya kutokana na kifo cha mchezaji wa zamani Tanzania Prisons, Young Africans na timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’.


Taarifa kutoka Mbeya, zilizothibitishwa na uongozi wa Mkoa zinasema kwamba mchezaji huyo alifariki dunia usiku wa kuamkia leo Ijumaa Februari 17, 2017 kwenye Hospitali ya Wilaya ya Rungwe.

MSIBA MWINGINE KWENYE SOKA LA TANZANIA MCHANA HUU

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikito taarifa ya kifo cha Nahodha wa timu ya 94 Green Warriors, Ikongo Julius Mbaga aliyefariki dunia leo alfajiri (Februari 17, 2017) kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambapo alikuwa amelazwa.

KUELEKEA MCHEZO WA KESHO KATI YA YOUNG AFRICANS, N'GAYA CLUB


 


Maandalizi ya mchezo wa kesho wa kimataifa kati ya Young Africans ya Tanzania na Ng’aya ya Comoro, yamekamilika kwa asilimia 100.

Timu zote zipo Dar es Salaam, ambako Young Africans wao wameweka kambi kwenye Hoteli ya Zimbo iliyoko Kariakoo kwenye makutano ya mitaa ya Ndovu na Nyamwezi, Dar es Salaam.

Kwa upande wa timu ya N’gaya, yenyewe imefikia Hoteli ya Kaluganje iliyoko Mtaa wa Gerezani, Kariakoo wakati waamuzi kutoka Uganda, pamoja na Kamishna wa mchezo wanatarajiwa kutua leo.

VIONGOZI NA WANACHAMA 215 WA CHADEMA WAFUNGULIWA KESI MAHAKAMANI


CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema wanachama na viongozi wake 215 wamefunguliwa kesi katika mahakama mbalimbali nchini tangu kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. 


Chadema imesema wanachama hao wamepandishwa kizimbani katika jumla ya kesi 78 huku wengi wao wakinyimwa dhamana na wale waliopatikana na hatia, walipewa adhabu za vifungo bila ya kupewa fursa ya faini.

Thursday, February 16, 2017

MPYA--MCHEZAJI WA YANGA NA TAIFA STARS AFARIKI DUNIAMchezaji wa zamani wa Timu yanga na Taifa Stars Godfrey Bony amefariki Dunia kutokana na maradhi yaliyomsumbua kwa Muda Mrefu Mkoani Mbeya akilokuwa anafanyiwa matibabu.

Bony Taarifa za mwisho ambazo Mtandao Huu ulizipata alikuwa anasumbuliwa na Ugonjwa ambao Ulikuwa haujatambulika lakini Taarifa nyingine za watu wake wa Karibu zilieleza kuwa alikuwa anasumbuliwa na TB ugonjwa ambao ulimfanya kulazwa Hospitali ya Rungwe akiwa hawezi kufanya chochote hadi hapo Kifo chake kilipomfika.

Godfrey Bony enzi za uhai wake amewahi kuzichezea kwa mafanikio makubwa Timu za ,Yanga, Tanzania Prisons na Taifa Stars.

Taarifa zaidi zitakujia Hapa hapa 

Chadema yalia na Viongozi wastaafu,Manji kortin kwa kula unga,Yanga yamuokoa,Simba yaibamiza Simba ya africa (african lyon) Taifa.Soma magezeti ya leo ijumaa Feb 17,2017 hapa

Jana Waziri Mwakyembe alitishia Kukifuta chama cha wanasheria Tanganyika TLS,Sasa Hii ni Kauli ya Julius Mtatiro Muda Huu


Hakuna sheria wala kanuni kwenye Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) ambayo inazuia wakili ambaye ni mwanachama au kiongozi wa chama cha siasa kuwa Rais wa TLS.

TIMU YA NGAYA YA COMORO YAWASILI NCHINI KUMENYANA NA YANGA JUMAMOSI UWANJA WA TAIFA

 Wachezaji wa Timu ya Ngaya ya nchini Comoro wakiwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam leo mchana kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya Yanga utakaofanyika kesho kutwa Uwanja wa Taifa. Katika mchezo wa awali uliofanyika Comoro Yanga ilishinda bao 5-1.


 Picha ya pamoja na viongozi wao baada ya kuwasili.
Mmoja wa viongozi wa timu hiyo (kushoto), akitoa maelekezo kabla ya kuondoka uwanjani hapo. (Picha na blog ya habari za jamii.com)
Wachezaji wa timu hiyo wakiingia kwenye gari kuelekea hotelini walikofikia.

Wednesday, February 15, 2017

Sio Unga,Msanii Diamond afunguka kilichomfanya aitwe polisi na kupigwa Faini

 "Niliripoti kituo cha polisi kutokana na video clip tuliyopost naendesha gari bila kufunga mkanda, kuachia usukani, nimepewa onyo na Kulipa faini"-Diamond Platnumz


Makonda Hachomoki,afunguliwa kesi Sita,Diamond anaswa,Masogange naye ndani vita ya Unga,Gwajima amuombea manji wodini,Hakuna Bifu alikiba na Diamond,Simba waitangazia Vita Yanga,Soma Magazeti ya leo Alhamis Feb 16 2017

MPYA--NI KWELI MANJI ANATUMIA MADAWA YA KULEVYA,KESHO KUPANDISHWA KIZIMBANI--ASEMA SIRRO


Hatimaye imedhibitika kuwa mwenyekiti wa timu ya soka ya Yanga na tajiri mkubwa nchini Tanzania Yusuph Manji anatumia madawa ya kulevya na kesho atapandishwa kizimbani kwa Tuhuma hizo akiwa pamoja na watuhumiwa wengine wanaosikiliwa kwa sakata kama Hilo.


Katika Kipindi cha E Sport Kutoka radio eFM kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es salaam Kamanda  SIMON SIRRO amemdhibitishia Mtangazaji Maulid Kitenge kuwa Vipimo vya mkemia mkuu wa serikali alivyofanyiwa Tajiri huyo vinaonyesha kuwa ni Mtumiaji wa Madawa ya kulevya(Hakuyataja aina yake) na kusisitiza kuwa kesho mtuhumiwa huyo atapandishiwa kizimbani kujibu shitaka hilo.

Mwakyembe atembelewa na Uongozi wa TLS


Serikali imekiasa Chama cha Wanasheria cha Tanganyika (TLS) kibaki kuwa chombo cha kitaaluma cha kulinda weledi, viwango na maslahi mapana ya uanasheria na kisikubali kuyumbishwa na mihemko ya uanaharakati wa kisiasa isiyo na tija kitaaluma.

Akiongea na ujumbe wa TLS kwenye ofisi yake ndogo ya Dar es Salaam leo  (15/2/17), Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria, Dk.  Harrison Mwakyembe amesema TLS ibakie njia kuu kama ilivyo kwa vyama vingine vya kitaaluma nchini, isighilibiwe na michepuko.

KAMPUNI YA SIMU YA TIGO YAWAANZISHIA WATEJA WAKE KIFURUSHI KISICHO ISHA MUDA 'HALICHACHI'


 Meneja Chapa wa Tigo,  William Mpinga (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa kifurishi kisicho isha muda cha halichachi. Kulia ni Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael.
 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
 Mkutano ukiendelea.
Wapiga picha wakichukua taarifa hiyo.

LIGI KUU YA WANAWAKE SASA KUANZA FEBRUARI 26Ligi Kuu ya Wanawake ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) hatua ya 6 Bora ambayo ilikuwa ianze Febrauri 18, 2017 Uwanja wa Karume, imesogezwa mbele kwa muda wa juma moja.

Ligi hiyo sasa itaanza rasmi Februari 26, 2017 kwenye uwanja huohuo wa kumbukumbu ya Karume, Ilala mahali zilipo ofisi za TFF. Hii ni kutokana na sababu ambazo ziko nje ya uwezo wetu.

NI SIMBA, AFRICAN LYON KESHO ASFC UWANJA WA TAIFAKesho Alhamisi Februari 16, 2017 timu za mpira wa miguu za Simba na African Lyon zitacheza mechi yao katika Raundi ya Sita ya kuwania Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) yaani Azam Sports Federation Cup.

WAGANDA KUAMUA MCHEZO WA YOUNG AFRICANS V WACOMORO


Mchezo wa marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Young Africans ya Tanzania na Ngaya ya Comoro hatua ya awali utachezeshwa na Waamuzi kutoka Uganda.


Kwa mujibu wa taarifa kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), waamuzi hao ni Alex Muhabi Nsulumbi atakapuliza filimbi uwanjani.